Kitendo cha Waziri Gwajima kuagiza Mchungaji Gwajima akamatwe kinadhihirisha kuwa Serikali hii haiwezi kushindana kwa hoja

Sasa sisi tufanyeje? Maana hujaeleweka kabisa...!

Unless, tuambie umesikia nini kutoka kwa huyo Dr Hosea...
 
Nilidhani serikali hii itakuwa smart kwenye kushughulika na Gwajima (Mchungaji) lakini kitendo cha waziri wa afya kuagiza mchungaji huyo akamatwe badala ya kujibu hoja zake kinaendelea kuthibitisha kuwa tuko kwenye mwendelezo wa utawala usiokubali mawazo na hoja mbadala.Serikali ilipaswa itambue kuwa kumkamata Gwajima ni kuutangazia umma kuwa serikali imeumbuliwa na mchungaji huyo...
Anayeamini kuwa Christianity ndiyo dini ya kweli ya Mungu anaamini kwa dhati ya moyo wake kuwa yuko right. Vivyo hivyo wanaoamini kuwa Islam ndiyo dini ya kweli ya Mungu;

wanaoamini kuwa COVID-19 Vaccine ndiyo itakayomuokoa mwanadamu; au wale wanaoamini kuwa COVID-19 ndiyo itakayomuangamiza mwanadamu.

Tujifunze tu kuvumiliana na kuishi pamoja! Kila mtu yuko sahihi kwa mujibu wa uelewa wake na imani yake!
 
kwa maana swala la chanjo ni hiari na Gwajima ni mchungaji hivyo basi mchungaji amechunga kondoo wake kulingana na anavyojua wanahitaji kula nini na kuwaonya kuwa kitu fulani msile..

kutokana na 1 2 3 ,na sio kwamba askofu amewaambia watanzania wote wasitumie chanjo hapana amewaambia waumini wake na ndio maana hakuitisha mkutano na waandiahi wa habari ili kuzungumza swala la chanjo bali alitumia uwanja wa kanisa lake kuwaambia waumini wake.

Je serikali kuagiza gwajima akamatwe haioni kuwa wanakiuka tamko lao la uhiari wa kutumia chanjo? na ni kuingilia maswala ya dini na imani binafsi ya mtu!?.
 
Halafu wanapoona mwitikio kuwa Mdogo wasizani ni sababu ya Gwajima la hasha!

Baadhi ya waTZ wengi ni watu wa kupuuzia mambo, mtu anapewa miiko na daktari ili apone lakini anapuuza?!...
sasa ndugu yangu embu fikiria tukienda wote kuchanja na dozi zenyewe zimekuja 1M tu ukizingatia sisi tupo 50M+ nani atachanja nani ataacha.
 
Nilidhani serikali hii itakuwa smart kwenye kushughulika na Gwajima (Mchungaji) lakini kitendo cha waziri wa afya kuagiza mchungaji huyo akamatwe badala ya kujibu hoja zake kinaendelea kuthibitisha kuwa tuko kwenye mwendelezo wa utawala usiokubali mawazo na hoja mbadala...
Niliposikia tangazo la Waziri Gwajma kwenye tiivi,nikiwa migombani moivo,nikashtuka nikajiuliza mmm,kumbe hata balozi wa nyumba 10 anaweza kuwaambia jeshi la polisi,takukuru,tiss,magereza nakuamuru wanitafute wanikamate niende kuandika maelezo,nikajiuliza kirahisi hivyo tu.

Nikasema hapa tayari madaraka yameshalevya mtu.Nchi hii inakuwa kama haina taratibu na miiko ya uongozi,hata elimu ya siasa ya darasa la pili imetushinda.Hakuna mkuu wa Nchi,tupotupo tu.

Baadaye kumbe wapo wengi sana waliofikiri kama mimi badala ya utekelezaji,wakarekebisha na kushauri.Iweje leo hii kwenye majukwaa wala huna mamlaka hayo, unadhalilisha uongozi mzima na uonekane kwa wananchi kuwa hawajui wanachokifanya.Mimi nikafikiri hivi.Ingekuwa busara itumike.

Kuna Waziri wa Mambo ya ndani,Waziri wa Ulinzi na usalama wangeshirikishwa jambo hili,tena kimya kimya bila sisi wananchi wa kawaida kujua.Ona sasa mnavyolikoroga na kujibizana kwenye majukwaa.

UONGOZI NI DHAMANA.Leo umekalia kiti,kesho mwingine.Tuheshimu nafasi za wengine,nao wanaweza ndiyo maana wakapewa hizo nafasi.
 
Nilidhani serikali hii itakuwa smart kwenye kushughulika na Gwajima (Mchungaji) lakini kitendo cha waziri wa afya kuagiza mchungaji huyo akamatwe badala ya kujibu hoja zake kinaendelea kuthibitisha kuwa tuko kwenye...
Hoja za kitaalamu zimetolea sana ila watu hawaziamini na nadhani kwa sababu ni jana tu serikali hii hii ilizikataa hizo hoja ambazo wanazitoa leo. Kumbuka sampuli za mapapai, mbuzi nk. alichokifanya mwenda zake na watu wakashangilia. Watu walisahau kuwa kwenye computer huwa ni "gabbage in gabbage out". Huwezi kupata jibu sahihi katika research yeyote kama umekosea kukusanya data.

Tatizo Gwajima alitakiwa akae kimya asihamasishe watu especially kwa vile mwenyekiti wake akiungwa mkono na wengi ndani ya chama chao kupitia hamashauri kuu wanasema chanjo ni salama baada ya kujiridhisha kuwa ni salama. kuendelea kupinga si sawa kwani wengi wakisema ndiyo na wachache wakisema hapana inapita hoja ya ndiyo. Pili kuendelea kubisha na kumtusi boss wako ni insurbodination.

Wengine wetu tulikuwa tunashangaa na hoja zilizokuwa zinatolewa na tunashukuru kuwa serikali imebadili muelekeo. Kuna msemi unasema "better late than never". Huu ugonjwa haujawahi kuondoka nchini, na watu wamekuwa wakifa muda wote tokea ulivyoingia. Kwa vile taarifa zilikuwa hazitolewi watu wanadhani ugonjwa uliisha na haupo. Anyway ni jukumu la mtu binafsi kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya afya yake. Gwajiboy akae kimya asihamasishe watu aache watu waamue wenyewe. Kwani watanzania wote ni mbumbumbu!!!! Au anadhani yeye peke yake ndiye aliyesoma na mwenye akili!!!!
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom