Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Ni Kitendo cha kusikitisha sana kimejiri leo kwenye Mkutano Mkuu wa Yanga ndani ya Ukumbi wa DYCCC Chang'ombe, kumzomea Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Wilfred Kidao ambaye alikuwa Mwakilishi kutoka katika Shirikisho hilo.
Kwakweli hiki Kitendo si cha kistaarabu, ni Kitendo cha kihuni kwenye Mkutano wenye Heshima na Mustakabari wa Soka la Tanzania tena mbele ya viongozi wengine waalikwa ambao wanaheshimika sana nchini akiwemo mgeni rasmi Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na ni kukosa heshima kwa mamlaka yenye dhamana ya kuongoza mpira nchini Tanzania.
Viongozi wa Yanga acheni kupelekeshwa na mihemko ya mashabiki wasiojielewa. Kwani haya ndo matunda ya Makamu/Kiti kuita Press Conference na kuaminisha Mashabiki na Wanachama kwamba timu inaonewa madai ambayo hata Rais Mstaafu Kikwete alipinga kwenye Kubwa Kuliko (Yanga Day).
Mpira ni mchezo wa wazi Uwanjani, mnataka TFF wafanye nini? Wafunge mabao wao badala ya Sarpong ama mnataka TFF wasajili wachezaji wenye viwango wao badala ya Engineer? Au mnataka TFF waandae timu badala ya Viongozi?
Kwakweli Viongozi Jitafakarini, kisha mpige hatua mbele na muombe radhi kwa Katibu Mkuu Wilfred Kidao pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.