Kitendo cha Viongozi Kuinama mbele ya Mkulu ni Rasmi au kimeanza Awamu hii?

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,091
4,715
Nimekua najiuliza swali kila ninapoona mkutano wa mkulu akiongea na viongozi mbalimbali Ukumbi wa Kikwete. Ikitokea mkulu kamtaja moja wapo wa viongozi waliopo ukumbini katika hotuba yake lazima uyo kiongozi tajwa asimame halafu ainame hivi kuelekea kwa mkulu.

Huu utaratibu nimeuona sana kwenye drama za kale za kikorea, sasa najiuliza huu ni utaratibu rasmi wa ki protokali? na ulikuwepo awamu zote au ndo umeshamiri awamu hii?

Naelewa kusimama kama ishara ya kujitambulisha kama umetajwa ili wasiokujua wamuelewe mkulu, ila kitendo cha kuinama kusujudu huwa sijaelewa.

Kama kuna mtaalamu wa protokali anieleweshe.
 
Hata wao hawajui ni kwanini wanafanya hivyo ukiwauliza... Mie nimeanza kuona awahu hii, wanamwabudu zaidi ya aliyeko juu ya vyote.. Cheza na njaa, wewe... Si tu wanahofu ya kutumbuliwa, pia wanahofu ya misukosuko ya makando kando yao baada ya kutumbuliwa, hakuna aliye msafi huko. Na mkulu anajua hivyo.
 
Mungu mtu dikteta Jiwe lazima asujudiwe vinginevyo utakiona cha mtema kuni, nadhani hata wafalme kule nchi za ghuba huwa wanasujudiwa hivyo si vibaya tukajifunza na kuiga yale 'mazuri' ya nchi za wenzetu(sarcasm).
 
Hizo ni swaga tu, hakuna hata kanuni inayomtaka mtu kuinama kama kanisani tunavyofanya ukienda madhabahuni.
Kwani wewe umeona ktk awamu zote kuna awamu ambayo wateule wa mkulu walitumbuliwa kama awamu hii? Sasa kwanini watu wasinyenyekee kwa Dr. ambaye mkononi mwake ameshika mkasi wa kutumbua?
 
Ishu iko hivi:-

tapatalk_1558852188968.jpeg
 
Ni utaratibu wa Kawaida, hata kwenye vikao vya kikazi kama unataka utoke nje wakati mwenyekiti anaongea, unamuangalia na kuinama, ni kuonyesha kuwa unaheshimu kiti au mamlaka

Mkuu hawa vijana wa sikuhizi tukiwaambia wasome soft skills, office ethics, communication skills wanaona ni vitu havina maana, matokeo yake wanataka kuhoji hata vitu obvious. tatizo wanadhani pale wanainama kwa mtu, kumbe wanainama kwa position, kiti, mamlaka
Tuendeleee kuwapa elimu
 
Ni kubembeleza kibarua
Nimekua najiuliza swali kila ninapoona mkutano wa mkulu akiongea na viongozi mbalimbali Ukumbi wa Kikwete. Ikitokea mkulu kamtaja moja wapo wa viongozi waliopo ukumbini katika hotuba yake lazima uyo kiongozi tajwa asimame halafu ainame hivi kuelekea kwa mkulu.

Huu utaratibu nimeuona sana kwenye drama za kale za kikorea, sasa najiuliza huu ni utaratibu rasmi wa ki protokali? na ulikuwepo awamu zote au ndo umeshamiri awamu hii?

Naelewa kusimama kama ishara ya kujitambulisha kama umetajwa ili wasiokujua wamuelewe mkulu, ila kitendo cha kuinama kusujudu huwa sijaelewa.

Kama kuna mtaalamu wa protokali anieleweshe.
 
Labda kuna semina elekezi walipatiwa
Hata wao hawajui ni kwanini wanafanya hivyo ukiwauliza... Mie nimeanza kuona awahu hii, wanamwabudu zaidi ya aliyeko juu ya vyote.. Cheza na njaa, wewe... Si tu wanahofu ya kutumbuliwa, pia wanahofu ya misukosuko ya makando kando yao baada ya kutumbuliwa, hakuna aliye msafi huko. Na mkulu anajua hivyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom