Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,293
- 217,274
Nimetafakari na kujiuliza sana jambo hili , huyu mtu tuliyeaminishwa kwamba ni msaliti wa Taifa , akashambuliwa kinyama na kutelekezwa ili akafie mbali , kama haitoshi akavuliwa ubunge bila huruma na akatishwa asirudi nchini , bali pamoja na lundo la vitisho Lissu amerudi nyumbani kishujaa.
Cha ajabu ni kwamba kila anapopita kwenye kampeni zake za kuomba Urais watu wanajaa kupita kiasi , na cha kushangaza zaidi ni huko kanda ya ziwa ambako tuliaminishwa kwamba ni ngome ya watu wengine ndiko ilikovunjiwa rekodi ya umati kwenye mikutano yake , Katoro , Sengerema na Geita ni mifano hai ya hoja yangu
Swali langu ni hili , kwa umati huu unaojitokeza kwenye mikutano ya Lissu huko kanda ya ziwa ni kiashiria cha jambo gani ?
Hizi hapa ni picha za Geita , Mkoa unaosemekana alizaliwa Mgombea Urais wa CCM , jioneeni wenyewe .