Kitendo cha Spika Ndugai kuutangazia Umma mkopo wa Lema ni kinyume na katiba na sheria. Lema hana cause of action dhidi ya Ndugai na benki hapa?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Kitendo cha Spika Ndugai kuamua kutangaza mkopo wa Mbunge Mheshimiwa Lema hadharani kimedhihirisi jinsi Bunge linavyozidi kukosa ustaarabu.

Lakini pia kinyume na Katiba ya nchi ibara ya 16 na sheria inayosimamij mabenki wateja wao, zote hizo zilinda haki ya faragha.

Inawezekana Spika amejua Mkopo wa Lema ama kwa nafasi yake lakini pia inawezeka benki iliyomkopesha Lema imevujisha siri ya mteja wao.

Hoja yangu nikuwa Mheshimiwa Lema hana redress ya kisheria kuhusu huku kuikwa kwa maksudi kwa faragha yake?
 
Kunywa maji kwanza acha papara.....hebu jaribu kusoma ulichoandika ni sahihi kwa mtu mwenye busara.


Elimu, Elimu, Elimu
Lema, Lema! Hivi ninyi munadhani Wabunge ni malaika? Kwani kamutangazia nani? Mbona watumishi wengine mikopo inatajwa wazi ktkmaofisi yao. usiwe watumwa wa hiari kwa wabunge! Eti faragha, hiyo nayo ni faragha! nyoooooooor!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kinga ya kibunge inamlinda mkuu.

Lakini ni busara na hekima tu,alichokifanya Spika leo sio kitu kizuri sina hakika kama hata hao CCM wenzake wamefurahishwa nacho.

Nadhani ni vyema zaidi Spika akachukua likizo akapumzika Dr Tulia amsaidie. Kuna kitu naona hakiko sawa,amekuwa na hasira hasira sana.
 
Hamna uwezekano nje ya Bunge...kwa kuzingatia ibara ya 100 ya katiba ya JMT.
Labda kwenye kamati ya Maadili na Uongozi wa Bunge..nje ya apo hamna namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kinga ya kibunge inamlinda mkuu.

Lakini ni busara na hekima tu,alichokifanya Spika leo sio kitu kizuri sina hakika kama hata hao CCM wenzake wamefurahishwa nacho.

Nadhani ni vyema zaidi Spika akachukua likizo akapumzika Dr Tulia amsaidie. Kuna kitu naona hakiko sawa,amekuwa na hasira hasira sana.
Wamefurai kwani ujasikia makofi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom