Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi!. Watanzania Sasa Tugomee...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi!. Watanzania Sasa Tugomee...!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pascal Mayalla, Sep 25, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Nimeguswa na kitendo cha Mchungaji Christopher Mtikila kugoma kukamatwa na polisi bila arrest warrant, ni kitendo cha kustahili pongezi, kufuatia polisi wetu kutekeleza majukumu yao ya kipolisi kwa umbumbumbu wa hali ya wa sheria kunakopelekea ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu hadi kusababisha vifo vya raia wasio na hatia akiwemo Mpiganaji, Daudi Mwangosi!.

  Mara baada ya kushinda kesi yake ya uchochezi, kuna polisi mmoja wa cheo cha chini, alikwenda pale mahakamani na RB ya kosa liingine la jinai ambalo Rev. Mtikila anatuhumiwa kubomoa nyumba ya mtualipaswa kukamatwa!. Kwa kuanzia Mtikila alimbeza kuwa polisi huyo ni wa cheo cha chini sana kuweza kumkamata kiongozi wa Chama cha kitaifa!. Akamwambia yeye hana haja ya kukamatwa, akihitajika polisi, huwa anakwenda mwenyewe, hata Saidi Mwema hili analijua, sasa iweje uje unikamate as if mimi ni mhalifu?, akamgomea na kumwambia huwezi kunikamata wewe!.

  Ndipo Mtikila akamuuliza, si unajua mimi nazijua sheria!, haya basi naomba hiyo arrest warrant uliyopewa unikamate!. Polisi yule akatoa RB, Mtikila akamwambia hiyo ni RB, siyo arrest warrant, kama kweli umetumwa kunikamata, ulipaswa upewe arrest warrant ya kunikamata!. Mtikila akaondoka bila kuguswa na askari wote waliojazana mahakama ya Kisutu.

  Yule polisi akaishia kuwalalamikia polisi wenzake hawakumpa ushirikiano wowote ili hali amewaonyesha RB!.

  Lengo la pongezi hizi kwa Rev. Mtikila, ni Watanzania wengi ni wahanga wa unyanyasaji wa polisi kwa kutotambua haki zao!. Watu wengi wa kawaida akishatumiwa polisi tuu, wananywea na kujisalimisha, hali iliyopelekea polisi kufanya arrest bila arrest warrant, na wakati mwingine hufanya hadi serach bila search warrant kwa sababu wanaokamatwa hawajui haki zao!.

  Tena mtu akishikwa na polisi, na kuulizwa maswali, hujibu mbio mbio bila kuelewa kuwa unapokamatwa kwa kosa lolote, "you have the right to remain silence" mpaka upate legal reprsentation!. Its high time somo la uraia lifundishe haki za binaadamu in full tangu primary ili watu wajua raia ndio yuko juu ya kila kitu, hata rais wa nchi ni mtumishi wako, na polisi ndio kabisa, alipaswa kukulamba miguu!.

  Hata familia ya Daudi Mwangosi wanapaswa kulishitaki jeshi la polisi na kudai fidia ya kifo cha mpendwa wao, not only for loss of love, and loss of life, but loss of bread winner na serikali inapaswa kulipa fidia, waweze kuishi vizuri maisha yao yote, as if Daudi Mwangosi is still alive!.

  Kitendo hiki cha Mchungaji Mtikila Kugomea Arrest ni cha Kupongezwa, Haya Shime Watanzania Sasa, Tusikubali Kuendelea Kupelekwa Pelekwa, Tugomee hata ....

  Naomba kuwasilisha!.

  Pasco.
   
 2. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,662
  Likes Received: 5,256
  Trophy Points: 280
  Sitachoka kusikitika jinsi askari wa tanzania, tena wenye vyeo vya chini wanavyotumika pasipo hata kua na ufahamu. Hivi mnapokua huko mafunzoni ya awali huwa mnafunzwa nini?? Au ndio tuzidi kuamini kimbilio la walio feli ni....!
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  safi sana Mtikila....kaonesha njia nzuri..........
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sawa,nami nimemsikia leo kupitia habar za clouds fm,ila huyo ulomtaja hapa si mahala pake
  BAJABIRI
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bajabiri, nahisi kama sijakuelewa vile, naomba unifafanulie "hapa sii mahali pake" kivipi labda nitakuelewa?!.
  P.
   
 6. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Hebu tujuzwe pia namna ya kulishtaki jeshi na Polisi wanapomkamata mtu kwa kutumia RB ili na wao waadhibiwe kwa fidia so iwe sote tunafuata Sheria bila shuruti na kuwaonea wasiojua Sheria
   
 7. h

  hacena JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  tutambue kuwa kuna makosa polosi watakamata wakiwa na hati ya kukamata na kuna makosa utakamatwa pasipo hati, kuhusu marehemu Mwangosi ningeshauri familia yake ifungue civil case ile criminal jamhuri waendelee kushtaki.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Polisi wa Tanzania wengi hawajui wanachofanya. Nafikiri kuna kila sababu ya kuongeza mafunzo ya sheria na haki za binadamu ili waweze kupambana vizuri na changamoto zinajitokeza sasa hivi bila kuishia kuwa wahalifu.
   
 9. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,130
  Likes Received: 1,732
  Trophy Points: 280
  hivi kirefu cha RB ni nini vilee?
   
 10. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Halafu sio kila mtu hata kama una arrest warrant eti unakamata tu kama kibaka... Wako watuambao unawataarifu tu kuwa wanahitajika polisi basi watakuja tu.. may be kama ni kesi ya mauaji lakini hizi kesi za mbuzi eti mmeandamana bila kibali unamuarrest dk slaa tena mbele ya umati wa washabiki wake... si unatafuta balaa wewe?? kwani ukimtumia taarifa anahitajika polisi hatokwenda?? Sijui wanatumia nini kufikiri anyway!
   
 11. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Report Book
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  mkuu Pasco ninachofaham katika maswala ya kisheria kuna ukamataji wa aina mbili. Ukamatai wa hati ya kukamatia na uakamtaji usiokuwa na hati ya kukamatia.
  1. Ukamataji na hati ya kukamatia.
  Zipo 2, inayotolewa mahakaman ambayo mtikila aliidai, na Rb inayotolewa Kituo cha polisi ndo hiyo huitwa Hii inayotoka mahakaman huwa inatolewa baada ya mtu kupewa dhamana halafu akashindwa kuhudhuria mahakani. Au mtu amemdhamini mtu lakini mtu wake hafiki, hutolewa hati hiyo ili akamatwe asaidie kumpata aliyedhaminiwa. Lakini pia hutolewa kwa ajili ya kuwakamata watu wanaoaminika kuwa na ushahidi wa kukamilisha kesi lakini kila wakitumiwa (samansi) summons hawaitikii wito, ndipo askari hupewa hati hiyo kumfikisha mahakaman mtu wa aina hiyo.

  Kwa upande wa hati ya kukamatia inayotoka polisi, na baada ya mtu kumlalamikia mtu, sasa ili kukusanya ushahidi mtu sharti akamatwe afikishwe kituoni ili upelelezi uendelee kabla ya kufikishwa mahakaman. Polisi wanatakiwa kumshikilia mtu si zaidi ya masaa 24 kabla ya kupeleka mahakan, lakini masaa na siku huongezeka kwanza kwa ushahidi kutokamilika na mtu mwenyewe akawa hana vigezo vya kupata dhamana.

  KWA NINI MTIKILA ALIKATAA.
  Kwa maoni yangu ni kuwa, mtikila alijua kabisa kuwa hilo ni zengwe anaundiwa, kwani kama ni kustakiwa au kufunguliwa kesi, kwa nini wasubiri amalize kesi moja halafu ndo wamkamate? Kwani ilikuwa haiwezekani kumkamata kabla ya kwenda mahakani? By the way, watu ambao ni viongozi, kulingana na hadhi zao ndani ya nchi, huwa hawakamatwi, huwa wanapigiwa simu na hufika kituo cha polisi kusikiliza shtaka lake na mambo mengine hufuatia.

  Ndio maana wakati anamjibu askari huyo, alimwambia sijawahi kuitwa nikakataa sasa iweje wewe utumwe kuja kunikamata? na akamfanyia ubabaishaji kidogo halafu akasepa.

  Sasa kama na wewe Pasco ni mtikila, au una hadi sawa na mtikila, mtu akulalamikie, ifunguliwe kesi dhidi yako, askari aje kukuita kuwa unatakiwa polisi halafu ukatae, utakuwa unajisababishia fedheha tu, kwani najua utakuwa umewapa grounds za kukufanyia kitu. Epuka fedhaha, itika wito, kataa neno kwa taratibu zilizopo.

  yangu ni hayo tu.
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  RB=Rice + beans,
  RB=Report Book no. yaani ni kesi ya ngapi kufunguliwa kwenye kitabu cha polisi cha upokeaji taarifa.
   
 14. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  ndilo balaa alilolitaka askari huyo, lakini siyo yeye ni njaa. Nasikia posho na mshahara bado havijasomeka, sasa ukimpa vijisent anang'oa akili zote, anatanguliza njaa yake mbele mwisho wa siku fedheha tu.
   
 15. Mundungus Fletcher

  Mundungus Fletcher JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 327
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo la familia ya mwangosi kushtaki polisi ningeahkuru kama tungepata ufafanuzi legal framework nani na nani mwenye uwezo wa kuwasue polisi kwenye kifo cha Mwongosi. Niliandika post yangu nikiuliza the same question
  Link www.jamiiforums.com/jukwaa-la-sheria-the-law-forum/322342-je-nani-anaweza-kuwashtaki-polisi-walio-muua-mwangosi.html#post4612512
   
 16. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  naunga mkono hoja
   
 17. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi huwa nawatimuaga sijui mtikila aliniiga.
   
 18. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kweli maana askari alijua Mtikila alikuwa right ndo maana hakumkamata
   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  jogoolakigoma. tupe experience yako usije kuwa unatafuta sifa za kijinga.

  unaweza kukataa kuwekwa chini ya ulinzi kwa kuwa umemdharau askari aliyekuja kukukamata, askari kama anaweza sheria inamruhusu kutumia nguvu kiasi kukufikisha kituoni, lakini ni kwa baadhi ya makaosa ambayo anajua kabisa usipofika kituoni siku hiyo utatoroka. Na ukikataa kwa kutaka kuonesha wewe n noma, anashauriwa akupotezee, aende kwa kiongozi wake then kiongozi anatuma zile njemba zinazovaa kama maroboti, ninachofaham kuhusu wale watu ni kama wanavuta bangi, hawana kutoa taarifa, ni amri tu, na ukikataa unalo. nimeyaona sana kaka.

  Kama na wewe ni mtu maarufu, unaweza kumtimua kwa kuzingatia nature ya kosa unalotuhumiwa nalo na kutokuwepo uwezekano wa kukimbia. Mtu kama mtikila, atakimbia aende wapi?
   
 20. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Nini tofauti ya Search Warrant na Arrest Warrant. Na inatolewa na nani na katika mazingira gani???
   
Loading...