TANAPA, TAWA na Waziri husika walikuwa wapi.
Akiwa kwenye ziara Mkoani Katavi rais John Pombe Magufuli aliagiza Mamlaka ya Hifadhi za Wanyamapori nchini (TAWA) kuchimba bwawa na kujaza maji kwa ajili ya viboko wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
“Ninawaagiza TAWA kuanzia kesho wapeleke maji wachimbe bwawa wajaze maji. Wanyama hao wanatuingizia fedha nyingi, kwa nini tushindwe kuwatunza,” alisema Rais Magufuli.
Najiuliza, hadi kufikia hali hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii alikuwa wapi, hao TAWA na TANAPA walikuwa wapi.
Ndio kusema taasisi husika hazikuona kuwa hilo ni tatizo hadi rais aingilie kati, je kama asingepita sehemu hiyo Viboko wangeendelea kuteseka? Viongozi hao wamepewa madaraka, wamepewa vitendea kazi wana kila kitu na kila mwezi wanapokea mshahara kwa kazi hiyo walikuwa wapi kulishughulikia.
Ni wakati sasa kwa wahusika kuwajibika kwa kumsaidia rais kuliko kusubiri rais awajibike kwao.