Kitendo cha professor muhongo kukacha kula hotel alikopangiwa.. Ni mbinu nyingine ya kujilinda..?

Kwi kwi kwiii hivi Mwakyembe anapaka kiwi usoni siku hizi? Nimemuona jana hadi huruma kwakweli. Prof watch your back and watch it carefully....,.
 
Unacheza na magamba bora aanze kukimbia kuliko ngozi yake kugeuzwa kama ya pundamilia!
 
kwenye gazeti la mwananchi la leo kurasa ya 10 kuna habari inayosema professor muhongo alikataa kwenda kula chakula alichoandaliwa kwenye hotel ya mount meru na kwenda kula kwa mamalishe..

Habari inasema alipofika karibu na geti la kuingia hapo alibadili uamuzi na kuamuru apelekwe mahali atakapopata chakula cha kitanzania huku akisema haoni sababu ya kula vyakula vya bei mbaya wakati kuna watanzania hawana umeme..! Hata hivyo aliwaruhusu maofisa alioongozana nao waende wakale pale mount meru hotel..

Inasemekana hata wakati alipokuwa dodoma mke wake alimleta mpishi toka dar kwa ajili ya kuhakikisha professor muhongo anapata chakula toka kwenye “mikono salama”..

Swali kubwa la kujiuliza hapa.. Professor muhongo anaonekana dhahiri “ana-cover his back”.. Dhidi ya asiowafahamu.. Kina nani..? Jee anafahamu nini kuhusu mustakabali wa maisha yake..? Ameshadokezwa chochote kuhusu usalama wa maisha yake..? Serikali yake inahakikisha vipi usalama wake kutokana haya yanayotokea kwenye wizara ya nishati na madini..? Maana sio siri professor muhongo amejitengenezea maadui wengi ndani ya muda mfupi toka apewe uwaziri na kuyafanya yale ambayo ameyafanya..!

Nawasilisha..
ni vyema kujihami wasije wakamwikembe
 
Back
Top Bottom