Kitendo cha Mwakalebela kuita waandishi na kulalamika ni Ushamba

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Mimi ni shabiki wa Yanga kama nijulikanavyo hapa jukwaani.

Ila nimeshangaa kinoma kuona Mwakalebela akiitisha vyombo vya habari na kuanza kulalamika kuhusu kuonewa na waamuzi viwanjani, cha ajabu zaidi anasema kuwa Yanga itajitoa kwenye ligi endapo changamoto alizozisema zikiendelea. Binafsi ninaona ni ujinga wa kiwango cha juu zaiidi kwa kiongozi mkubwa kama yule wa klabu kufanya jambo kama lile la kijinga.

Ni kweli changamoto ya uamuzi imeonekana, lakini sio sababu ya Timu kushindwa kufanya vizuri mpaka uitishe vyombo vya habari na kuanza kuwalalamikia wengine kwa makosa yao wenyewe viongozi. Kushindwa kupata matokeo mazuri recently kumetokana na machaguo ya kijinga ya mwalimu na sio kwa sababu ya kunyimwa penati.

Ushamba huu iliwahi kufanywa na Haji Manara alipokuwa anaita waandishi wa habari akiwa na Flat Screen akionyesha jinsi Simba ilivyokuwa inanyimwa penati. Sasa inakuwaje kiongozi wa juu wa hadhi yake arudie kufanya ushamba wa aina hii?

Ametukera na kutuudhi wengi.
 
Mi najiuliza hivi yule Mwakalebela aliyekuwa Tff na huyu wa yanga ni mmoja, kama ni mmoja kwanini alipokuwa Tff alifanya kazi vizuri lakini alipokuja yanga amekuwa utopolo.

Tatizo linaweza kuwa yanga au Mwakalebela binafsi.
 
Tuliwaambia achaneni na mechi ya As Vita vs Simba, kwani inaweza kuwaathiri kisaikolojia hamkusikia....sasa na Morison ndo anazidi kuwakera unadhani mtu mzima Mwakalebela ataacha kudata?stay away from Simba guys kwa mustakabali wa afya zenu.
 
Daaah,zile tambo kuwa wanabeba ndoo zimeishia wapi jamani? Swala la morisson hawalizungumzii tena,hizi ni dalili kuwa dozi inawaingia sawa sawa.

Walianza kuwa mashabiki wa kila mpinzani wa simba kimataifa ila kila waliyemshabikia aliishia kutafunwa na mnyama dili likaharibika,sasa wameanza kutafuta vijisababu.

All in all yanga kikosi hakijitoshelezi,na nawataarifu tu mkijidanganya kujitoa ligi kuu mwende ligi ya zanzibar mtakutana kule na mnyama anaitwa mla ndege.
 
Pona pona ya yanga kurudi kwenye mstari ni sisi labda tupigwe 5 na wale waarabu hapa nyumbani lakini tukitoa draw au kushinda uto lazima wajitoe kwenye ligi kweli kama walivyo sema.yaani tume wa athiri ki saikolojia kweli na sasa tuna jionea wenyewe.
 
yanga imeathirika kisaikolojia kupitia mafanikio ya Simba wanayopitia sasa.

yanga yeye anawaza kumfunga simba badala yakuwaza kushinda michuano ya ligi.

Nia ya Mwakalebela ni kutafuta huruma kwa maamuzi na kupelekea waamuzi wakachezesha game kwa pressure zaidi ili yanga inufaike.
 
Wewe ulipost hii taarifa ndio mshamba mkubwa wewe kwa elimu yako ya masuala ya mpira utajilinganisha na Mwakalebela usimfundishe kitu cha kuongea utajilinganisha na mtu mwenye Masters mikia ni mikia tu ndio shida ya kuuza timu kwa wahindi Mo mhindi ceo ndio walewale meneja wa timu ya wanawake mtoto wa Mo hapi ndipo mtu mwenye akili angequestion hapo oo kwa sababu tunapata matokeo mazuri basi hivi uliisikia taarifa ya fedha ya simba kwa nwaka uliopita mmepigwa na hamjitambua kazaneni na hayo sio habari za Mwakalebela wewe kubishana na Mwakalebela ni sawa na mtoto wa darasa la nne kubishana na mwanafunzi wa chuo kikuu katika mambo ya Equestion
 
Jifunze kuandika ukizingatia comma na nukta ewe utopolo.
 
Mi najiuliza hivi yule Mwakalebela aliyekuwa Tff na huyu wa yanga ni mmoja, kama ni mmoja kwanini alipokuwa Tff alifanya kazi vizuri lakini alipokuja yanga amekuwa utopolo.
Tatizo linaweza kuwa yanga au Mwakalebela binafsi.
Kwani hao TFF si ndio wana hujumu mpira wa Tanzania.Ivyo alivyo ndo inatoa picha halisi ya uozo wa shirikisho au wauaji wa mpira wa Tanzania
 
Wewe ulipost hii taarifa ndio mshamba mkubwa wewe kwa elimu yako ya masuala ya mpira utajilinganisha na Mwakalebela usimfundishe kitu cha kuongea utajilinganisha na mtu mwenye Masters mikia ni mikia tu ndio shida ya kuuza timu kwa wahindi Mo mhindi ceo ndio walewale meneja wa timu ya wanawake mtoto wa Mo hapi ndipo mtu mwenye akili angequestion hapo oo kwa sababu tunapata matokeo mazuri basi hivi uliisikia taarifa ya fedha ya simba kwa nwaka uliopita mmepigwa na hamjitambua kazaneni na hayo sio habari za Mwakalebela wewe kubishana na Mwakalebela ni sawa na mtoto wa darasa la nne kubishana na mwanafunzi wa chuo kikuu katika mambo ya Equestion
Mwaipopo /mwakalebela akili zenu zinafanana
 
Hawafanyi hivi kwa makusudi, huu ni mkakati ili waamuzi waanze kuchezesha kwa hofu mechi zao na wao wapate faida.
IMG-20210219-WA0000.jpeg
 
Wewe ulipost hii taarifa ndio mshamba mkubwa wewe kwa elimu yako ya masuala ya mpira utajilinganisha na Mwakalebela usimfundishe kitu cha kuongea utajilinganisha na mtu mwenye Masters mikia ni mikia tu ndio shida ya kuuza timu kwa wahindi Mo mhindi ceo ndio walewale meneja wa timu ya wanawake mtoto wa Mo hapi ndipo mtu mwenye akili angequestion hapo oo kwa sababu tunapata matokeo mazuri basi hivi uliisikia taarifa ya fedha ya simba kwa nwaka uliopita mmepigwa na hamjitambua kazaneni na hayo sio habari za Mwakalebela wewe kubishana na Mwakalebela ni sawa na mtoto wa darasa la nne kubishana na mwanafunzi wa chuo kikuu katika mambo ya Equestion
Mkuu, weka vituo basi, maana unavyoandika inaakisi jinsi ulivyo na hasira
 
Wewe ulipost hii taarifa ndio mshamba mkubwa wewe kwa elimu yako ya masuala ya mpira utajilinganisha na Mwakalebela usimfundishe kitu cha kuongea utajilinganisha na mtu mwenye Masters mikia ni mikia tu ndio shida ya kuuza timu kwa wahindi Mo mhindi ceo ndio walewale meneja wa timu ya wanawake mtoto wa Mo hapi ndipo mtu mwenye akili angequestion hapo oo kwa sababu tunapata matokeo mazuri basi hivi uliisikia taarifa ya fedha ya simba kwa nwaka uliopita mmepigwa na hamjitambua kazaneni na hayo sio habari za Mwakalebela wewe kubishana na Mwakalebela ni sawa na mtoto wa darasa la nne kubishana na mwanafunzi wa chuo kikuu katika mambo ya Equestion
Acha dharau, toa na wewe maoni yako tuyaone.. mikia mikia unatuwaaza na bado!
 
Back
Top Bottom