Hivi karibuni, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na Baraza Kuu la vijana Hussein Bashe alizungumza na waandishi wa habari na kumshambulia Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe kuwa ni mnafiki, asiyefaa hata kwa ubalozi wa nyumba kumi na akaapa kupiga kampeni ili Waziri huyo asichaguliwe kuwa Mjumbe wa NEC kupitia kapu. Hata hivyo jitihada za kutaka Membe asichaguliwe, zilishindwa kwani alishinda japo Bashe alijitokeza na kubeza ushindi huo kuwa ni mdogo na kazidiwa na makada vijana ikiwa ni pamoja na Januari Makamba.
Kisha akabainisha kuwa anamuunga mkono Edward Lowassa anayetajwa kuwania urais 2015 kupitia chama hicho. Wengi tulitarajia kumuona Membe akiibuka kumjibu Bashe lakini siku zinaenda, hatuoni Membe akifanya hivyo. Sasa nauliza, je ukimya wa Membe;
1. Unaonyesha kuwa kampuuza Bashe na maneno yake?
2. Unaonyesha busara na hekima?
3. Unaonyesha uvumilivu?
4. Kamuogopa Bashe?