Kitendo cha Mbatia kumfungulia Kesi Halima Mdee je anajua kuwa anafanya kazi ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitendo cha Mbatia kumfungulia Kesi Halima Mdee je anajua kuwa anafanya kazi ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Joblube, Apr 21, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakuna kitendo kilichonishangaza kama cha Jemsi Mbatia kufungulia kesi H. Mdee hasa kwa kuwa wote wanajiita wapinzani na lengo lao ni kuitoa CCM madarakani. Kitendo kile kinanifanya kutambua uwezo mdogo wa baadhi ya wanaojiita wanasiasa, kwa sababu mimi natoka jimbo hilo na kama kweli Mbatia angelikua na uwezo wa kiuongozi angepaswa kuwa na ulewa kidogo tuu usihitaji shahada yeyote kuwa hata leo hii uchaguzi wa jimbo la kawe ukirudiwa hana uwezo wa kumshinda H. Mdee kwa sasa jinsi anavyokubalika nasisitiza kwa sasa. Hili nimeliona wakati wa kampenini na hata sasa kule site wanasema Mbatia hawezi kushinda anafanya kazi aliyotumwa na CCM.

  Pili angepaswa kujua kuwa kitendo cha kumfungulia kesi mbunge mwenzake wa upinzani kinafanya aonekane yeye anafanya kazi kwa kivuli cha CCM hivyo kumpunguzia heshima kwa wanaounga mkono upinzani. Hawa ndio wanasiasa wa tanzainia wenye kudai wana sera mbadala wa hizi za CCM lakini jambo dogo kama hili hawawezi kusoma alama za nyakati.

  Tujadili
   
 2. S

  SunStrong Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yule ni nccr manunuzi
   
 3. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ..Mkuu, nimeipenda hii! Chukua Tano! :A S thumbs_up:
   
 4. J

  Joshua Bukuru Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Mimi nadhani huu ni uelewa mdogo wa kwako. Mbatia anayo haki ya kushitaki pale taratibu, kanuni na sheria za uchaguzi zinapokiukwa. Kitendo cha yeye kwenda mahakamani ni haki yake na tambua kuwa hizi ni tuhumu na mahakama haijamtia Mdee hatiani basi tusubiri tuone haki hii itakwenda kwa nani, kwa sababu hili ndio jukumu la msingi la mahakama. Tusiwe tunaenda mbali wakati mwingine kwa sababu kujadili mambo yaliyopo mahakamani ni kuingilia uhuru wa mahakama. Tuziache mahakama zifanye kazi zake lakini kumbuka kuwa pia Mbatia anayo haki ya kushtaki pale anapoona inamfaa kufanya hivyo, na hili hajatumwa na ccm kama unavyodai.
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwani hamjui Mbatia anawakilisha mawazo ya ccm singilizeni hata maongeze yake kwenye makangamano .
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono. Wapinzani wanaipinga CCM na wapinzani wanapingana pia wao kwa wao. Haiwezekani kuwe na ukiukwaji wa taratibu (tuhuma) halafu mtu aliyetendewa anyamaze kimya ati kwa kuwa katendewa na mpinzani mwenzake, alaa!! Wapinzani wanapingana kwa kuwa hakuna makubaliano ya kuachiana majimbo na sera zao pia zinatofautiana ndio maana CHADEMA hawakumuachia Kafulila atambe peke yake kule kigoma japokuwa alikuwa akikubalika. Tuache sheria zichukue mkondo wake na wala sio kujificha katika kichaka cha Upinzani huku wapinzani wengine wakiwa hawatendewi haki.
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hamkutuhumu alipogombea leo mnamtuhumu kwa kwenda mahakamani! Aliwekeza hela nyingi bwana. Lazima arushe mateke angalau.
   
 8. KABAVAKO

  KABAVAKO JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama Mbatia aligundua kuwa Halima Mdee alishinda kwa kukiuka sheria ni lazima amshitaki, na hiyo ndio demokrasia yenyewe. Angalia sana! Unaweza kudai kuwa unatetea Demokrasia kumbe ndio unaizika, kwa kudhani kwamba kwa kuwa wewe ni mpinzani basi watu wakuunge mkono hata unapovunja sheria.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu uko sawa. Naanza kuhisi kwamba humu ndani ya forum tunakuwa watovu wa demokrasia. Ni vema tukajipambanua kwa kutetea demokrasia na wala si ushabiki wa vyama na watu. Vyama havitatufikisha kokote. Mimi kwangu vyama katika nchi hii kuanzia CCM, CHADEMA, CUF, UMD, Siju MAKINI, utitiri mwingine, n.k ni magenge tu ya wasaka tonge!!
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  lazima kujua kuwa ana haki kisheria kudai haki yake anayohisi kuwa ameporwa.

  Wapeni nafasi na mahakama itaamua mbivu na mbichi
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wacha afungue kesi ashindwe tena, afungue tena ashindwe tena hadi 2015... Mbatia ana haki!!! Lakini si dhani kama kila haki ni kukimbilia mahakama
   
 12. N

  Nanu JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama ana madai ya maana anahaki ya kwenda mahakamani!!!
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mwamume kwetu mwiko kumpeleka mwanamama mahakamani kweli.:whoo:
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwenu pazuri!! Ingekuwa kwetu mwanamke asingegombea akasimama jukwaa moja na wanaume!!
   
 15. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  Anapoteza muda wake bure..snitch huyo.
   
 16. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  taratibu zinazolalamikiwa zisije zikawa ni zile za jinsi wapiga kura walivyolinda kura zao zisi"PORWE" sijui Msarendo na Kimbunga mtasemaje
   
 17. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mbatia si wa kwanza kufanya kazi aliyotumwa na CCM. Lamwai naye pia....
   
 18. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mbatia ni bwabwa, yaani punga linahemewa kisogoni
   
 19. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tuache unafiki, kama Mbatia na ushahidi wa kutosha na anaamini kuwa Mdee hakushinda kihalali ni haki yake kwenda mahakamani, kuwa mpinzani na kuwa na lengo la kuiondoa CCm madarakini haimaanishi kuwa zifanyike rough kufikia malengo we need fair play and that applies to both CCM and oppositions! go Mbatia it is your right!
   
Loading...