Kitendo cha kutoa mimba ni ukatili mkubwa sana. Tafadhali usitoe mimba hata kama unapitia wakati mgumu

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,563
188,760
Habari.

Kuna mambo ya ajabu sana kwenye jamii zetu na kila kukicha yanazidi kutokea na kuna siku yataonekana ya kawaida.

Mada inaweza kuwa na uzi wenye maneno yasiyofaa ila ndio maneno ambayo hata vitabu vya dini hutumia hayo.

Mwanamke kuwa na ujasiri wa kutoa mimba hapa tukiwatoa wale waliandikiwa na daktari kimatibabu na kiafya imetakiwa kuwa hivyo.

Mwanamke kama ameweza kutoa mimba kwa kuamua yeye / kushawishiwa na mwanaume wake na kukubali huyo ni zaidi ya kahaba au malaya kabisa.

Naweza kuwapa mfano mmoja ambao nilikutana nao moja kwa moja. Kuna mwanamke mmoja niliwahi kukutana nae katika harakati za hapa na pale.

Kwa kweli nilitumia kila njia ya kuwa nae takribani mwaka mzima alisema yupo kwenye mahusiano hivyo basi kuna wakati niliendelea kufanya mambo yangu na kuachana na upande huo wa mahusiano.

Mambo yalikwenda baada ya mwaka mmoja na miezi miwili yule mwanamke sijui nini kilitokea ila kwa maelezo yake mambo hayakuwa sawa na mahusiano yake.

Ikafika hatua za mwanzo alifanikiwa kutoa ile mimba na baada ya hapo mahusiano yao yalivunjika ila kiafya aliteseka kidogo hadi kurudi sawa.

Kutokana na ukaribu nae niliona kabisa alihitaji msaada wa karibu hivyo nilijitolea kwenda nae hospital na kuwekewa ratiba ya kumuona daktari (Nilikuwa nafahamiana nae haikuwa ngumu sana kutusaidia kwa swala hilo la kufanyiwa usafi).
Alifanyiwa usafi na kupewa dawa kwa muda mara tatu ndani kama ya week tatu mfululizo.

Alifanikiwa kurudi katika hali yake kama kawaida na maisha yakaendelea. Ila mambo kwa upande wake yalibadilika kwa kiasi kikubwa na kutaka tuwe kwenye mahusiano.

Aisee! Huyu mwanamke ki ukweli nilimsaidia lengo kubwa arudi katika hali yake si kwa ajili ya mahusiano.

Maana mwanamke aliyetoa mimba kwa upande wangu namuona ni zaidi ya kahaba / malaya.

Wanawake wote kuwekeni makini sana kwenye maamuzi yenu hata mwanaume akushauri vipi/ hali ya maisha ngumu kiasi gani chonde chonde usitoe mimba.

Kutoa mimba ni kujikubali na kutwaa cheo cha ukahaba na umalaya.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu.
 
Kweli kabisa ndio maana kuna laana huwa zinawapata mfano mwingine akishatoa mimba basis ujue kizazi au uzao wake utamsumbua
Uzazi kusumbua hauhusiani na kutoa mimba, Kuna watu wametoa mimba zaidi ya kumi na Wana watoto Hadi mapacha, Kuna watu hawakuwa wahuni na hawajatoa mimba ila ndo hawajashika ujauzito
 
As expected wengi watakaokuja hapa ni wanaume na wanakuja kutoa lawama na kuwapa wanawake majina hayo Kama kahaba. Shameless indeed.

It's easier to write behind your keyboard and point filthy fingers without being honest about putting a woman or two in such a situation.

King James Version, John 8:7 Jesus Christ said to the crowd let he who has not sinned, cast the first stone.

Wangapi mumenunua P2, wangapi mumetoa hela ya microprostol, wangapi mumewapa wanawake mimba na kuzikataa? Then here you are.....
 
Wangapi nimenunua P2, wangapi nimetoa hela ya microprostol, wangapi mumewapa wanawake mimba na kuzikataa? Then here you are.....
Tusamehe basi Karucee, we've sinned and ask for forgiveness. Hayo uliyotaja, pills, kutoa pesa za kufanya abortion, kukataa mimba nk most men tumeshiriki...
He who hasn't sinned should be the first to cast a stone!
 
Uzazi kusumbua hauhusiani na kutoa mimba, Kuna watu wametoa mimba zaidi ya kumi na Wana watoto Hadi mapacha, Kuna watu hawakuwa wahuni na hawajatoa mimba ila ndo hawajashika ujauzito
Toa mifano hai tafadhali, nani huyo katoa zaiid ya mimba 10 kisha akapata mapacha?
 
Mbona huko mitaani hawasemwi! Toa mimba for health reasons, otherwise jifungue msaidiane kulea. I'd never consider my child a bastard hata kama atapatikana pasi na ndoa!
I wish men's wakue na huo mtazamo
 
Kosa halihalalishwi kwa kosa mkuu.

Jaribu kuishi humo mkuu.
As expected wengi watakaokuja hapa ni wanaume na wanakuja kutoa lawama na kuwapa wanawake majina hayo Kama kahaba. Shameless indeed.

It's easier to write behind your keyboard and point filthy fingers without being honest about putting a woman or two in such a situation.

King James Version, John 8:7 Jesus Christ said to the crowd let he who has not sinned, cast the first stone.

Wangapi mumenunua P2, wangapi mumetoa hela ya microprostol, wangapi mumewapa wanawake mimba na kuzikataa? Then here you are.....
 
Uzazi kusumbua hauhusiani na kutoa mimba, Kuna watu wametoa mimba zaidi ya kumi na Wana watoto Hadi mapacha, Kuna watu hawakuwa wahuni na hawajatoa mimba ila ndo hawajashika ujauzito
wengine ni laana sio wote ambao in matatizo ya uzazi mengine yanachangiwa na MTU mwenyewe
 
Back
Top Bottom