Kitendo cha kumsuta mbunge nje ya bunge tafsiri yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitendo cha kumsuta mbunge nje ya bunge tafsiri yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NgomaNgumu, Jul 28, 2011.

 1. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kitendo cha kumsuta mbunge wa CCM ndugu Deo nje ya bunge, kwakweli sijui kinatufahamisha nini kuhusu waheshimiwa wabunge wetu.

  Kwa ujumla haionekani kua ni professional bali ni sawa na kumvunjia heshima mtu na kumnyima uhuru wa kutoa maoni wakati akiwa bungeni. Kitendo kilichofanyika ni hatari na ni vyema kikakemewa no matter huyo mbunge alizungumza nini.

  Kwanini kama mtu yoyote alikua na swali asiulize ndani ya bunge? Baada ya kutoka nje ya bunge sio professional kuanza kubishan nje ya bunge ambapo maoni yatakayotolewa pale after all hayatakua na maslahi yoyote na wananchi.

  Ni vizuri kutofautisha kati ya vitendo vya mitaani na vitendo vya watu ambao wamepewa dhamana na wananchi kutetea maslahi yao.
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Wamemuonea huruma kumsuta, wangemtandika mangumi na kumng'oa meno angalau mawili kilaza wa magamba yule. kwani amepelekwa bungeni kwenda kuzomea? mbwa kabisa huyu.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ngomangumu unajua kilichotokea au unaandika tu kwa kuwa umepata nafasi ya kutumia computer ya ofisi
   
 4. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tuelezee ndugu binafsi sijaona kwahiyo sielewi vizuri,
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Unajua, mbunge wa magamba ndo ana fujo. Wewe watu wametoka unakwenda kwao na kuwaambia waache utoto! Yeye fili ndo alishindwa kuwa mstaarabu, mbona wengine hawakusutwa kwanini iwe yeye! Magamba waache umagamba wao bwana, sasa kwa kusema vile alitaka wamchekee tuuu!
   
 6. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Deo ni natural mjivuni, kwapa,magumashi.....huyu alijiandaa sana kuupata uwaziri na mkakati alonao ni mchuchuma -liganga vimrejeshe mjengoni....

  Anatamani leo kesho mzee majiyatanga a rip aikwae ile fursa ya lobbyist general wa ile project.

  Hahahaaaaaaaaaa.....deo bwana, lakini hao wabunge wamempatia tiba....lakini wamtembelee kule jimboni sasa anamhofia pindi chana
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Huyo Deo ndio alianza kuwaita wenzake watoto baada ya kumuunga mkono mbunge mwenzao aliyetolewa nje. Ungekuwa wewe ungekubali? Na ni nani mgomvi kati yao? Ningekuwa mimi ningerusha ngumi kabisa achana kumsuta.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa maksudi mazima huyu mbunge wa CCM (Deo) aliwafuata wabunge wa upinzani nje kuwatukana! Kumbuka wabunge hawa wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi walikuwa wanajadiliana wao kwa wao, hawakumuutia wala hawakuhitaji mchango wake Deo.

  What rights has he got to meddle into other people's affairs? Deo ana busara gani mpaka ajione anaweza kuwapa somo wabunge wenziwe? Kinamhusu nini kwa Wenje kutolewa nje? Yeye ni mwenyekiti wa mjadala? Anajuwa kanuni za bunge kushinda wabunge wa upinzani? Who the hell does think he is?

  Next time wamtandike mangumi, liwalo na liwe. Wanafiki kama Deo wametuchosha.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,764
  Trophy Points: 280
  huyu si alitaka kufa kwenye maji akiwa amepanda ngarawa? ameshindwa kuwapelekea wananchi wake boti ya maana? anawalamba ccm miguu tu huku wananchi wake wanakufa kwa njaa
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa yangu jana alinishangaza sana. Ni class mate wangu pale Forest Hill Moro, alikuwa mpole na very analytical na nimeshangaa jinsi amabavyo amefanya jana kuwafuata wenzake na kuwaponda. Ukiwa Mbunge wa CCM, kweli unapoteza uwezo wako wa kufikiri.
   
 11. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  Unajua ukipewa kazi ya kufundisha chekechea hata kama ni professor au Dr. huwezi kubehave kama unavyhokuwa na wanafunzi wa university, no!

  Ni lazima na wewe ujigeuze ufanane nao ili mambo yaende na nadhani wabunge wa upinzani sasa wanalazimika kujifananisha na hao 'chekechea' ili mambo yaende lakini sio busara wapinzani kukubaliana na ccm hata pale wanaposema "1+1=11".

  That is an alternative way of dealing with the magambaz
   
 12. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ngomangumu, jina lako linamaanisha jinsi vile ulivyo? Nauliza tu.

  Unajua kuwa duniani hakuna profession ya ubunge? Unajua kuwa mabunge duniani yanakusanya watu wa professions mbalimbali?

  Tafuta kujua kwanini alikuwa akisutwa kabla ya kumwangalia namna alivyowekwa kati mmagamba huyo.
   
 13. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JIMBO la Mheshimiwa Deo litakuwa wazi hivi karibuni.
   
 14. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  yatawashinda mtasemaaaaaa mpaka makoo yawakauke mnataka ndio yeye hamtaki ndio yeye.ondoeni chuki zenu hakuna binadamu asie kosea,kama amekosea chamsingi nikumelewesha sio kumtupia lawama na vijembe.
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hii mipasho yoote kaisababisha jk tuuuu!
  Wacha tuseme bwana, ila umesahau yeye ndo aliacha kuwatolea vijembe wenzake!?
  Magamba wepesi wa kusahau eeeh!
   
 16. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Semeni lakini msizue,nyie hakuna hata anaeongea jambo la maana hata moja yote mnaongea pumba2,kwani hana mazuri aloyafanya? hamumsifu mtu mpaka afe,mnalo hilo linawasokota ndani ya roho.
   
 17. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumsuta Filikunjobe sawa tu, jimboni wanamsuta, Mkewe nae anamsuta na sasa wabunge... hivi hadi hapo hajajua tu kwamba ana matatizo?
   
 18. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa Watu waliolelewa maadili ya Kiuanaume au Kiumeni kamwe picha ya Deo sio tu hadhi yake ya Ubunge bali pia kwa hadhi yake kama Mwanaume ni aibu kwa Mwanaume Mzima lijari kusimama akilumbana na wakina Mama wengine ni hadhi ya Mama yake kama yule Mama Kaihula [Mbunge Viti Maalumu Chadema] aliyekuwa anamwambia akashughulikie matatizo ya Wananchi wake juu ya mradi wa makaa ya mawe na chuma Linganga na Mchuchuma ambako mpaka sasa hawana majibu ya tatizo hilo.Nimeona aibu mimi kama Mwanaume kuona Mwanaume Mwenzangu akipewa Ukweli kupitia mipasho ya kinamama kwa kutumia lugha ya Mwili ya wakina Mama wanayotumia wakiwa wanalumbana mitaani yaani kwa kiswahili KUSUTANA.

  Wabunge aina ya Deo ndio hao ambao tunasema CCM ilifanya makosa kuwapa dhamana ya kugombe ubunge kupitia tiketi ya CCM.Sijui ana elimu ya kiwango gani.Anajua dhahili kuwa wabunge wa Chadema walitoka nje wakiwa wametoka na ghadhabu kisha yeye pasipo fikra na busara anawafuata akiwa na ile ile akili ya VIONGOZI walio wengi ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI kuwa daima wao wako sahihi,na si vinginevyo na kuwaongezea kejeri za kuwatuhumu kuwa ni wakolofi na wasiofuata kanuni.

  Ingekuwa imetokea mafichoni tungesema hatujui ila Watanzania wameona kupitia Luninga nini kimetokea.Kwa ujumla Deo alichofanya ni kuwazodoa [Provoke].Ni tendo lisilo la kiungwana tena limemzalilisha sana kwa watu waelevu [Intellectual] wamempimia kijiko na si koleo.
  Hatimae tunamuona kwenye televisioni yuko na kinamama ambao ukiwangalia wanavyolumbana nae dhahili katika lugha ya mwili ya wakina Mama [Body language] unaona dhahili ni kama wakina mama wanavyosutana na Mwanamke Mwenzao mitaani kwetu.

  CCM Jamani maadili yenu yanapolomoka kupitia viongozi wenu aina ya DEO ni picha chafu isiyopendeza kuiona kati ya kijana DEO mbunge wa Wananchi kupitiia tiketi ya CCM akilumbana na Wakina Mama.

  Kisaikolojia picha ile ya DEO na Wakina Mama wale, Wanawake mitaani wanamuona DEO kama kiwakilishi cha Wanaume Waongo wanaosutana na wanawake.

  Natoa challange kwa CCM,wachukue Picha zilizopigwa kati ya Deo na kinamama wazipeleke kufanya maojiano kupitia Picha zile [A Picture Speek athousands words] haswa wakina Mama waulizwe wanatafsiri nini kwenye picha hizo zilizombele yao.Majibu yatakayotoka hapo Ndio impact ya kuwa na viongozi type ya Deo ndani ya CCM na Serikalini.Wabunge wapenda vijembe,majungu na ujuaji usio na tija vilivyopelekea kuiponza CCM mpaka kufika hapo ilipo sasa ya KUCHOKWA NA BAADHI YA WANANCH.

  Wabunge wa CCM wanaitaji mafunzo ya mahusiano [Public Relation] na miongozo mingine ya jamii kimahusiano juu ya muuonekano [Bahaviour].Na mafunzo hayo yasifanye na watu ndani ya CCM bali yafanywe na makampuni au taasisi zenye kujua mapokeo ya umma dhidi ya matendo ya kiongozi au mwakilisha wa wananchi mbele ya umma yasio ndani ya CCM.Kwa kuwa yanayoendelea ndani ya Watendaji wa CCM ni matokeo ya Mafunzo ya ndani kwa ndani.lakini wakifundishwa kutoka nje watajiona mapungufu yao na hivyo watajifunza kwa faida yao na faida ya CCM kama chama.
   
 19. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kumsuta ilikuwa haitoshi wangempa kipigo cha haja
   
 20. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Acheni ubaguzi nyinyi...yaani mwanamke akiingia bungeni kwa tiketi ya viti maalum tu basi 'anakuwa mwanamke wa bar' asiye na uwezo wowote!? Sikatai kuna wabunge wengine wa vitu maalum hawakustahili kuwepo bungeni (both kwa wanaMagamba na wanaMagwanda) lakni hawajatokea baa, na si kweli kuwa hawana uwezo kiasi cha kufananishwa na wahudumu wa bar au machangudoa wa Jolly's!
   
Loading...