Kitendo cha kumlipia Mahari mwanamke kimepitwa na wakati.

Free ideas

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
3,453
1,930
Tangu zamani nimekuwa nikijiuliza kwa nn mwanake analipiwa mahari??,nikagundua kuwa ni utamaduni ambao tumerithi toka kwa vizazi vilivopita.lakini nikajiuliza tena kwa nn utamaduni huu bado tunao nakati kwa mtazamo wangu naona kama umepitwa na wakati!!
Baadhi ya sababu wanazodai watu kwa kitendo hiki ni hiz.
1.Ni kuwapa heshima wazazi wa binti
2.kama shukrani kwa wazazi wa binti
3.kufidia ghalama walizotumia kmlea na kumsomesha pia.

Lakini kwa nn na mambo haya wasifanyiwe wazazi wa kijana????.kwan wao hawahitaji shukran?.Hiz ghalama za Mahali kwa nn wasianzishe hata biashara wakainua maisha yao??,
Kulipa mahali hakuna tofauti na kumnunua binti kama ununuavyo baiskel dukani kisha unaenda kuipanda na kitumia utakavyo.
Kitendo hindi ndo chanzo cha manyanyaso na kukandamizwa na pia mifumo dume katika familia nyingi maana si kakipia???
Ni maoni tu jamani mnaweza kukosoa ama kusapot
 
hili ni suala la mila na dini zaidi, kwetu kidini mahali ni kiasi au kitu anachataka binti na anakabidhiwa yeye mwenyewe, ukija katika mila zetu za kiafrika ni suala la maamuzi ya wazazi, sioni shida hapo...
 
Wazee wetu walipata maagizo hayo kutokana na dini.
Ebu fungua bible/msaafu utakutana na hizo taratibu.
Kwahiyo ukisema imepitwa na wakati,unamaanisha Kwamba amri ya mungu imepitwa na wakati!!
 
Mie sifikilii hivo Naona ni utoa heshima kwa familia ya mke ni utamaduni mzuri uliokuwepo kwa karne nyingi! Japo viwango vya mahari siku hizi vimekua vikubwa ni vema vikapunguzwa ila kutoa mahari sioni tatiZo hapo!
 
Kwa sisi Wapare kuna kitu inaitwa " mcheku" (bikra), ukioa lazma ulipie. Wengine ni wizi mtupu,
 
Mie sifikilii hivo Naona ni utoa heshima kwa familia ya mke ni utamaduni mzuri uliokuwepo kwa karne nyingi! Japo viwango vya mahari siku hizi vimekua vikubwa ni vema vikapunguzwa ila kutoa mahari sioni tatiZo hapo!

Pia, Mahari yanaonyesha ni jinsi gani unampenda huyo binti.
 
Mie sifikilii hivo Naona ni utoa heshima kwa familia ya mke ni utamaduni mzuri uliokuwepo kwa karne nyingi! Japo viwango vya mahari siku hizi vimekua vikubwa ni vema vikapunguzwa ila kutoa mahari sioni tatiZo hapo!

Sawa lakini kwa nn heshima hii asipewe pia kijana kwa wazazi wa binti kutia chochote kwa wazazi wa kijana??,nahisi manyanyaso ya familia ama wanawake majumbani hili la mahari linachangia pia
 
Tangu zamani nimekuwa nikijiuliza kwa nn mwanake analipiwa mahari??,nikagundua kuwa ni utamaduni ambao tumerithi toka kwa vizazi vilivopita.lakini nikajiuliza tena kwa nn utamaduni huu bado tunao nakati kwa mtazamo wangu naona kama umepitwa na wakati!!
Baadhi ya sababu wanazodai watu kwa kitendo hiki ni hiz.
1.Ni kuwapa heshima wazazi wa binti
2.kama shukrani kwa wazazi wa binti
3.kufidia ghalama walizotumia kmlea na kumsomesha pia.

Lakini kwa nn na mambo haya wasifanyiwe wazazi wa kijana????.kwan wao hawahitaji shukran?.Hiz ghalama za Mahali kwa nn wasianzishe hata biashara wakainua maisha yao??,
Kulipa mahali hakuna tofauti na kumnunua binti kama ununuavyo baiskel dukani kisha unaenda kuipanda na kitumia utakavyo.
Kitendo hindi ndo chanzo cha manyanyaso na kukandamizwa na pia mifumo dume katika familia nyingi maana si kakipia???
Ni maoni tu jamani mnaweza kukosoa ama kusapot
kwa mila zetu mwanaume anaoa. mahari ni kama namna ya kupata the title ya muoaji thats mwanaume ndio anatoa. wazazi wa kiume hawawezi kudai mahari because that will mean mwanao kaolewa, ambayo haileti maana nzuri kwetu.

summary: mahari inampa mwanaume title ya 'muoaji'
 
Wazee wetu walipata maagizo hayo kutokana na dini.
Ebu fungua bible/msaafu utakutana na hizo taratibu.
Kwahiyo ukisema imepitwa na wakati,unamaanisha Kwamba amri ya mungu imepitwa na wakati!!
ok sawa lakini kutoa mahari sidhan kama ni amri ya mungu,huu ni utamaduni ambao tumerithi kama nilivosema katika uzi,lakini kuna haja gani ya kueneleza tamaduni hii ambayo mi naiona ni ya ukandamizaji upande mmoja??,
 
Ukandamizaji wakikwambia ulete 5m na zaidi. Kama ni reasonable kwanini....kwa upande wangu ni zawadi ya binti.
 
kwa mila zetu mwanaume anaoa. mahari ni kama namna ya kupata the title ya muoaji thats mwanaume ndio anatoa. wazazi wa kiume hawawezi kudai mahari because that will mean mwanao kaolewa, ambayo haileti maana nzuri kwetu.

summary: mahari inampa mwanaume title ya 'muoaji'

Sawa nimekuelewa
 
Tangu zamani nimekuwa nikijiuliza kwa nn mwanake analipiwa mahari??,nikagundua kuwa ni utamaduni ambao tumerithi toka kwa vizazi vilivopita.lakini nikajiuliza tena kwa nn utamaduni huu bado tunao nakati kwa mtazamo wangu naona kama umepitwa na wakati!!
Baadhi ya sababu wanazodai watu kwa kitendo hiki ni hiz.
1.Ni kuwapa heshima wazazi wa binti
2.kama shukrani kwa wazazi wa binti
3.kufidia ghalama walizotumia kmlea na kumsomesha pia.

Lakini kwa nn na mambo haya wasifanyiwe wazazi wa kijana????.kwan wao hawahitaji shukran?.Hiz ghalama za Mahali kwa nn wasianzishe hata biashara wakainua maisha yao??,
Kulipa mahali hakuna tofauti na kumnunua binti kama ununuavyo baiskel dukani kisha unaenda kuipanda na kitumia utakavyo.
Kitendo hindi ndo chanzo cha manyanyaso na kukandamizwa na pia mifumo dume katika familia nyingi maana si kakipia???
Ni maoni tu jamani mnaweza kukosoa ama kusapot

Hizo ni sababu za kujaribu kulipa suala la mahari usasa. Lakini kwa asili za huku kwetu mahari ilitolewa kwa sababu mwanamke alikuwa anachukuliwa kama property. Hivyo wewe unayemuoa lazima uilipie hiyo property na wale wanaopoteza hiyo property (yaani wazazi) ni lazima wawe compensated. Watu watakupa sababu nyingi na nyingine za kidini ili kuhalalisha hilo suala lakini ukweli unabaki pale pale kwamba suala hili liliangaliwa kwa mtazamo wa kwamba wanawake wanakuwa owned.

Kwangu mimi suala halina mjadala hakuna kuuza mtu wala kununua mtu. Kama zawadi watapata tu, zawadi watu huwa hawapangiani. Kama heshima ya kutunza watoto vizuri wote wanastahili tena wazazi wa kijana kwa nyakati hizi za uliberali na changamoto tosha.
 
  • Thanks
Reactions: KUN
Ukandamizaji wakikwambia ulete 5m na zaidi. Kama ni reasonable kwanini....kwa upande wangu ni zawadi ya binti.

What is reasonable MadameX? Halafu hiyo zawadi ya binti kwanini watu wakae kitako wakupangie, muoaji hawezi kukaa na mchumba wake wakaombana zawadi?
 
mkuu mimi nakusupport kwa 100%,binasfi nimekuwa nikilitafakari sana hili jambo la mahalinatoa ahadi mbele ya mwenyezi Mungu na kwa wana JF wote nitafanya kitu tofauti kabisaa kwa binti zangu,nina watoto 2 wa kike na Mungu akaipenda ikifika kipindi cha kuolewa hawa binti zangu nitafanya hivi,...kama kawaida nitamtwanga fungu la kutosha huyo mwanaume atakayetaka kuoa binti yangu,kama atafanikiwa kuleta hicho kiasi cha pesa kwa mfano mil 5,nitahifadhi hizo pesa zote bila kutumia hata sent moja huku na mimi nikiandaa kiasi cha pesa kama hicho,jumla zitakuwa mil 10,...nitazikabidhi hizo pesa zote kwa hao wanandoa siku wanapoanza maisha yao ya ndoa ili ziwasaidie kuanzia maisha.hii ni ahadi amabyo lazima nitahitimiza
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom