Kitendo cha kumchanganya Pengo na madawa ni cha hatari

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,663
Habarini wakuu,

Wiki takribani moja na nusu iliyopita jiji la Dar es salaam na viunga vyake lilitetema, kwa kitendo cha kishujaa cha mkuu wa mkoa Paul Makonda kwenda mbele ya vyombo vya habari na kutaja majina ya wale ambao yeye anadai wana uhusika kwenye mtandao wa madawa ya kulevya.

Lakini katika awamu ya pili ya utajaji wa majina, mmoja wa waliotajwa naye alienda kwenye vyombo vya habari kutoa yake ya moyoni. Hakukuwa na tatizo kuhusu hatua yake, kwani nchi hii inaongozwa kwa misingi ya sheria inayojali angalau kwenye maandishi, uhuru wa kujieleza.

Katika kuongea mbele ya vyombo vya habari, bwana yule alisikika akisema "Mbona asimwite Kadinali Pengo amsaidie?" Ni swali hilo lililonifanya kuleta uzi kwenye jukwaa hili la siasa. Mimi kama muumini wa kanisa Katoliki nimeumizwa sana na kauli hiyo. Kauli ya kumchanganya Pengo ambaye ni kiongozi wa wakatoliki wote Tanzania, na Katoliki ambayo ni taasisi ya kidini yenye nguvu duniani, ni jambo la hatari sana sana sana..

Sitaki kuongea mengi ila nataka kutoa angalizo kwa watu,.. unapokuwa unaongea na public na ukamzungumza mtu fulani kwanza tafakari kwa mapana yule unayemuongelea ni nani? wanaomzunguka ni watu wa aina gani? wanaohusiana naye ni watu wa aina gani? Taasisi aliyopo ni ya aina gani?...... mtu unakurupuka tu kama bata kwenye maji "binadamu wote ni sawa ila watu wote sio sawa" hivo lazima mtu uwe makini pale unapozungumza kuhusu watu.

Nawasilisha

Naantombe Mushi

Kama sehemu ya uzi huu, naamba watu mkajisomee kitabu kilichaandikwa na Michael Thomsett ---> Heresy in Roman Catholic Church mpate kujua kanisa katolic ni taasisi ya aina gani? na huwa inafanya nini kulinda status yake kwenye jamii...
 
Mtoa mada acha uzezeta, wanadamu wanamkosoa ALLAH aliyetuumba itakuwa mwanadamu acha kuabudu mtu
Nani kaandika ana muabudu mtu? Nnachoongelea hapa ni watu kuepuka kutoa allegations zinasababisha damage kwa jamii.. Nyie jifanyeni tu na ID zenu za uwongo,, mtaingia kwenye hatari,, endeleeni kumuhusisha Pengo na ujinga wenu huo
 
Kwani pengo ni Mungu
Pengo sio Mungu, na wala hakuna sehemu nimesema yeye ni Mungu.. Nimetoa tu angalizo kwamba aheshimiwe na iwe mwisho mtu kuja publicly na shutuma za kuleta damage kwa kanisa...

Sasa endelea kujifanya Pengo sio Mungu, halafu uende ukaitishe press kama alivofanya yule bwana juzi.. umuhusishe tena na madawa. ukweli utaupata
 
Kijana labda ni mgeni hapa jf , kuna uzi humu unamhusu pengo mwenyewe akilalamika kusingiziwa kuuza unga , ilikuwa january 2012 kama sijakosea .

Na kwa vile makonda kaamua kuchukua taarifa za vijiweni , sasa kilichomfanya aogope kumtaja pengo ambaye aliwahi kujitetea kuhusiana na hilo ni nini ?

Pengo kama mwanadamu na shabiki wa ccm anayo mapungufu lukuki , mwache ajadiliwe ili Mungu amchukulie hatua .
 
Mtu yeyote anapobanwa sehemu kwa tuhuma halafu akaanza kuanza kuhangaika kutaja watu wengine ni wakumwangalia kwa umakini mkubwa.
Ni utetezi dhaifi sana kwanza,,, huwezi kujitetea kwa kusema kwanini fulani hamjamtaja...
 
Back
Top Bottom