Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,835
114,355
Wanabodi

Ilani ya uchaguzi ya chama cha siasa ndio barua ya kuomba kazi ya kutawala kwa chama fulani, ukiisha chaguliwa, utekelezaji wa ilani ndio mkataba kati watawala na watawaliwa, mtu au kiongozi yoyote huwezi kujiibukia bila kikao chochote na kesema jambo fulani ulililoahidiwa kwenye ilani yako ya uchaguzi, lililokifanya chama cha kushinda, huwezi kusema kuwa jambo fulani sio kipaumbele chako. Hii ni hadaa na breach of contract, hivyo CCM na serikali yake, ilipaswa ku vacate Ikulu ya Magogoni come 2020 for breach of contract and non compliance of its promises kwenye ilani!, kitendo hicho ni hoodwinking!.

Leo nimepata tena fursa ya kuendelea na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa" swali likiwa jee kitendo cha kukiuka kipengele kwenye ilani yako ya uchaguzi iliyo kuweka madarakani bila kikao chochote rasmi cha utenguzi wa kipengele cha ilani, sio udikiteta?. Kama jibu ni ndio, what does that mean kwa huko tuendako?.

Jee hoja ya udikiteta nchini Tanzania bado ni dhana tuu au mwanzo ndio ilikuwa dhana tuu, lakini sasa as days go by, huko tuendako, kama tumeanza kuushuhudia udikiteta wa ukweli ukweli kidogo kidogo, japo ni udikiteta mwema, udikiteta mzuri wa kuleta maendeleo, a benevolent dictatorship, what should we expect in future?, kwasababu hata wale ruthless dictators walianza hivi hivi kwa kuwa populist and benovelent ones, then ruthless!.

Udikiteta Tanzania ulianza kwa the consolidation of powers kwa wakuu wa mihimili yote kupiga magoti kuomba ruhusa ya kutekeleza baadhi ya majukumu yao yanayohusu kusafiri nje ya nchi, kupiga magoti kuomba ruhusa kwa mkuu wa mhimili mmoja. That was good kuwazuia safari zisizo na manufaa kwa taifa, ni udikiteta mzuri!.

Ukaja udikiteta wa kukanyagwa kwa katiba katika kipengele cha freedom of speech, expression and movement on political ralies. Watu tukapiga kelele humu hadi tukamuuliza mwenyewe anatumia mamlaka gani ndani ya katiba yetu?, jibu sote tunalijua. Ila pia huu ni udikiteta mzuri maana hapa nchi ya Bongo, siasa zilizidi!, kila kitu siasa!.

Wakati yote haya yakifanyika, wana CCM kazi yao ilikuwa ni kushangilia tuu. Sasa ni zamu ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM inakanyagwa, jee wana CCM wataendelea kushangilia au kutatokea wana CCM bold wa ukweli na kuambiana humo ndani ya vikao vyao kuwa this is not right?.

Jee Udikiteta ni Nini?,
Udikiteta ni maamuzi yoyote yanayofanywa mtu mmoja ambayo yanakwenda kinyume cha katiba, sheria, taratibu na kanuni, ni maamuzi ya kidikiteta, ila maamuzi hayo sio lazima yawe ni maamuzi mabaya. Maamuzi mengine ya kidikiteta ni maamuzi mazuri kabisa na udikiteta huo unafanywa kwa nia njema kabisa, ndio unaitwa benevolent dictatorship.

Hivyo udikiteta sio matendo au vitisho, bali hata kauli tuu za mtu mmoja kuamua jambo lolote kwa utashi wake mwenyewe bila kikao chochote na kuutangaza uamuzi huo hadharani, kuwa ndio msimamo unaohitaji utekelezaji tuu bila kuhoji. Uamuzi huo unakuwa ulifikiwa kwa kauli ya mtu mmoja tuu bila ya ushirikishwaji kupitia kikao chochote au mashauriano. Uamuzi huu ni uamuzi wa kidikiteta, ila sio lazima uwe ni udikiteta m-baya.

Sasa naomba niwapeleke kwenye msingi wa hoja hii ni kipengele hiki cha ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 iliyomwingiza rais Magufuli madarakani.

Capture1.PNG

Kwa vile kipengele hiki kiko kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, hii maana yake kuna Kikao cha CCM kilikaa kikajadili hoja hii na kuiingiza kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Msingi wa ushindani kisiasa ni kushindanisha ilani, chama chochote kinachoshinda uchaguzi, kitahesabika, kimeshinda kwasababu ilani yake imekubalika zaidi kuliko ilani nyingine zote.

Ilani ya uchaguzi ya chama chochote, pamoja na kuwa na vipengele vingi, lakini inahesabika as a single document, hivyo chama kikishinda baada ya kuinadi ilani yake, ushindi huo unahesabika ni kufuatia Kukubalika kwa ilani yao, na serikali itakayo undwa inatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama kilichoshinda uchaguzi Mkuu huo.

Hivyo ushindi wa CCM kwa Uchanguzi Mkuu wa mwaka 2015, ulichangiwa na ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 kwa Watanzania katika Umoja wetu kuamua kuichagua CCM kutokana na ahadi lukuki katika ilani yake ikiwemo ahadi kuwa watoto wa kike watakaopata ujauzito wakiwa shuleni, wataendelea na masomo.

Kitendo cha mtu mmoja yoyote kuibuka na amri yoyote inayokwenda kinyume cha ilani ya Uchaguzi ya CCM bila kikao chochote kilichokaa na kilichotengua ilani hiyo, huu ni udikiteta wa wazi kabisa wa mchana kweupe ila ni udikiteta mwema.

NB. Neno dikteta lisitumiwe vibaya, sio kila Udikiteta ni Udikiteta m-baya, Udikiteta mwingine ni Udikiteta mzuri unaitwa benevolent dictator anayefanya dictatorship kwenye mambo ya kuketa maendeleo, ni a benevolence dictatorship hivyo huo Udikiteta unafanywa kwa nia njema na dhamira safi ya kulisaidia taifa letu na kuliletea maendeleo.

Kama ulivyo huu uamuzi wa kutowahurumia wala kuwavumilia watoto wowote wa kike wanaopata ujauzito, bila kujalisha wamepataje iwe ni kwa hiari, kubakwa au kudanganywa etc, uamuzi huu ni wa kidikiteta ila ni Udikiteta mzuri kuzuia vitendo vya ngono kwa wanafunzi, ili iwe fundisho kwa wengine.

Tungefuata Ilani ya uchaguzi ya CCM inavyosema na kuruhusu watoto wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo, this would be opening the pandora box, ni kama kuwahamasisha watoto wetu kufanya ngono tena bila kinga maana ukipata ujauzito utaendelea na masomo so why uogope ngono?.

Haki ya mtoto kupata elimu bila kubaguliwa iko kwenye ibara ya 26 ya Tamko la Haki za Binadamu la Mwaka 1948 linampa kila mtu haki ya kupata elimu Katika Tanzania haki hii ya elimu imetambuliwa na Katiba ibara ya 11( 2), Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 1995, Sheria ya Elimu ya mwaka 1978, Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 chini ya kifungu namba 9 na nyingine nyingi vimechangia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa katika kutekeleza haki za mtoto kupata elimu, hivyo tamko hili la rais Magufuli, ni japo ni tamko la ubaguzi, kuwabagua watoto wanaobakwa na kupata mimba za utotoni. Mtoto yoyote wa chini ya umri wa miaka 18 akipata ujauzito ni amebakwa, hivyo kuzuiliwa kuendelea na elimu ni kubaguliwa, ila tamko hili limetolewa na rais Magufuli not as rais wa nchi, but as a concerned Father for the well being ya binti yake. Hakuna mzazi anayetaka binti yake apatie ujauzito shuleni!. Hivyo ubaguzi huu unafanywa kwa nia njema ili kutoa fundisho kwa watoto wengine, ni ubaguzi mzuri, hivyo udikiteta huu ni udikiteta mzuri.

Uamuzi kama huu ni Udikiteta mzuri kama ule wa kuwazuia Watanzania wasio na kazi wasikalie kuzurura majiani kwa kisingizio cha kuandamana na kushinda vijiweni vya siasa kwa kisingizio cha kuhudhuria mikutano ya hadhara.

Madikiteta wote duniani huanza kwa kuwa populists kisha ndio hugeuka for the better or for the worse!. Jee kwa mwendo huu tunaokwenda nao, are we heading to the right direction for the better or are heading the wrong direction for the worse?. Naunga mkono mkono juhudi zote zinazofanyika kuinyoosha nchi hii ambayo ilikuwa imepinda na katika kunyoosha huku lazima tutegemee maumivu ya hapa na pale ambayo ni inevitable, hivyo wakati tukishangilia haya, pia tuwe tayari kulia na kusaga meno just in case akienda kwenye extremes za the other direction!.

Katika mfumo wa siasa za vyama vingi, japo katika kupiga kura, tunashindanisha wagombea, lakini katika mfumo wa utawala, nchi itaendeshwa kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya chama kilichoshinda urais, hivyo hata wabunge wote wa upinzani na madiwani, wote wataongoza kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM,

Mgombea anayeshinda anashinda kwasababu ilani ya chama chako imekubalika na baada ya ushindi wa jumla, mshindi akija na hoja kuwa jambo fulani katika ilani iliyompa ushindi na kusema sio ajenda yake, mfano katiba mpya, hi some sort ya udikiteta na utapeli fulani wa kisiasa.

CCM imekuwa ikitumua hadaa kushinda chaguzi mbalimbali kwa kuweka vipengele vutia katika ilani zao, kumbe ni hadaa tuu, baada ya ushindi, ilani hizo huwekwa pembeni!.

Uchaguzi wa mwaka 1995 hoja ya OIC ilikuwa moto, ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 1995 ikasema Tanzania itajiunga OIC, Agustino Lyatonga Mrema na NCCR Mageuzi, akanadi kuleta mahakama ya Kadhi. Baada ya ushindi, CCM ikaitelekeza hoja ya OIC!.

Uchaguzi wa 2000, CCM ikaiparamia hoja ya mahakama ya Kadhi, na baada ya uchaguzi, wakaitosa.

Uchaguzi wa 2010, Chadema ndio walikuwa na hoja ya katiba mpya, lakini baada ya CCM kushinda, JK akaanza mchakato wa Katiba mpya na CCM wakaiweka kwenye ilani yake ya 2015 iliwemo hoja ya wanaopata ujauzito kuendelea na masomo, lakini baada ya ushindi, rais Magufuli amegeuza kibao kuwa Katiba mpya sio kipaumbele chake, na hakuna kusomesha wanaopata ujauzito!. Hii hi hadaa, ni utapeli na kama ni uamuzi wa mtu mmoja, bila kikao chochote, huu ni udikiteta!.

What Are The Consequences za Udikiteta?.
Mimi sitatizwi na udikiteta wowote unaofanywa na kiongozi yoyote kwa sababu yoyote, ninachochelea mimi ni matokeo ya huo udikiteta na mwisho wa dikiteta!. Haijawahi kutokea popote hapa duniani, kiongozi dikiteta akawa na mwisho mwema!. Angalia mwisho wa madikteta wote duniani, hawana mwisho mwema!. Kwanini tusiwasaidie viongozi wetu kwa kuwaelimisha kitu kinachoitwa karma ambacho kitawahukumu kwa matendo yao?. Kwanini viongozi wetu wasitende mema ili wajaaliwe mwisho mwema na waishi maisha yao to the fullest?.

Nimalizie kwa lili lile swali la msingi Jee Kitendo Cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?. If yes what does that mean?.

Paskali
Rejea kuhusu udikiteta
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...
Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia ...
Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya ...
Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli | Page ...
Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
UDIKTETA: Hongera Sana TWAWEZA, TZ hakuna Udikteta! Ila ...


Rejea za Vifungu
ICC - Legal Tools record: Convention on the Rights of the Child
ICC - Legal Tools record: Universal Declaration of Human Rights
United Nations Official Document
Research and reports
Full list
ICC - Legal Tools record: Policy Paper on Sexual and Gender-Based Crimes
http://www.oecd.org/els/family/43570328.pdf
ICC - Legal Tools record: Nairobi Declaration on Women and Girls' Right to a Remedy [...]
Child protection from violence, exploitation and abuse
Ijue Sheria ya Mtoto na Haki zake.indd - Tanganyika Law Society
Manufaa ya kudumisha haki za watoto - HakiElimu
tamko la jukwaa la haki za watoto - Tanzania Child Rights Forum
 
Madikiteta wote duniani huanza kwa kuwa populists kisha ndio hugeuka for the better or for the worse!. Jee kwa mwendo huu tunaokwenda nao, are we heading to the right direction for the better or are heading the wrong direction for the worse?. Naunga mkono mkono juhudi zote zinazofanyika kuinyoosha nchi hii ambayo ilikuwa imepinda na katika kunyoosha huku lazima tutegemee maumivu ya hapa na pale ambayo ni inevitable, hivyo wakati tukishangilia haya, pia tuwe tayari kulia na kusaga meno just in case akienda kwenye extremes za the other direction!.
Ahsante sana mkuu
 
Jibu ni ,Kitendo hicho ni cha kidikteta na aliyekifanya huitwa Dikteta.
Watu walimsema na kumlaani Tundu Lissu alivyosema rais ni dikteta uuchwara,leo wanaanza kukubali.
Na punde watakubali kuwa issue ya "makinikia" imefanywa hovyo na Tanzania hatutapata chochote.
 
Aliekuambia kua tunaongozwa na ilani ya CCM ni nani??
Wewe mwenyewe wajua kua Mafisadi wa CCM ndio waliotufikisha hapa tulipo leo na ilani zao hizo zikiwepo, ingekua ni ilani inayoongoza basi tegemea tungekua kulekule tulikokuwepo siku zote,

Zidumu Fikra Zinazodhaniwa kua Sahihi za Rais,............!!!!!!!!!!!!!
 
Sheria za nchi zinakiukwa seuze Ilani za vyama? Ilani sio msaafu wala Biblia bro!
Anayeongoza nchi bila kufuata ilani ya chama kilichomwingiza madarakani na sheria na katiba ya nchi anaitwa Dikteta.Ni swala la utambuzi tu,mleta mada hajasema ilani haiwezi kuikiukwa ila anauliza hicho kitendo si ni cha kidikteta?
 
Bunge ni mhimili unaojitegemea,anatoa yeye maagizo kwa spika huku kasimika Naibu spika wake. Katiba inavunjwa tu,utamskia Mimi mpenzi wa Mungu,mpenda haki,mzalendo na msema kweli!!!

Najaribu kuwaza kama kuna baraza lake la ushauri,wanathubutu kumshauri?! Maana alishasema yeye ni dereva asiyesikiliza wengine!!!
 


Hapa ni mwendo wa mateka mikono juu, mkuu akisema ndo Ilani yenyewe.

Subiri usikie wazee wa utetezi watakuja kutueleza hapa.
 
Kwa hili la kutowaruhusu wanafunzi waliopata ujauzito wasiendelee na masomo mimi naungana na mh. Raisi, hatuwezi kuruhusu binti kupata mimba akazae halafu arudi shuleni hii sio sawa
So akirudi darasani kusoma ni nini kinaharibika? Wewe unapata maumivu gani kwenye mwili wako kuhusu mtoto aliyekwenda kuendeleza elimu yake? Una roho mbaya tu. Nahisi hata sura yako iko hivyo hivyo
 
Kwanza unatakiwa ielewe kuwa hakuna chama chochote cha siasa hata duniani kilichotimiza Ilani yake ya Uchaguzi 100% katika utawala wake.

Kutotimiza Ilani ya uchaguzi haina tofauti na kukiuka Ilani hiyo.

Kwa hiyo unataka kutuambia utawala wa Marais waliopita walitimiza Ilani zao za uchaguzi na kama hawakutimiza walikuwa ni madikteta!

Juzi serikali ya conservative nchini Uingereza ilitupilia mbali ahadi zake nne za Ilani ya uchaguzi baada ya kuingia madarakani, kwa mantiki yako, utawala wa Waziri Mkuu, May niwa kidikteta!

Kwa kumalizia, hakuna Ilani ya uchaguzi iliyokiukwa kwa sababu hata maelezo ulio highlight yako general. Mwanafunzi aliyepata mimba bado anaruhusiwa kuendelea na masomo katika shule zingine za binafsi.

Kinachoshangaza, hii hoja ya wenye mimba kuendelea na masomo ilishakataliwa bungeni na wabunge wengi hata kabla ya Rais hajatoa tamko lake.
 

JembeNaNyundo,
Hii, 'Mmh' inaonesha dawa na sindano vimeingia!! Ukiona mtu mzima anagugumia ujue dawa imekolea.
Anachosema Paskal ni ukweli na uwazi. Nakubaliana naye kabisa kuwa huu ni UDIKTETA kwa 100% ila napingana naye kusema ni UDIKTETA MZURI. Hakuna udikteta mzuri au mbaya, udikteta ni udikteta tu!!! Pengine uzuri utakuwa upande wa dikteta mwenyewe kwa vile yeye anafaidi madaraka na haathriki na maamuzi hayo ya kidikteta.

Kulikuwa na Madikteta wa karne kina Hitler na kina Mussolini, kina Amini, Bokassa na wengineo, walitamba na walifaidi maisha wakti wa enzi zao, lakini leo hii wako wapi? Tell me my friend, where are they? They have gone forever and already judged by God. Biblia inasema baada ya KIFO NI HUKUMU, there is no repetance for sinners after death!!!!
 
Back
Top Bottom