Kitendo cha kiti cha Spika kuwapendelea wabunge wa CCM sasa kimepitiliza!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,483
30,155
Kitendo kilichofanywa juzi na mbunge wa Kasulu, kwa tiketi ya CCM, Augustine Vuma, cha kuichana Bungeni, hotuba ya wapinzani, na kitendo hicho kukingiwa kifua na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, ni kitendo cha kihuni na kinapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na wapenda demokrasia na wapenda amani wa nchi hii popote walipo.

Kitendo hicho kitazidi kuwajaza visasi wabunge wa upinzani, kwa kuona kumbe kiti cha Spika kina "double standard" katika kuchukua hatua za nidhamu, kati ya wabunge wa upinzani na wabunge wa CCM!

Hata hivyo kitendo hicho cha kuichana hotuba hiyo kimeonekana ni kitendo cha kawaida kabisa kwa Naibu Spika, Dk. Tulia Jackson, ambaye hakuchukua hatua yoyote dhidi ya mbunge huyo "mhuni" na badala yake akawatoa nje wabunge watatu wa upinzani, ambao ni John Heche (Tarime vijijini) Esther Matiko (Tarime) na Dk Emmaculate Sware (Viti maalum) kutokana na kulalamikia kitendo cha Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, cha "kupotezea" kitendo hicho cha utovu wa hali ya juu wa nidhamu, kilichofanywa na mbunge mwenzie wa CCM

Nimekuwa nikijiuliza hivi ingetokea kwa mbunge wa upinzani, ndiye kafanya kitendo kama hicho, cha kuichana hotuba ya Waziri wa Fedha, Philip Mpango,si ndiyo huyo mbunge angefungiwa hadi Bunge hili litakapomaliza kipindi chake mwaka 2020, na mbunge huyo "kupotezwa" kabisa??

Nimekuwa pia nikijiuliza, hivi kiti cha Spika, si ndicho ambacho kimekuwa kikiwatoa wabunge wa upinzani kiholela, kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu, kama walivyowafanyia wabunge, Godbless Lema wa Arusha na mbunge mwenzake, Halima Mdee, kwa sababu tu ya kuunga mkono kauli iliyotolewa na CAG kuwa Bunge ni dhaifu??

Hivi watanzania tunaweza kuliweka kundi gani Bunge letu, kama haliwetendei haki wabunge wetu wa upinzani, ambao wamechaguliwa na wananchi wao majimboni, ili kuwasemea matatizo yao na badala yake ni kiwatimua Bungeni kila kukicha na badala yake wakiona wabunge wenzao wa CCM, wakipata kinga ya kiti cha Spika, hata wakifanya makosa ya "kufa mtu" kama alivyofanya mbunge wa Kasulu vijijini, ya kuichana hadharani, hotuba ya kambi rasmi ya upinzani??

Hivi kiti cha Spika, kinafahamu kuwa kambi rasmi ya upinzani, ipo kwa mujibu wa sheria??

Mungu ibariki Tanzania na ukijaalie kiti cha Spika ili kitende haki sawa kwa wabunge wote wa Bunge hilo, wale wa upinzani na wa CCM. Amen
 
Hivi kwa kitendo kama hiki kilichofanywa na Naibu Spika cha kufanya upendeleo wa waziwazi kabisa wa wabunge wenzao wa CCM kwa kutowachukulia hatua, hata pale wanapofanya vitendo vya kuzivunja kanuni za Bunge, kama alivyofanyiwa Mbunge wa Kasulu Mashariki, cha kuichana hadharani hotuba ya kambi rasmi ya upinzani, si ndiyo watanzania tumethibitisha pasipo shaka yoyote, kuwa hiki chombo chetu cha Bunge kweli ni dhaifu sana??
 
1132991
 
Back
Top Bottom