Kitendo cha Jaji Mkuu kutambua nafasi ya Makamu wa Rais Bara kama Makamu wa Pili; Je, ni bahati mbaya ama?

Hata huyo waziri mkuu mamlaka yake yanaishia Tanganyika kule Zanzibar hana ubavu wa kumwajibisha yeyote.
Zamani Rais wa Zanzibar ilikuwa akitaka kugawa mipaka upya ya wilaya na mikoa basi lazima ashauriane na Rais wa muungano lakini baadaye wakafanya marekebisho ya katiba wameondoa kipengele hicho sasa anaamua bila ya kushauriana na Rais wa muungano, yaani kwa ujumla muungano wetu hauweleweki kabisa.
Muungano wa udongo huu
 
Kiufupi kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Makamu wa Rais wa Tanzania+Jaji Mkuu wa Tanzania+Waziri Mkuu+Spika wote ni Wakubwa kuliko Rais wa Zanzibar maana Katiba imewatambua wao kushika Mamlaka ya Nchi kama Rais hayupo.

Lakini ukweli ni kuwa hao wote kule Zanzibar hawatambuliki-sasa huo ni Muundo gani wa Muungano??
 
Hapa ndio uone blander aliyoifanya Nyerere ameleta mvurugano tu,Bahati nzuri ni kuwa Watanzania wengi ni mazezeta yatufatilii wala kujali ingekuwa Nchi za Watu wanaojielewa pasingetosha.
binafsi sioni madhara kwangu, kwasababu moyoni mwangu zenji huwa nahesabu sawa na wilaya fulani tu, na rais wao huwa sihesabu kama rais wangu au kama mtu mwenye wadhifa fulani kwangu.
 
....Lakini ukumbuke, hao wooote uliowataja ni wakubwa kwa Rais wa Zanzibar, siku ya sherehe ya mapinduzi kule Amaan Stadium, Rais wa Zanzibar ndiye boss kubwa, top manyota, aka Mgeni Rasmi, Upo hapo jombaaaa........
Kiufupi kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Makamu wa Rais wa Tanzania+Jaji Mkuu wa Tanzania+Waziri Mkuu+Spika wote ni Wakubwa kuliko Rais wa Zanzibar maana Katiba imewatambua wao kushika Mamlaka ya Nchi kama Rais hayupo.
Lakini ukweli ni kuwa hao wote kule Zanzibar hawatambuliki-sasa huo ni Muundo gani wa Muungano??
 
CJ wetu siyo mtu makini na ile nafasi aliipata kwa itikadi ya ukanda. Japo ni mtu mwema kama binadamu na mwalimu mzuri wa sheria, lakini kuwa CJ ni mzigo mkubwa sana kwake.
Ni kweli kabisa viatu havimtoshi ,haijui mahakama vizuri
 
Video hii imenifikirisha sio kiasi, sana tu, na kujiuliza, “Kwanini Mhe.Prof. IBRAHIM HAMIS JUMA, Jaji Mkuu wa Tanzania hutaja nafasi ya Makamu wa Rais kama “Makamu wa Pili” kila anapopaswa kufanya hivyo?”

Profesa amekuwa akirudia zaidi ya mara moja kiasi cha kutosha kusema kwamba “hakosei, bali anamaanisha” anachokisema.

Je, kuna protokali penginepo anaifahamu zaidi ya wengi kisheria au ni nini?

Tazama video:
 
Back
Top Bottom