Kitendo cha Jaji Mkuu kutambua nafasi ya Makamu wa Rais Bara kama Makamu wa Pili; Je, ni bahati mbaya ama?

Katiba ya nchi haisemi kuwa kila mgombea urais lazima awe na mgombea mwenza ambaye atamrithi urais endapo atafariki, kilichotumika ni katiba ya CCM.
 
Haya yote anayoyafanya huko Zanzibar yanaigusa wapi bara upande wa pili wa Muungano? Ukiangalia kwa umakini, utaona hitaji la katiba mpya. Kw asteucture hii ya Muungano, raisi wa Zanzibar anatakiwa kuwa na hadhi sawa na Waziri mkuu ambaye pamoja na kwamba ni Waziri mkuu wa JMT kimazoea shughuli zake zimekuwa zikiishia bara. Huwa havuki maji, hii ni tofauti na raisi na makamu wake; hawa hata kuchaguliwa kwao kuna hitaji kuwe na uwiano wa kieneo, kwa mantiki hiyo hawa ndio viongozi wa muungano period.

Hapa inabidi wamkaribishe wakili msomi Tundu Antipas Lissu aje atufafanulie kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania kuhusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 2020 kuwa na Makamu wa Pili wa Rais ktk serikali ya Muungano wa Tanzania.

Je rais wa Zanzibar SMZ aliye mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar BLMZ walimshindikiza hayati mwendazake John Pombe Magufuli kutambua ukubwa wa Rais wa SMZ aliye mwenyekiti w BLMZ katika serikali ya Muungano wa Tanzania?

Na ndiyo maana Hayati rais John Magufuli wala Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano hawajatia neno kuhusu Jaji Mkuu wa Tanzania kutambua uwepo wa kiaina wa Makamu wa Pili wa Rais ktk serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka hapo katiba itapobadilishwa na kutambua uwepo wa Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais ktk serikali ya Muungano wa Tanzania ili kumuweka panapostahili kiitifaki / kiprotokali Rais wa SMZ ktk Setikali ya Muungano wa Tanzania.


Haiwezekani rais wa SMZ atambulike kama mjumbe aliye na wadhifa wa uwaziri ktk mkutano wa baraza la mawaziri wa Muungano ( kabineti). Wakati rais wa serikali ya SMZ kiitifaki kwa sasa ni mkubwa kuliko Makamu wa Rais wa JMT pia ni mkubwa kuliko Waziri Mkuu wa JMT.

Rais wa SMZ anaongoza nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano, ana bendera ya rais wa SMZ ana vikosi maalumu, KMKM na valantia katika nchi ya Zanzibar, ana uwezo wa kuvunja Baraza la Uwakilishi Zanzibar pia kuitisha uchaguzi Zanzibar wakati kwa mfano Makamu wa Rais JMT na waziri mkuu wa JMT hana madaraka hayo wala wadhifa unaokaribia U-Amiri Jeshi wa Majeshi ktk nchi.
 
Alienda kumjwakilisha Rais kama ambavyo JPM alivyowahi kumteua JK akamuwakilishe
Uwakilishaji wa JK ulikua ceremonial tu kwenye shughuli ya kitaifa huko alikoenda,ila Mwinyi Hussein ilikua na technical decision zaidi kwa Tanzania as all.
 
Hakuna la ajabu hapo. Ni muendelezo wa viongozi duni tulionao. Utamuona mtu ni profesa kumbe shiiida! Walichojaliwa ni kukosa aibu ya kuzungumza kwenye hadhira.
Ignorance of civics and civic education altogether.
 
Acha kupotosha, Rais wa Zanzibar anakuwa mjumbe wa baraza la mawaziri kwa nafasi yake kama rais wa Zanzibar yeye sio sawa na mawaziri wengine wa kisekta ambao ndio wapo chini ya Waziri Mkuu.

Na wakifuata rank anaanza Rais, Makamu wa rais, Rais wa Zanzibar na anayefuata ndio Waziri Mkuu.
1642921235883.png


Kama Rais wa Zanzibar kwenye Cabinet ni zaidi ya Waziri Mkuu, kwanini Rais na Makamu wasipokuwepo anapewa Waziri Mkuu kuongoza vikao?
 
Back
Top Bottom