Kitendo cha Jaji Mkuu kutambua nafasi ya Makamu wa Rais Bara kama Makamu wa Pili; Je, ni bahati mbaya ama?

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,048
3,227
Hii imekaaje wadau, Naona Jaji Mkuu amerudia maraa nyingi sana kuitambua Nafasi ya Makamo wa Rais wa Tanzania Bara kama Makamo wa pili ilhali tuna Nafasi Moja tu ya Makamo wa Raisi kwa Bara , Je matukio haya ni ya bahati mbaya ama alikua anakusudia na kuna Jambo ndani yake ?

Tizama hii

-------
Wasalaam,

Ni zaidi ya mara tano Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma Juma anatamka au kutaja kwa nafasi zao Makamu wa Rais kuwa Makamu wa pili wa Rais .

Je, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuna Makamu mmoja tu wa Rais ;

Kwa mjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara 47.-(1) inasema; "Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa
ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla",

Sheria ya 1994Na.34 ib.1,
Sheria ya 2000Na.3 ib.9.
"MKAMU MMOJA
WA RAIS",

Katika hii video Profesa Ibrahim Juma Juma kwa nyakati tofauti amekuwa akimtaja Makamu wa Rais wa Tz kama Makamu wa pili wa Rais.

Amefanya hivyo kwa Rais Samia akiwa Makamu wa Rais wa Hayati Magufuli na amefanya hivyo kwa Dkt Isdor Mpango na kumtaja kuwa Makamu wa pili wa Rais.

Je ni ulimi kuteleza ?
Ni Makusudi
Au anajua sana Katiba na sheria zake mbona amekuwa akitaja bila woga?

Hii hapa video

View attachment 1979976
 
Kwa hiyo hujui kama rais wa SMZ kuwa ndiye makamu wa kwanza?
Sio kweli. Marekebisho ya Katiba ya 1992 yaliyoruhusu Mfumo wa Vyama Vingi yalimuondoa Rais wa Zanzibar kama Makamu wa Rais. Sasa hivi anatambulika kama RAIS WA ZANZIBAR, MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ZANZIBAR NA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
 
Rais was Zanzibar ni mjumbe was Baraza la mawaziri kirank Yuko chini ya waziri mkuu
 
Acha kupotosha, Rais wa Zanzibar anakuwa mjumbe wa baraza la mawaziri kwa nafasi yake kama rais wa Zanzibar yeye sio sawa na mawaziri wengine wa kisekta ambao ndio wapo chini ya Waziri Mkuu.

Na wakifuata rank anaanza Rais, Makamu wa rais, Rais wa Zanzibar na anayefuata ndio Waziri Mkuu.
 
Upo sahihi sana.
 
Sio kweli. Marekebisho ya Katiba ya 1992 yaliyoruhusu Mfumo wa Vyama Vingi yalimuondoa Rais wa Zanzibar kama Makamu wa Rais. Sasa hivi anatambulika kama RAIS WA ZANZIBAR, MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ZANZIBAR NA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Ni sawa. Lakini mwenye nchi kutoka Zenjibay kaona iwe hivyo! Tatizo liko wapi? Mbona haukuitishwa uchaguzi mkuu baada ya rais kufia madarakani kama tulivyofundishwa kwenye somo la uraia mashule baada ya mfumo wa vyama vingi? Bwai bwai!
 
Hii imekaaje wadau, Naona Jaji Mkuu amerudia maraa nyingi sana kuitambua Nafasi ya Makamo wa Rais wa Tanzania Bara kama Makamo wa pili ilhali tuna Nafasi Moja tu ya Makamo wa Raisi kwa Bara , Je matukio haya ni ya bahati mbaya ama alikua anakusudia na kuna Jambo ndani yake ?
Hakuna la ajabu hapo. Ni muendelezo wa viongozi duni tulionao. Utamuona mtu ni profesa kumbe shiiida! Walichojaliwa ni kukosa aibu ya kuzungumza kwenye hadhira.
 
Hii imekaaje wadau, Naona Jaji Mkuu amerudia maraa nyingi sana kuitambua Nafasi ya Makamo wa Rais wa Tanzania Bara kama Makamo wa pili ilhali tuna Nafasi Moja tu ya Makamo wa Raisi kwa Bara , Je matukio haya ni ya bahati mbaya ama alikua anakusudia na kuna Jambo ndani yake ?

Tizama hii

Hatuna makamo wa rais bara mkuu, tuna makamo wa rais wa JMT naye kwa cheo hicho ni mmoja tu. Huyo aliemtambulisha vyinginevyo kafanya kimakosa. Rais wa SMK si makamo wa rais JMT kikatiba lakini ni mjumbe wa baraza la mawaziri wa JMT kwa nafasi yake.
 
Acha kupotosha, Rais wa Zanzibar anakuwa mjumbe wa baraza la mawaziri kwa nafasi yake kama rais wa Zanzibar yeye sio sawa na mawaziri wengine wa kisekta ambao ndio wapo chini ya Waziri Mkuu.
Na wakifuata rank anaanza Rais, Makamu wa rais, Rais wa Zanzibar na anayefuata ndio Waziri Mkuu.
Kasome katiba waziri anakuwaje juu ya waziri mkuu, kwani wametumia mjumbe was Baraza la mawaziri na sio rahisi wa Zanzibar, waziri mkuu majukumu yake kikatiba yameainishwa
 
Makamu wa Rais wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania ni mmoja tu, Soma kifungu cha 47 cha Katiba.
Nanukuu vifungu vidogo vya kwanza:
47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa

ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya

Muungano kwa jumla, na hususan-

(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku

hata siku za Mambo ya Muungano;

(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;

(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini

au yuko nje ya nchi.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa

Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa

pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake

wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na

watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais

akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa
 
Hii imekaaje wadau, Naona Jaji Mkuu amerudia maraa nyingi sana kuitambua Nafasi ya Makamo wa Rais wa Tanzania Bara kama Makamo wa pili ilhali tuna Nafasi Moja tu ya Makamo wa Raisi kwa Bara , Je matukio haya ni ya bahati mbaya ama alikua anakusudia na kuna Jambo ndani yake ?

Tizama hii

CJ wetu siyo mtu makini na ile nafasi aliipata kwa itikadi ya ukanda. Japo ni mtu mwema kama binadamu na mwalimu mzuri wa sheria, lakini kuwa CJ ni mzigo mkubwa sana kwake.
 
Back
Top Bottom