Kitendo cha ITV kufumbia macho tukio kubwa la kuvurugwa kwa uchaguzi wa Mayor Kinondoni

Kisheria, habari bila chanzo cha habari ni uzushi. Mmesema waandishi walioruhusiwa kuingia ndani ni Uhuru publishers tu. Sasa ITV wangesema wameipata wapi hiyo habari??
Pili;
Si mwajua kuwa lazima kuangalia habari unayo i publish?? Pongezi zangu kwa yule mmama mkuu wa ITV. Kwa mwoga huenda kicheko lakini kwa shujaa kilio. B/up saana Joyce
dead brain
 
Siku zote tambo za Chadema Media hazikutokana na ujasiri wa Viongozi na Wamiliki wake bali utayari na utashi wa Mh Jakaya Kikwete,
 
Mkiki tarifa zako hazijitosherezi,kavute bangi kwanza ndio ujikutoa Maelezo yenye uhakika.kama ulikuwepo pindi ITV wanachukuwa hayomatukio wewe ulishindwa nini kuchukuwa na kutulishia
 
NIMEFURAHI SANA CCM KUSHINDA UMEYA WA KINONDONI!! Anayebisha aandamane aone!! chadema siasa zenu za matukio zishapitwa na wakati na mwaka huu mtalia hadi mtasaga meno!! serikali ya magufuli ni serikali makini sana
Kama ukawa walishinda na CCM wakakubali inawapaswa na wao wakubali hapo ndio heshima itarudi
 
kwani ulikuwa hujui kama vyombo vya hbari haviko huru mkuu? mboa hii ipo sana tu...kumbukeni Mh Zitto Kabwe aliwaasa wanahabari na vyombo vya habari kuwa .......akishamalia na vyama vya siasa atwaingilia wanahabari na vyombo vya habari lakin zitto hakueleweka sasa wacheni tuisome namba kimya kimya hivyo hadi ihapo akli zetu zitakapo kaa sawa
 
Mkiki tarifa zako hazijitosherezi,kavute bangi kwanza ndio ujikutoa Maelezo yenye uhakika.kama ulikuwepo pindi ITV wanachukuwa hayomatukio wewe ulishindwa nini kuchukuwa na kutulishia
ulikuwa sahihi kuzaliwa tanzania.
 
Kitendo cha ITV kufumbia macho tukio kubwa la kuvurugwa kwa uchaguzi wa Mayor Kinondoni, kunakiweka kituo hicho katika orodha ya vituo visivyo huru katika tasnia ya habari. Ama kwa uoga au kwa amri kutoka juu ITV wameukosea sana umma wa watanzania kwa kushindwa kuonesha tukio hili.

Ni jambo la ajabu kwamba waandishi wa ITV walikuwepo Magomeni kwenye ukumbi wa Halmashauri wakati wajumbe wa CCM na UKAWA wakiwasili, walikuwepo pia ukumbini wakati CCM wakisigina sheria kwa kufanya uchaguzi batili, na walikuwepo pia makao makuu ya CHADEMA Mwenyekiti alipofanya Press Conference. Sasa kwanini hawajaripoti?

Kwamba habari ilitupwa kapuni na Mhariri? Kwamba wameona haina umuhimu? Kwamba muda waliotumia kutafuta habari hiyo umepotea bure? Bado sioni sababu yoyote yenye mashiko kwa ITV kushindwa kurusha habari hiyo.

Waliobserve kilichotokea ukumbini, wakaobserve CCM wakiendesha uchaguzi bila akidi kutimia, na wakaenda Kinondoni kuhudhuria PC ya Chadema. Kwahiyo walikua na information tips kutoka angle zote tatu muhimu. Wangetumia tips hizo kutoa habari objective ya kilichotokea. Sasa kwanini hawajaripoti? Kama tuna vyombo vya habari vilivyojawa uoga kiasi hiki, basi tuna safari ndefu sana ili kuweza kupata vyombo huru vya habari.

Malisa GJ
Kwani Melisa ni nani kuwapangia ITv cha kureport?
Kwani ITV wanapangiwa na chadema habari za kurusha?
 
NIMEFURAHI SANA CCM KUSHINDA UMEYA WA KINONDONI!! Anayebisha aandamane aone!! chadema siasa zenu za matukio zishapitwa na wakati na mwaka huu mtalia hadi mtasaga meno!! serikali ya magufuli ni serikali makini sana
Unajua kwanini vikundi vya uasi huwa vinazaliwa kwenye nchi mbalimbali?
Na sababu hizo zikivizalisha hapa kwetu unadhani tutakuwa salama kweli?
 
Huenda hawajafumbia macho, huenda wamefungwa mdomo, ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kupambania mitandao ya kijamii kama Jamiiforums kuwa huru na kuongeza idadi ya wananchi wenye kupata huduma ya internet.

Tunakoelekea huenda taarifa muhimu zikawa zinapatikana kwa njia ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuishia kutumika kueneza propaganda za vikundi/vyama fulani.
 
Kitendo cha ITV kufumbia macho tukio kubwa la kuvurugwa kwa uchaguzi wa Mayor Kinondoni, kunakiweka kituo hicho katika orodha ya vituo visivyo huru katika tasnia ya habari. Ama kwa uoga au kwa amri kutoka juu ITV wameukosea sana umma wa watanzania kwa kushindwa kuonesha tukio hili.

Ni jambo la ajabu kwamba waandishi wa ITV walikuwepo Magomeni kwenye ukumbi wa Halmashauri wakati wajumbe wa CCM na UKAWA wakiwasili, walikuwepo pia ukumbini wakati CCM wakisigina sheria kwa kufanya uchaguzi batili, na walikuwepo pia makao makuu ya CHADEMA Mwenyekiti alipofanya Press Conference. Sasa kwanini hawajaripoti?

Kwamba habari ilitupwa kapuni na Mhariri? Kwamba wameona haina umuhimu? Kwamba muda waliotumia kutafuta habari hiyo umepotea bure? Bado sioni sababu yoyote yenye mashiko kwa ITV kushindwa kurusha habari hiyo.

Waliobserve kilichotokea ukumbini, wakaobserve CCM wakiendesha uchaguzi bila akidi kutimia, na wakaenda Kinondoni kuhudhuria PC ya Chadema. Kwahiyo walikua na information tips kutoka angle zote tatu muhimu. Wangetumia tips hizo kutoa habari objective ya kilichotokea. Sasa kwanini hawajaripoti? Kama tuna vyombo vya habari vilivyojawa uoga kiasi hiki, basi tuna safari ndefu sana ili kuweza kupata vyombo huru vya habari.

Malisa GJ

Umbeaa mtupu hapa kazi tuu .
 
Back
Top Bottom