Kitendo cha gari la Mkuu wa Mkoa Mara kugongeshwa na mtoto wa dereva ni dhahiri agizo la Waziri Mkuu lilipuuzwa

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
874
1,000
Labda wazuie lisilale nyumbani lakini kuzuia lisiende nyumbani ni ujinga.
yaani hata kama kuna dharula nyumba ni?!?! Au napitisha tu mboga. Sasa huyu alienda kuosha gari kuna kosa kuoshea nyumbani kwake?!?! Wajameni haya matukio yanatokea sana duniani yuko mmoja majuzi hapa aliiba ndege akaigongesha!!!. Tusitumie bahati mbaya hii kulaumiana na kuzushiana
 

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,652
2,000
story iko hivi!

Watetezi wa dereva wa Mkuu wa Mkoa wanadai kwamba dreva alichukua Gari hilo kwenda kuliosha nyumbani kwake;

Alipomaliza kuliosha mgeni akaingia, Akaliacha Gari hilo likiwa silencer, akaingia ndani kuteta na mgeni;

Mtoto nae akaliiba kwenda kuoshea mtaani ndipo akalipiga chini!

Baada ya dereva (baba) kupata taarifa ya ajali (alizimia)

(Ukichambua coincidence hii pamoja na kwamba haina logic)

Bali imekiuka agizo la waziri Mkuu;
Ambapo alipiga marufuku madreva wote wa magari ya serikali kwenda na magari nyumbani mwao!
...............
Mambo kama haya;
  • Ndiyo yanayofanya magari ya serikali kutumia mafuta mengi pasipo sababu
  • Yanachangia magari ya serikali kusafilisha magendo
  • Yanachangia vipuri na spea za magari ya serikali kuibiwa na kubadilishiwa
  • Tunayapisha njiani kwa ving'ora kumbe house girl kaliiba ili awahi gengeni nk
YAMKINI HATA DOGO ALITUMWA AKANUNUE SODA YA MGENI CHAP
Kuna vitu havizuiliki we nae,hayo magari yanaendeshwa na watu na siyo mizimu kutoka sayari nyingine..nimetoka kuosha gari nikaona bucha ikanunua mboga na nyumbani kwangu ni uelekeo huo huo wa ofisini nisipitishe hiyo mboga kweli??haiwezekani! sema tu watu wawe na weredi kwenye mali za serikali ma mashirika na siyo kuwazuia kwa mambo madogo madogo kiasi hicho,huyo yeye yamkini alikua ni dereva asiyejali kampa gari mtoto wake na akaleta madhara.tena huyo anapaswa tu kusamehewa na kwa kitendo hicho hawezi kurudia wala wengine kufanya uzembe huo.
 

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,652
2,000
Kila mtu hutetewa na MUNGU kwa namna zake,kuna watu wanauwa lakini wanakutwa na hatia ya kuua bila kukusudia na wanafungwa miaka michache,kuna watu wanamakosa makubwa lakini wanakuja kuachiwa kwa msamaha na wanakua wamejutia makosa yao na hawarudii tena,sembuse dereva na ameshafiwa na huyo mtoto mwenyewe,MUNGU atampa kiasi cha mateso atakachokiweza
daaaah jiwe akipata hii habari, namhurumia sana dereva sijui pssf yake itabaki salama.., gharama ya gari si chini ya 250m jiwe atamuacha salama kweli? ikiwa mimi situation yangu kwa sasa kazini ni ndogo tu lakini ninavyopelekeshwa natamani hata wanifukuze kazi tu niachane nao kwa huyu ni mungu tu aweke mkono wake aisee
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,717
2,000
Adam Malima ni mwungwana sana

1565259402227.png
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,085
2,000
Kwanza huyu hakua dogo alikua mtu mzima miaka 26. Huyu ni mtu mzima kabisa he should have known better. Aidha dogo kachuma janga and it's very unfortunate it costed his life.

Utundu kwa watoto hasa wa kiume ni jambo la kawaida, mimi nimeanza kuiba gari nikiwa form2 si magari ya home wala ya serikali mzee akikaa vibaya napita nayo. Mzee wangu alinifundisha gari rasmi nikiwa na miaka15 ili nikiiba awe na uhakika kwamba am safe na huu ushauri alipewa na dereva wake mwenyewe kwamba mfundishe dogo gari ili hata akiiba uwe na uhakika kwamba atarudi salama. By form4 nilikua natoka nalo kwa uhuru kabisa na mafuta nawekewa so long as narudi home by 7pm. Those were the days.

Pamoja na hayo bado nilikula bonge ya mzinga na gari kuisha lote. Bahati yangu nilipona. Nilikua mdogo bado, utoto mwingi, speed sana na kuona gari ni rafiki yangu kumbe ni machuma tu yanakuua anytime hata kama umeliendesha miaka20.

All I'm trying to say is magari ni machuma tuyaendeshe kwa tahadhari sana.
 

Mr. Bigman

JF-Expert Member
May 7, 2011
2,563
2,000
Malezi ya mtoto hayako sawa.

Ofisi ya baba siyo ya kucheza nayo.

Haijalishi gari iko silent au loud ila ni ofisi ya baba hiyo hauchezi nayo.

Mfano akafukuzwa kazi na hali ikawa mbaya wanafamilia watakua wanakuangalia kwa jicho la "Yote umeyataka wewe"
Dah! Sentensi ya mwisho imejaa Mambo ya uswahilini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom