Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Yalianza malalamiko Mkoa wa Ruvuma kuwa CHADEMA wameteua mbunge wa viti maalum ambaye si mwenyeji wa Mkoa huo. Wanawake wa BAWACHA wakaandamana kupinga ukandamizaji huo wa CHADEMA. Hawakusikilizwa.
Zikaja taarifa za Frederick Sumaye kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani. Hili lilijadiliwa kimya kimya wengi wakiwa na mtazamo kuwa Sumaye kajidhalilisha kugombea nafasi hiyo. Hapa suala la Ukaskazini kusimikwa Pwani halikujadiliwa.
Sasa limekuja hili la Patrick Ole Sosopi kugombea Uenyekiti wa CHADEMA kanda ya Ziwa Nyasa. Hili limeanza kupigiwa kelele. Baadhi ya wana CHADEMA hasa kwenye magroup ya facebook wameanza kupaza sauti kuwa kinachofanywa na CHADEMA Makao Makuu 'kuimport' watu wa Kaskazini kugombea uongozi kwenye kanda zingine hakika halikubaliki. Ikumbukwe kuwa karibu safu yote ya Wakurugenzi wa CHADEMA Makao Makuu wanatoka Kanda ya Kaskazini. Sasa kanda zingine wameanza kuwapangia nani awaongoze kitu ambacho si sahihi.
Swali la kujiuliza, je ni kweli CHADEMA hawana watu sahihi wa kuongoza chama kwenye kanda tofauti na wale wanaotoka Kaskazini? Au kuna nini nyuma ya pazia?