Kitendo cha CHADEMA 'kuimport' viongozi wa Kanda kutoka Kaskazini, je nini nyuma ya pazia?

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Yalianza malalamiko Mkoa wa Ruvuma kuwa CHADEMA wameteua mbunge wa viti maalum ambaye si mwenyeji wa Mkoa huo. Wanawake wa BAWACHA wakaandamana kupinga ukandamizaji huo wa CHADEMA. Hawakusikilizwa.

Zikaja taarifa za Frederick Sumaye kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani. Hili lilijadiliwa kimya kimya wengi wakiwa na mtazamo kuwa Sumaye kajidhalilisha kugombea nafasi hiyo. Hapa suala la Ukaskazini kusimikwa Pwani halikujadiliwa.

Sasa limekuja hili la Patrick Ole Sosopi kugombea Uenyekiti wa CHADEMA kanda ya Ziwa Nyasa. Hili limeanza kupigiwa kelele. Baadhi ya wana CHADEMA hasa kwenye magroup ya facebook wameanza kupaza sauti kuwa kinachofanywa na CHADEMA Makao Makuu 'kuimport' watu wa Kaskazini kugombea uongozi kwenye kanda zingine hakika halikubaliki. Ikumbukwe kuwa karibu safu yote ya Wakurugenzi wa CHADEMA Makao Makuu wanatoka Kanda ya Kaskazini. Sasa kanda zingine wameanza kuwapangia nani awaongoze kitu ambacho si sahihi.

Swali la kujiuliza, je ni kweli CHADEMA hawana watu sahihi wa kuongoza chama kwenye kanda tofauti na wale wanaotoka Kaskazini? Au kuna nini nyuma ya pazia?
 
Dah. Hii sasa ni hatari. Kwa hiyo ni wa Kaskazini tu ndio wanaoweza kuongoza?
images
 
sasa hivi wasukuma wanawekwa kila mahali,kama wewe sio msukuma huna nafasi.

hata watu wa kaskazini waliokuwa na nafasi wamebambikwa kesi,wewe hesabu tu waliotundikwa kesi ni wa wapi
 
Nakumbuka bunge lilopita Shinyanga(sasa Shinyanga na Simiyu) ilikuwa na wabunge wanne was kuchaguliwa ila viti maalumu mmoja tu wakati Kilimanjaro ilikuwa na wabunge watatu wa kuchaguliwa lakini viti maalum walikuwa 10+. Chadema iliiangalie hili kwa jicho LA tai.
 
Yalianza malalamiko Mkoa wa Ruvuma kuwa CHADEMA wameteua mbunge wa viti maalum ambaye si mwenyeji wa Mkoa huo. Wanawake wa BAWACHA wakaandamana kupinga ukandamizaji huo wa CHADEMA. Hawakusikilizwa.

Zikaja taarifa za Frederick Sumaye kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani. Hili lilijadiliwa kimya kimya wengi wakiwa na mtazamo kuwa Sumaye kajidhalilisha kugombea nafasi hiyo. Hapa suala la Ukaskazini kusimikwa Pwani halikujadiliwa.

Sasa limekuja hili la Patrick Ole Sosopi kugombea Uenyekiti wa CHADEMA kanda ya Ziwa Nyasa. Hili limeanza kupigiwa kelele. Baadhi ya wana CHADEMA hasa kwenye magroup ya facebook wameanza kupaza sauti kuwa kinachofanywa na CHADEMA Makao Makuu 'kuimport' watu wa Kaskazini kugombea uongozi kwenye kanda zingine hakika halikubaliki. Ikumbukwe kuwa karibu safu yote ya Wakurugenzi wa CHADEMA Makao Makuu wanatoka Kanda ya Kaskazini. Sasa kanda zingine wameanza kuwapangia nani awaongoze kitu ambacho si sahihi.

Swali la kujiuliza, je ni kweli CHADEMA hawana watu sahihi wa kuongoza chama kwenye kanda tofauti na wale wanaotoka Kaskazini? Au kuna nini nyuma ya pazia?
HAKUNA YA KUJADILI ZAIDI YA CHADEMA...HAKUNA HABARI DUNIANI AU TZ??
 
kama tuhuma hizi ni za kweli na si propaganda basi chadema kinaelekeaa kukosa sifa ya kujipambanua kama chama cha kitaifa na si cha kikanda. naomba kina ben saanane waje wathibitishe haya ili sisi wanchama wengine tupate mwanga
 
sasa hivi wasukuma wanawekwa kila mahali,kama wewe sio msukuma huna nafasi.

hata watu wa kaskazini waliokuwa na nafasi wamebambikwa kesi,wewe hesabu tu waliotundikwa kesi ni wa wapi
Aisee!..ndio maana wasukuma wanasema sasa hivi ni zamu yao.
 
Hizi ni fikra za kinyang'au kugawa watu kwa misingi ya kikanda, kikabila, kidini n.k, watu hawaulizani hayo mambo, utaifa kwanza hayo mengine peleka kwa wajinga wenzio ambao katika dunia ya Leo bado wanaulizana makabila
 
Yalianza malalamiko Mkoa wa Ruvuma kuwa CHADEMA wameteua mbunge wa viti maalum ambaye si mwenyeji wa Mkoa huo. Wanawake wa BAWACHA wakaandamana kupinga ukandamizaji huo wa CHADEMA. Hawakusikilizwa.

Zikaja taarifa za Frederick Sumaye kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani. Hili lilijadiliwa kimya kimya wengi wakiwa na mtazamo kuwa Sumaye kajidhalilisha kugombea nafasi hiyo. Hapa suala la Ukaskazini kusimikwa Pwani halikujadiliwa.

Sasa limekuja hili la Patrick Ole Sosopi kugombea Uenyekiti wa CHADEMA kanda ya Ziwa Nyasa. Hili limeanza kupigiwa kelele. Baadhi ya wana CHADEMA hasa kwenye magroup ya facebook wameanza kupaza sauti kuwa kinachofanywa na CHADEMA Makao Makuu 'kuimport' watu wa Kaskazini kugombea uongozi kwenye kanda zingine hakika halikubaliki. Ikumbukwe kuwa karibu safu yote ya Wakurugenzi wa CHADEMA Makao Makuu wanatoka Kanda ya Kaskazini. Sasa kanda zingine wameanza kuwapangia nani awaongoze kitu ambacho si sahihi.

Swali la kujiuliza, je ni kweli CHADEMA hawana watu sahihi wa kuongoza chama kwenye kanda tofauti na wale wanaotoka Kaskazini? Au kuna nini nyuma ya pazia?
Samahani mkuu Lizaboni ivi wewe huwa unatoka kanda gni?...cyo kwa nia mbaya mkuu.
 
Back
Top Bottom