Kitendo cha Bunge kuendelea kuwakumbatia wabunge waliovuliwa uanachama wao na Chadema, kinaonyesha udhalilishaji wa mhimili wa Mahakama?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,130
Tulipokea taarifa jana kuwa Mahakama Kuu, chini ya Jaji John Mgeta, kuwa ameyatupilia mbali maombi ya wabunge 19, wakiongozwa na Halima Mdee, waliofungua shauri lao Katika Mahakama hiyo kupinga kuvuliwa uanachama wao na kilichokuwa chama chao cha Chadema.

Ikumbukwe kuwa wabunge hao mwezi November 2020, walivuliwa uanachama wao na Kamati Kuu ya Chadema.

Hata hivyo uamuzi huo wa Chadema "ulidhihakiwa" sana na aliyekuwa Spika wa wakati huo, Job Ndugai na akadai kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya mwisho wa wabunge gani waendelee kuwepo Bungeni, kwa hiyo akawahakikishia wabunge hao wasitishike na mtu yoyote, kwa kuwa yeye atawalinda.

Kama tujuavyo ni kuwa Spika Ndugai alijiuzuru nafasi hiyo ya u-Spika na aliyerithi nafasi yake, Tulia Ackson, tarehe 16/5/2022 naye alitoa msimamo wake, baada ya kupata barua toka Chadema, kuwa Baraza Kuu (ambalo wabunge hao walikata rufaa zao) chama hicho kimeafiki uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu, ya kuwavua uanachama wao, kuwa yeye kama Spika mwenye Shahada ya PhD ya sheria ni lazima afuate sheria na kwa kuwa wabunge hao wamelipeleka suala lao mahakamani, kwa hiyo itabidi asubiri uamuzi huo wa Mahakama, na kama Mahakama nayo italitupilia mbali shauri hilo, itabidi alazimike kuutii mhimili huo wa Mahakama.

Jana Mahakama Kuu imeyatupilia mbali maombi hayo ya akina Halima Mdee na wenzake 18, pia Mahakama hiyo pia imelitupilia mbali ombi lao la kutaka waendelee na ubunge wao.

Kama tujuavyo pia kwa mujibu wa wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge yeyote ni LAZIMA awe mwanachama wa chama cha siasa.

Leo tarehe 23/6/2022 wameonekana wabunge hao waliovuliwa uanachama wao na Chadema, baadhi yao wakiuliza maswali ndani ya Bunge.

Nimuulize maswali mepesi tu Spika wetu, Tulia Ackson, je yeye ameamua kwa makusudi kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, wakati akijua kuwa hata Mahakama, aliyotuambia kuwa ikifikia uamuzi, hata yeye itabidi aitii Mahakama hiyo?

Je, kwa kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, wakati mchakato wote wa kuwavua ubunge umeshafika tamati, je hiyo ni ishara ya wazi kabisa kuwa mhimili wake wa Bunge umeupuuza mhimili mwenzake wa Mahakama na kuuona kuwa si lolote wala chochote?
 
Hukumu imetolewa jana mchana hivyo nadhani kuanzia leo asubuhi mamlaka zinazohusika zinaandaa nyaraka za kisheria ili kutekeleza hukumu ya mahakama. Kuandaa nyaraka na kuzifikisha sehemu husika kwa utekelezaji kunahitaji muda na umakini!

Tuvute subira!
 
Kwa taarifa yako ni kuwa Bunge limeshaarifiwa "officially" kuhusu uamuzi huo wa mahakama
 
Wee mpuuzi haujui kuwa hao wanalipwa mapesa mengi wakati wao si wabunge, pesa hizo ni zetu.
Kodi yenyewe hulipi, what I mean hao wenzenu wanajua wanacho kifanya, hizo sakata ziko well planned, kama hujasoma mzumbe, ilboru, kilakala, huwezi kuelewa kitu
 
Kumbe mnafundishwa kudharau sheria na katiba! Ndiyo sababu nchi inaendeshwa bila katiba.
 
Wengi mtabisha tu lakini katiba ni makaratasi tu spika Tulia hataifata hiyo katiba covid 19 wataendela kula pesa za wanuka jasho na hakuna kitu watafanywa
 
Tulipokea taarifa jana kuwa Mahakama Kuu, chini ya Jaji John Mgeta, kuwa ameyatupilia mbali maombi ya wabunge 19, wakiongozwa na Halima Mdee, waliofungua shauri lao Katika Mahakama hiyo kupinga kuvuliwa uanachama wao na kilichokuwa chama chao cha Chadema.

Ikumbukwe kuwa wabunge hao mwezi November 2020, walivuliwa uanachama wao na Kamati Kuu ya Chadema.

Hata hivyo uamuzi huo wa Chadema "ulidhihakiwa" sana na aliyekuwa Spika wa wakati huo, Job Ndugai na akadai kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya mwisho wa wabunge gani waendelee kuwepo Bungeni, kwa hiyo akawahakikishia wabunge hao wasitishike na mtu yoyote, kwa kuwa yeye atawalinda!

Kama tujuavyo ni kuwa Spika Ndugai alijiuzuru nafasi hiyo ya u-Spika na aliyerithi nafasi yake, Tulia Ackson, tarehe 16/5/2022 naye alitoa msimamo wake, baada ya kupata barua toka Chadema, kuwa Baraza Kuu (ambalo wabunge hao walikata rufaa zao) chama hicho kimeafiki uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu, ya kuwavua uanachama wao, kuwa yeye kama Spika mwenye Shahada ya PhD ya sheria ni lazima afuate sheria na kwa kuwa wabunge hao wamelipeleka suala lao mahakamani, kwa hiyo itabidi asubiri uamuzi huo wa Mahakama, na kama Mahakama nayo italitupilia mbali shauri hilo, itabidi alazimike kuutii mhimili huo wa Mahakama.

Jana Mahakama Kuu imeyatupilia mbali maombi hayo ya akina Halima Mdee na wenzake 18, pia Mahakama hiyo pia imelitupilia mbali ombi lao la kutaka waendelee na ubunge wao.

Kama tujuavyo pia kwa mujibu wa wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge yeyote ni LAZIMA awe mwanachama wa chama cha siasa.

Leo tarehe 23/6/2022 wameonekana wabunge hao waliovuliwa uanachama wao na Chadema, baadhi yao wakiuliza maswali ndani ya Bunge.

Nimuulize maswali mepesi tu Spika wetu, Tulia Ackson, je yeye ameamua kwa makusudi kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, wakati akijua kuwa hata Mahakama, aliyotuambia kuwa ikifikia uamuzi, hata yeye itabidi aitii Mahakama hiyo?

Je kwa kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, wakati mchakato wote wa kuwavua ubunge umeshafika tamati, je hiyo ni ishara ya wazi kabisa kuwa mhimili wake wa Bunge umeupuuza mhimili mwenzake wa Mahakama na kuuona kuwa si lolote wala chochote?
Dharau.Kwani mbwa kubweka kunamtisha mfugaaji
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom