mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,843
- 8,232
Ikinyesha mvua lawama,jua likiwaka lawama,si ajabu Mungu aliwachoka binadamu akapumzika siku ya saba.Tumshukuru Mh Rais kwa kutujengea fly over maarufu kwa jina la Mfugale. Kwa kweli inatusaidia kutuvukisha pale tazara kwa speed na kwenda kututupia pale Quality Centre kukumbana na Folen inayoanzia njia panda ya Chang'ombe Veta kuja tazara.
Zamani tulikuwa tunachelewa kufika kwenye ile folen na mara nyingi tulikuwa tukifika tunaikosa foleni ile.lakini kwa sasa alhamdulilah tunaiwahi na pale tunakaa kama nusu saa hivi. Si haba.
Mara nyingi nmekutwa na bahati hii ya kuwahi pale darajani kwenda kukutana na ile folen inayofikia pale quality centre.siku nyingine naweza pata bahati mbaya nikaikosa nikaenda kuikutia kule mbele ngozi.
Yote kheri.tunashukuru kwa daraja hili kutunyanyua huku na kwenda kutubwaga kule. Tuendelee kuombeana wadau.
View attachment 941904