Kitendawili msingi cha Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitendawili msingi cha Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Expedito Mduda, Dec 9, 2010.

 1. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tanzania ni tajiri katika rasilimali na bado watanzania wengi ni maskini. Kwa nini? Hiki
  ni kitendawili kikubwa ambacho tunapaswa kukijibu.
  Umaskini katika Tanzania sio ugonjwa ambao tiba yake haipatikani kwa urahisi. Kwa
  kweli umaskini tulionao huku tukiwa tumejaliwa rasilimali nyingi na utajiri mwingi
  unaotokana na mchakato wa mambo mengi yanayokuwepo kwa wakati mmoja.
  Hali tuliyo nayo imeletwa na mchanganyiko wa mambo mengi. Tunapaswa kuchunguza
  na kuchanganua mambo hayo na hasa tukijiangalia sisi wenyewe, mienendo yetu, na
  kisha tuelewe ukweli wetu, mazuri na kasoro zetu. Kuondokana na umaskini, ni lazima
  kufuata mchakato wa kubadilika. Mwenye wajibu katika kuongoza mchakato huo ni sisi
  wenyewe. Ni lazima tuwe viongozi wa mchakato huo. Haifai kuwaachia watu wa nje,
  wafadhili, ama fedha kutoka kwingine popote. Hatuwezi kufaulu kwa kujifunza na
  kupokea njia zilizosaidia nchi nyingine. Kikwazo cha maendeleo yetu ni utegemezi na
  kukosa uwajibikaji miongoni mwa mawakala katika jitihada za kuleta maendeleo.
  Kukosa uwajibikaji ndio sababu kuu na jambo kuu linalosababisha umaskini wetu. Ni
  lazima, kwa hiyo, tujiwajibishe wenyewe katika kujinasua na mtego huu. Lazima
  tujisumbue na tuhangaikie kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu tukitumia ubunifu wetu
  wenyewe na rasilimali zetu wenyewe.
  Mafisadi na kutokuwa na uaminifu ni vikwazo vikubwa sana katika kujiletea maendeleo! Watanzania tusimame kidete kuhakikisha mambo hayaendelei kuwa hivi yalivyo na hatua ya kwanza kubwa ni kuhakikisha tunapata katiba mpya!!!!!!!!!
   
 2. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maneno meeengi umeandika ambayo ni pumba!
  Ungeandika hapo penye red tu ungeeleweka!
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  usimkatishe tamaa bwana kama uwezi kuchangia waachie wengine watachangia
   
Loading...