Kitendawili kimetegwa - Kikwete Tegua...

Mzee Mwanakijiji,

uliyoyasema kwa kweli sina cha kuongeza, it is the whole truth.

Big up
 
MMM

Hoja yako ni nzuri na inapaswa kuungwa mkono.

Upungufu ninaouona katika hoja yako, ni pale unapotoa mwelekeo wa kwamba matatizo yote katika mchakato huu yanaletwa au kusababishwa aidha na Kikwete binafsi kama rais au na Chama chake. Kwa hili natofautiana na wewe.

Bila kujali hoja ya katiba mpya ni ya nani, ukweli upo pale pale kuwa mchakato wa katiba mpya umeanza. Kwa maoni yako mchakato huu unatokana na Rais pamoja na ikulu yake. Je hilo ni kosa? Rais kama kiongozi wanchi hii, hana jukumu la kujenga mwelekeo wa nchi hii? Kwa rais kuamua kuwaongoza watu wake katika jambo kubwa kama hili amekwenda kinyume na kazi zake? Ulitegemea nani mwingine atuongoze katika jambo kubwa kama hili kama si mtu tuliyempa dhamana ya kutuongoza? Kwani nchi yetu ingeingia vitani leo, nani angetuongoza kama siyo rais huyuhuyu hata kama baadhi hatumtaki au hatumpendi?

Hivyo basi, kusema kuwa mchakato huu kuasisiwa na rais ni moja ya mapungufu yake kwangu siafiki na hapo napingana nawewe. Nani kati yetu angemwelewa rais ambaye, jambo kubwa kama hili linaongozwa na mtu asiye kiongozi wetu tuliyemchagua.

Mada yako inamlaumu Rais na Chama chake kwa kutokuwa na majadilliano kati ya CCM/CHADEMA au KIKWETE/SLAA.

Je, CHADEMA wameonesha utayari wowote wa kukaa na CCM? Si hao CHADEMA wanaosema watahakikisha Kikwete?CCm hawafiki 2015? Katika sura hiyo, CCM watakuwa na moyo gani wa kukaa na watu ambao hawaonyeshi hata chembe ya heshima kwa Serikali au Rais aliyeko madarakani? (Rejea kauli ya Mbowe, mimi nachaguliwa na wananchi, RC anateuliwa na Rais) Mbowe anatoa kauli ya kuonyesha kuwa amesahau Rais amechaguliwa na Wananchi kutoka pembe zote za nchi na yeye kama mwenyekiti wa CHADEMA amechaguliwa na kundi dogo ndani ya Chama chake.

Mbowe pia amesahau, Rais amepewa mamlaka haya ya kuteua watendaji. Hatuwezi kudharau watendaji eti kwa sababu wameteuliwa na Rais. Hata CHADEMA ikiingia madarakani watakuwepo wateule wa Rais. Kama ma _RC hawatakuwepo anagalau mawaziri watakuwepo ambao ni wateule wa Kiongozi. Je watapaswa kudharauliwa?

Mwisho siafiki kuwa yote ya CCM ni mabaya na yote ya CHADEMA ni mazuri wala kinyume chake.

CHADEMA haijatupa hoja kwa nini wanasusia mjadala wa katiba bungeni. Kama ni swala la kusomwa mara ya kwanza, pili, tatu nk si waliseme humo bungeni?

Kuamua kususia mijadala ni dalili ya kuwa hawataki ionekana wanakubaliana na Serikali au Rais aliyeko madarakani. Ni sawa na hoja yako ndani ya mada hii. (CCM hawapaswi hata kushiriki mijadala ya katiba hi...)

Kwa hiyo tatizo hapa si mara ya ngapi unasomwa bali ni jinsi gani CHADEMA itaonekana inaongoza mchakato huu.

Chama kilichoko madarakani ni CCM na ndicho kinachopaswa kuwaongoza watanzania kwa kipindi hiki katika maswala ya nchi hii.

Naomba kuwasilisha.
 
Nakuunga mkono MM .Kikwete anatakiwa ategue kitendawili hicho.
Nadhani washauri wake ndio wabaya ,wananufaika na mfumo mbovu wa utawala kwa hivyo wanammezesha sumu ya chuki dhidi ya nia njema/umuhimu wa maridhiano.

Kikwete kama angekuwa mtu wa kusoma alama za nyakati angefanya maridhiano ili kuweka taswira njema kwa jamii.Ikumbukwe kuwa japokuwa alichakachua matokeo lakini bado alipata ushindi kidogo sana hivyo ni dhahiri kuwa umaarufu wake kwa jamii upo chini ya 50%.
Kiongozi ambaye hana umaarufu kwa jamii yake huyo sio kiongozi bali ni mtawala (Ruler) na mara nyigi huongoza kwa kufuata hulka/ushabiki wa kundi la watu wachache wanaomzunguka kwa maslahi yake/yao binafsi,kama afanyavyo JK na CCM.
 
Mada iliyoanzishwa ni nyingine na nyie kwa uvivu wenu wa kufikiri mnaanzisha mada nyingine ya kumkosoa Mwita25.Acheni kugeuza jukwaa hili kuwa Facebook
kwa hiyo hukumaliza kusoma .......

Mhhhh ndugu yangu, ndio maana wa Bongo ni wavivu wa kusoma. Hii taarifa aloiandika Mwanakijiji ina urefu gani huo wa kumfanya mtu ashindwe kusoma au hadi achanganye paragraph?

Ndio maana tunaambiwa ukitakaficha pesa kwa M-TZ wewe weka noti katikati ya kitabu cha japo page 200 tu. Kama hii presentation tu waona ni ndefu inakuchanganya, je huu mswada tunaoupigia kelele leo hii ukiwekwa hapa mtandaoni kweli utaweza usoma na kuuelewa???

Anzisha ya kwako tuone itakuwaje mkuu,hii ni ya MMM.

We acha uvivu...

Kama unaona bandiko hilo lina paragraph nyingi ninaamini mambo yafuatayo...

1. Maswada wa katiba haujausoma
2. Hotuba ya Lisu hujasoma
3. Riport ya Mwakyembe kuhusu Richmond uliangalia tu kichwa cha habari
4. ......
 
jinsi siku zinavyokwenda mbele napoteza hamu ya kusoma post za mwanakijiji zamani nilikuwa mfusi na mpenda kusoma post zake na ilitokea nikiona jina lake nilikuwa naacha post zingine kwanza ili nijue mwanakijiji kaandika nini
 
"Tume itasikiliza maoni hayo na baadaye kutengeneza rasimu ya Katiba mpya ambayo baada ya kukubaliwa na Bunge itafikishwa kwa wananchi kutoa ridhaa yao kwa kupiga kura" - JK

"Ni kutokana na hoja hizo Spika akaamua Muswada uendelee kujadiliwa na Bunge na leo Bunge limeupitisha Muswada huo. Baadae Muswada utaletwa kwangu kwa ajili ya kutiwa saini uwe Sheria. Baada ya hapo itabakia kazi yangu na Rais wa Zanzibar kuunda hiyo Tume ili mapema mwakani kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ianze. Lengo letu ni kuwa ifikapo mwaka 2014 zoezi zima liwe limekamilika ili mwaka 2015 tufanye uchaguzi tukiwa na Katiba mpya. Itapendeza tukisherehekea miaka 50 ya Muungano na Katiba mpya. Ni matumaini yangu kwamba wananchi wote watashiriki kwa ukamilifu kutoa maoni yao kwa Tume hiyo" - JK
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ndugu zangu Kitendawili kimetegwa nani atakitegua. Chama cha Mapinduzi kimetaka kutumia madaraka na wingi wake kufanya kile ambacho hakikuwa na hakijawahi kuwa ndani ya ahadi zake. Kimetaka kufanya kitu ambacho hakikupewa ridhaa ya wananchi kukifanya. Sote tunakumbuka vizuri kuwa kampeni nzima ya uchaguzi wa mwaka jana kwa upande wa CCM haikuhusiana KABISA na suala la Katiba Mpya. Katiba Mpya haijawahi kuwa sehemu ya Ilani, ahadi au mipango ya Chama cha Mapinduzi kabla ya Disemba 31, 2010.

Ni uamuzi wa kudandia tena siyo kudandia tu bali kudandia na kushupalia. Leo wanadai kuwa ajenda ya Katiba Mpya ni yao. Lakini wanafanya hivyo wakikataa kabisa kukiri wala kutambua kuwa ajenda hiyo ilikuwa ni ya upinzani kwa miaka ishirini sasa tangu lile kongamano lilillozaa vyama vya upinzani nchini.

Ajenda ya Katiba Mpya imekuwa ni moyo udundao katika mioyo ya wapinzani nchini. Tangu mwanzo ilitambulikana kabisa kuwa mabadiliko ya kweli ya kitaifa hayawezi kutokea kwa kubadili watu tu, kubadili sera tu hata kubadili vyama ilitambulikana kabisa kuwa ni lazima kugusa Kitabu chetu Kitakatifu cha watu wa dini zote ambacho watunzi wake ni sisi wenyewe! Hatuwezi kubadilisha Biblia au Qurani lakini Katiba ni kitu pekee kitukufu ambacho kinatoka kwetu na hicho pekee kinatufunga sote sawa na hivyo kinaweza kubadilishwa na sisi wenyewe tu. Ajenda hii ya Katiba Mpya haiwezi leo kuwa ni ajenda ya CCM na wengine wanakaribishwa kama watoto wasio na kwao! Leo hii tumewaona wabunge wa CCM wakizungumza kwa jazba kana kwamba waliahidi hata mmoja wao kuwa wanataka Katiba Mpya.

Siyo Komba kwa kuimba wala Wasira kwa hasira aliyesimama mwaka jana kutaka Katiba Mpya ndani ya CCM. NONE. Leo wana ujasiri wa kubeza, kukebehi na hata kupiga mkwara wale wanaotaka katiba mpya kwa mfumo ulio wazi, wenye kuweka msingi juu ya wananchi siyo wabunge au Ikulu peke yake! Leo hii watu hawa wana ujasiri wa ulevi wa madaraka kwamba wako tayari kuamuru moto unye kama vile ulivyoteremka kule Sodoma na Gomora kisa tu tumewamua kuwageukia na kuwatazama! Na wapo watu wanaomini kabisa ati ajenda hii inaweza kuongozwa na CCM kwa vile tu CCM iko madarakani! Yaani, watu ambao juzi tu hawakuwa na wazo la Katiba mpya tena wakatubeza, na kutukebehi huku wakishindana kugongana wenyewe kwa maneno wanaweza kuandika mswada wa kusimamia uandishi wa Katiba tukaubali tu kwa vigelegele, ngoma na chereko chereko za vifijo.

Ngoja niliseme hili vizuri tu na kwa uwazi Ee Mungu nisaidie - maana tunazunguka mno - CCM haina uhalali wa madaraka ya kusimamia mchakato wa Katiba Mpya. Inaweza kushirikiana na wengine, inaweza kuzungumza na wengine, lakini yenywe peke yake haina hoja, uwezo, wala mandate (ridhaa) ya kufanya hivyo. Haimo kwenye ajenda yao, na Kikwete alipoamua kufanya hivyo mwishoni mwaka jana hakukuwa na kikao chochote cha Chama cha Mapinduzi ambacho kina madaraka ya kubadilisha sera za CCM. Hakukuwepo na kikao cha Halmashauri Kuu wala Mkutano Mkuu kilichofikia uamuzi wa kuandika Katiba Mpya. Huu ulikuwa ni uamuzi wa Ikulu na Ikulu peke na matokeo yake mswada mzima umezunguka Ikulu!

Wabunge wake hawakutakiwa hata kutoa maoni juu ya Katiba Mpya. Wangeweza kufanya hivyo tu kwanza kwa kukubali kuwa hoja hii ilikuwa inatoka nje yao (kwa wapenzi na wanaharakati) na kuwa kutokana na kutambua huko mchakato mzima kuanzia Alfa yake hadi Omega yake ungehakikisha kuwa watu wote wanashirikishwa siyo wanaburuzwa kwa mikwara ya kitoto na kejeli zisizo na kichwa wala miguu.

Kikwete sasa ametegwa. Kitendawili hiki ni yeye peke yake anatakiwa kukitegua. Alikipiga mwenyewe kwenye hotuba yake ya Disemba 31, 2010 alipotangaza na kutushtua kuwa hatimaye ameona mwanga na nuru ya ajabu ikimzukia na kuwa sasa serikali yake imekubali hoja ya Katiba Mpya . Jambo hili wengine tulilipokea kwa tahadhari tukihofia kile kinachotokea sasa. Tulihofia kuwa kwa vile hoja hii imechukuliwa na Ikulu (Kikwete) basi mchakato mzima utazunguka Ikulu na hivyo ndivyo ilivyokuwa na hapa ndipo kiini cha mgogoro wa sasa kilipo.

Wanaharakati na wanamageuzi nchini, wanayo haki ya kupinga, kukataa na kudhihaki mfumo ambao unapendekezwa na CCM na serikali yake ambao umepuuzia kwa makusudi au kwa sababu ya vimulimuli vya madaraka hoja zote tulizozitoa mwezi Machi. Watanzania ambao wamekuwa wakipigania mabadiliko ya Katiba kuanzia 1992 wanayo haki kabisa siyo tu ya kutoka ukumbini hata kusimama na kuanzisha mwamko wa kupinga kubambikiziwa Katiba Mpya kwa sababu tu watu wana madaraka. Kikwete asaidie kukitegua kitendawili hiki vinginevyo ni yeye ambaye atajiikuta anabeba lawama.

Ndugu zangu, kama sisi sote tutaweka miguu chini na kusema hatusogei na kuamua kugoma tulipo tutalazimishwa kuzungumza na kukaa pamoja wakati damu imemwagika. Hivi kwanini leo Kenya hawapigani mapanga? kwanini leo Zanzibar kuna muafaka, kwanini Zimbabwe kumetulia zaidi kuliko ilivyokuwa miaka michache iliyopita? Ni kwa sababu walifikia kwenye kilele cha kushindwa kuvumiliana. Pande mbili za hizo sehemu zote ziliweka miguu chini na kila mmoja aking'ang'ania upande wake na kukataa kuzungumza na mwingine wala kukubali kwamba yule mwingine yupo. Tangu uchaguzi mkuu wa mwaka jana nimetoa ombi wazi la kusema viongozi wetu wa kisiasa nchini wakae pamoja kuzungumza na siyo kuzungumza tu lakini pia kuwa tayari kukubali upande wa yule mwingine.

Kinachonisikitisha ni kuwa hadi hivi sasa inaonekana watu hawataki kukubali upande wa yule mwingine isipokuwa kwa lazima. "Kubalini msipokubali dola itumike!" wanasema waliolewa ugimbi ule wenye povu la madaraka. Wengine wanasema "msipokubali tutaandamana hadi msitawale" na wengine wanasema "mkiandamana tutawatia pingu hadi mkome" na wengine wanajibu "hamna pingu za kutosha wala magereza ya kufunga fikra". Matokeo yake - watalazimishwa kukaa chini na kuzungumza siku ile tutakapoamka na kusikia watu 50 wameuawa katika siasa! Mtasema tunachuria lakini ndivyo ilivyo mahali pote duniani!

Kikwete tegua kitendawili.

1. Usikubali mswada huu kama ulivyo. Hata wabunge wako waupitishe kwa mbwembwe. Upande wapili hautakubali. Na hamna namna ya kuwalazimisha watu milioni mbili kuukabali. Assadi hadi leo kashindwa anaua watu wake kila siku na bado wanasimama kumpinga. Risasi hazipo za kutosha. Bahati mbaya machozi hayana kikomo... Mkisema kuwa mtaendelea na mchakato na yeyote atakayepinga "atakiona cha moto" well.. mtakuwa mmetengeneza kundi kubwa la wanaowapinga na uzoefu unaonesha kuwa Watanzania nao ni wanadamu wakivuka mstari wa 'sina cha kupoteza isipokuwa utu wangu' tutalia na kusaga meno.

2. Pande mbili zikae chini kuzungumza na katika hili ni utayari wa Rais unasubiriwa. Pamoja na matokeo yale ya uchaguzi mwaka jana nilisema kaa chini na Dr. Slaa mzungumze. Nilimuuliza Dr. Slaa swali hili katika mahojiano na alisema yuko tayari wakati wowote kufanya hivyo. Lakini inaonekana kuna watu hawataki. Na hawa wasiotaka wanafanya hivyo labda kwa hofu kuwa ukikubali kuzungumza na Slaa (nyinyi wawili) basi utakuwa umempa ujiko au Kamati Kuu ya CCM na ile ya CDM vikikaa pamoja itakuwa mmeinua CDM. Well, je ni baya kiasi hicho? Kwamba mje kulazimishwa kukaa pamoja wakati miji inaungua, watu wanakimbiana na kukimbizana na polisi wametanda kila sehemu?

Kikwete tegua. Kitendawili hiki ni cha kwako, hakuna wa kukusaidia. Ulikianzisha mwenyewe na kwa namna nakuonea huruma kwa sababu historia inaweza ikakusamehe kwa mengi sana lakini hili la Katiba Mpya likivurundwa sidhani kama jina lako katika historia litakumbukwa kwa haiba nzuri hivyo. Lincoln anakumbukwa kwa mengi lakini la kutangaza emancipation ya watumwa kumemuweka kwenye level nyingine kabisa. Naamini jinsi utakavyosimamia mchakato wa Katiba Mpya bila kuonekana umeulazimisha ndivyo historia itakavyokukumbuka. Kwanini tufike huko kama tunaweza kuepuka kwa kukaa pamoja katika hali ya amani?

Kitendawili...
MMM

Mkuu unalazimisha "NDOA"

Nani atakuwa mke Chadema au CCM?

Ajenda hiyo ya kukaa na chama chochote cha siasa si ajenda ya chadema wanajitolesha sana..
 
Nakuunga mkono MM .Kikwete anatakiwa ategue kitendawili hicho.
Nadhani washauri wake ndio wabaya ,wananufaika na mfumo mbovu wa utawala kwa hivyo wanammezesha sumu ya chuki dhidi ya nia njema/umuhimu wa maridhiano.

Kikwete kama angekuwa mtu wa kusoma alama za nyakati angefanya maridhiano ili kuweka taswira njema kwa jamii.Ikumbukwe kuwa japokuwa alichakachua matokeo lakini bado alipata ushindi kidogo sana hivyo ni dhahiri kuwa umaarufu wake kwa jamii upo chini ya 50%.
Kiongozi ambaye hana umaarufu kwa jamii yake huyo sio kiongozi bali ni mtawala (Ruler) na mara nyigi huongoza kwa kufuata hulka/ushabiki wa kundi la watu wachache wanaomzunguka kwa maslahi yake/yao binafsi,kama afanyavyo JK na CCM.

Afanye maridhiano na nani?

Chadema mko tayari kufunga NDOA? na ccm

Kama hamuwezi hata kushirikiana na vyama vya siasa vingine itakuwa ccm> gosh
 
MMM

Hoja yako ni nzuri na inapaswa kuungwa mkono.

Upungufu ninaouona katika hoja yako, ni pale unapotoa mwelekeo wa kwamba matatizo yote katika mchakato huu yanaletwa au kusababishwa aidha na Kikwete binafsi kama rais au na Chama chake. Kwa hili natofautiana na wewe.

Bila kujali hoja ya katiba mpya ni ya nani, ukweli upo pale pale kuwa mchakato wa katiba mpya umeanza. Kwa maoni yako mchakato huu unatokana na Rais pamoja na ikulu yake. Je hilo ni kosa? Rais kama kiongozi wanchi hii, hana jukumu la kujenga mwelekeo wa nchi hii? Kwa rais kuamua kuwaongoza watu wake katika jambo kubwa kama hili amekwenda kinyume na kazi zake? Ulitegemea nani mwingine atuongoze katika jambo kubwa kama hili kama si mtu tuliyempa dhamana ya kutuongoza? Kwani nchi yetu ingeingia vitani leo, nani angetuongoza kama siyo rais huyuhuyu hata kama baadhi hatumtaki au hatumpendi?

Hivyo basi, kusema kuwa mchakato huu kuasisiwa na rais ni moja ya mapungufu yake kwangu siafiki na hapo napingana nawewe. Nani kati yetu angemwelewa rais ambaye, jambo kubwa kama hili linaongozwa na mtu asiye kiongozi wetu tuliyemchagua.

Mada yako inamlaumu Rais na Chama chake kwa kutokuwa na majadilliano kati ya CCM/CHADEMA au KIKWETE/SLAA.

Je, CHADEMA wameonesha utayari wowote wa kukaa na CCM? Si hao CHADEMA wanaosema watahakikisha Kikwete?CCm hawafiki 2015? Katika sura hiyo, CCM watakuwa na moyo gani wa kukaa na watu ambao hawaonyeshi hata chembe ya heshima kwa Serikali au Rais aliyeko madarakani? (Rejea kauli ya Mbowe, mimi nachaguliwa na wananchi, RC anateuliwa na Rais) Mbowe anatoa kauli ya kuonyesha kuwa amesahau Rais amechaguliwa na Wananchi kutoka pembe zote za nchi na yeye kama mwenyekiti wa CHADEMA amechaguliwa na kundi dogo ndani ya Chama chake.

Mbowe pia amesahau, Rais amepewa mamlaka haya ya kuteua watendaji. Hatuwezi kudharau watendaji eti kwa sababu wameteuliwa na Rais. Hata CHADEMA ikiingia madarakani watakuwepo wateule wa Rais. Kama ma _RC hawatakuwepo anagalau mawaziri watakuwepo ambao ni wateule wa Kiongozi. Je watapaswa kudharauliwa?

Mwisho siafiki kuwa yote ya CCM ni mabaya na yote ya CHADEMA ni mazuri wala kinyume chake.

CHADEMA haijatupa hoja kwa nini wanasusia mjadala wa katiba bungeni. Kama ni swala la kusomwa mara ya kwanza, pili, tatu nk si waliseme humo bungeni?

Kuamua kususia mijadala ni dalili ya kuwa hawataki ionekana wanakubaliana na Serikali au Rais aliyeko madarakani. Ni sawa na hoja yako ndani ya mada hii. (CCM hawapaswi hata kushiriki mijadala ya katiba hi...)

Kwa hiyo tatizo hapa si mara ya ngapi unasomwa bali ni jinsi gani CHADEMA itaonekana inaongoza mchakato huu.

Chama kilichoko madarakani ni CCM na ndicho kinachopaswa kuwaongoza watanzania kwa kipindi hiki katika maswala ya nchi hii.

Naomba kuwasilisha.
Bro you are missing the all point!... Laa ama hakika ni rahisi sana kusoma bandiko la mtu lakini sii rahisi kulielewa..

1. Katiba sio swala la rais kuongoza mchakato wake bali ni kiongozi wa nchi ambaye anatakiwa kuilinda KATIBA. hata tukienda vitani ni katiba ilompa mamlaka ya kuongoza vita hiyo na sii wahi wa Mwenyezi Mungu.. KATIBA sio yake wala hana ridhaa, ruksa wala mamlaka ya kuunda katiba Mpya kama chaguo lake kwa sababu hatuijengi nchi wala Utaifa kwa mtazamo wake.

2. Mbowe anaposema yeye amechaguliwa na wananchi anazungumza kama Mbunge wa Hai aliyechaguliwa na sio mwenyekiti wa CDM wala maswala ya Chadema, na ndio maana kajifananisha tofauti na RC, huwezi kupachika fikra zako ktk ukweli uliotengana...

3. Ombi la Mwanakijiji kuhusiana na JK akutane na kiongozi ama viongozi wa CDM ni apate kusikiliza maoni yao ambayo hayawapi CDM mamlaka ya kuunda katiba bali awasikie wakimwambia kwamba kabla hatujapitisha sheria ama Katiba mpya kuwa muswada inatakiwa upelekwe kwa wananchi ambao wataamua uundwaji wake.. Dira, miiko na maadili (haramu na halali) vitafuta, ili mradi katiba iwe mwongozo wa Utaifa kwa Watanzania wote..Sio CCM wala CDM wenye mamlaka yoyote juu ya Katiba isipokuwa wananchi hilo ndio pendekezo la Chadema na wamesimama hima kuhakikisha swala hili linatoka kwa wananchi wenyewe. Sielewi kwa nini JK na wanaCCM mnaona ugumu ktk hilo.

Zaidi ya yote haya CCM yenyewe ina wanachama zaidi ya millioni 4, mnao wanachama wengi kuliko vyama vyote combained..Sasa mnaogopa nini kuwapa wanachama wenu nguvu na mamlaka ya maamuzi ktk ujenzi wa katiba Mpya?
 
Bro you are missing the all point!... Laa ama hakika ni rahisi sana kusoma bandiko la mtu lakini sii rahisi kulielewa..

1. Katiba sio swala la rais kuongoza mchakato wake bali ni kiongozi wa nchi ambaye anatakiwa kuilinda KATIBA. hata tukienda vitani ni katiba ilompa mamlaka ya kuongoza vita hiyo na sii wahi wa Mwenyezi Mungu.. KATIBA sio yake wala hana ridhaa, ruksa wala mamlaka ya kuunda katiba Mpya kama chaguo lake kwa sababu hatuijengi nchi wala Utaifa kwa mtazamo wake.

2. Mbowe anaposema yeye amechaguliwa na wananchi anazungumza kama Mbunge wa Hai aliyechaguliwa na sio mwenyekiti wa CDM wala maswala ya Chadema, na ndio maana kajifananisha tofauti na RC, huwezi kupachika fikra zako ktk ukweli uliotengana...

3. Ombi la Mwanakijiji kuhusiana na JK akutane na kiongozi ama viongozi wa CDM ni apate kusikiliza maoni yao ambayo hayawapi CDM mamlaka ya kuunda katiba bali awasikie wakimwambia kwamba kabla hatujapitisha sheria ama Katiba mpya kuwa muswada inatakiwa upelekwe kwa wananchi ambao wataamua uundwaji wake, dira, miiko namaadili (haramu na halali) ili mradi katiba iwe mwongozo wa Utaifa kwa Watanzania wote..Sio CCM wala CDM wenye mamlaka yoyote juu ya Katiba isipokuwa wananchi hilo ndio pendekezo la Chadema na wamesimama hima kuhakikisha swala hili linatoka kwa wananchi wenyewe. Sielewi kwa nini JK na wanaCCM mnaona ugumu ktk hilo.

Zaidi ya yote haya CCM yenyewe ina wanachama zaidi ya millioni 4, mnao wanachama wengi kuliko vyama vyote combained..Sasa mnaogopa nini kuwapa wanachama wenu nguvu na mamlaka ya maamuzi ktk ujenzi wa katiba Mpya?

Mkuu nyie ndio mnawa mis-lead wananchi??

Nani aliyesema kwamba katiba ni ya RAIS?? NONE ila mchakato wake rais atahusika unless otherwise..

Wakutane na chadema??? what is so special with them??? who are they???

Besides wanakubali kuoolewa au kufunga NDOA???
 
Mkuu wangu hili ni swala la logic tu halina sababu ya kubabaishana. Nahodha hawezi kupanga utengenezaji wa meli wala hakuna aliyeshika uchoraji wala utengenzaji wa Meli iwe mpya ama kukuu..

Pengine wewe hujasoma mapendekezo ya Chadema kwani unatakiwa uwe nani ili usikilizwe! Haya ndio mawazo yenu wanaCCM ama kweli hamna tofauti na Madikteta...Ikiwa Jk hajui tatizo la katiba iliyopo ama sisi wananchi tunataka nini, ataweza vipi kuwachagua watu wenye uwezo wa kujenga katiba tuitakayo!
 
Juzi nimezungumza na kiongozi mmoja mstaafu wa juu wa magogoni, na tukagusia hili suala la Katiba. Kwa kauli yake akasema kuwa CCM (chama chake), kwa kutaka kuwanyima CHADEMA umaarufu kwa kutumia hili la katiba, ndiyo wanazidi kuwapa umaarufu zaidi kwa suala hilo hilo.

Ufafanuzi wake.

CHADEMA wamelileta suala la Katiba kama ilani yao ya Uchaguzi. Serikali ikapinga.
Kikwete akatangaza bila kushauriana na wenzake kuwa Katiba mpya linajadilika, na akatangaza kuanza mchakato. CCM wakadandia, wakaipora hoja.

Wakitengeneza Katiba nzuri na ikapendwa na wote, CHADEMA watasema kwa haki kabisa bila wao hilo lisingetokea.
Wakitengeneza Katiba mbovu na watu wakaiponda, CHADEMA watasema kwa haki kabisa kuwa CCM walidandia hoja bila kujua mwelekeo.

Yote hayo mawili yanawapa umaarufu CHADEMA.

Mwenzangu akamuuliza, kwa hiyo Mzee hapo wewe unaonaje? Nini kifanyike, maana sasa watu wanataka Katiba, CCM haikuwa tayari na CHADEMA wamewekwa pembeni? Jibu lake: Wazungumze, wote watu wazima hao. Hakuna lisilowezekana kama nia ya kweli ipo.

Watch for this political figure to start emerging into the Katiba thing kwa siku zijazo. Msishangae pia huo muswada kupitishwa na Bunge, na Kikwete kuukalia bila kufanya chochote katika kupima upepo na vuguvugu.
 
siasa mkuu ahitaji ubabe kama yanayofanyika sasa. Ubabe wa rais mgabe huko wapi kabaki kuwa rais hasiyekuwa na tija kwa maisha ya wazimbabwe. Nini hasa serkali inataka kufanya.

swali langu je ninani ajuaye rais anayekuja 2015. (ni edward, sio moringe, a aah! Ni ngoyae wa lowassa)

nakumbuka aliyekua rais wa zambia ndg kennedy kaunda alifanya kama haya kwa lengo mazuri ya chama chake. Rais chiluba alimsweka ndani licha ya kumfanyia kampeni kama sikosei.?
......penye blue masenator
 
MMM

Hoja yako ni nzuri na inapaswa kuungwa mkono.

Upungufu ninaouona katika hoja yako, ni pale unapotoa mwelekeo wa kwamba matatizo yote katika mchakato huu yanaletwa au kusababishwa aidha na Kikwete binafsi kama rais au na Chama chake. Kwa hili natofautiana na wewe.

Bila kujali hoja ya katiba mpya ni ya nani, ukweli upo pale pale kuwa mchakato wa katiba mpya umeanza. Kwa maoni yako mchakato huu unatokana na Rais pamoja na ikulu yake. Je hilo ni kosa? Rais kama kiongozi wanchi hii, hana jukumu la kujenga mwelekeo wa nchi hii? Kwa rais kuamua kuwaongoza watu wake katika jambo kubwa kama hili amekwenda kinyume na kazi zake? Ulitegemea nani mwingine atuongoze katika jambo kubwa kama hili kama si mtu tuliyempa dhamana ya kutuongoza? Kwani nchi yetu ingeingia vitani leo, nani angetuongoza kama siyo rais huyuhuyu hata kama baadhi hatumtaki au hatumpendi?

Hivyo basi, kusema kuwa mchakato huu kuasisiwa na rais ni moja ya mapungufu yake kwangu siafiki na hapo napingana nawewe. Nani kati yetu angemwelewa rais ambaye, jambo kubwa kama hili linaongozwa na mtu asiye kiongozi wetu tuliyemchagua.

Mada yako inamlaumu Rais na Chama chake kwa kutokuwa na majadilliano kati ya CCM/CHADEMA au KIKWETE/SLAA.

Je, CHADEMA wameonesha utayari wowote wa kukaa na CCM? Si hao CHADEMA wanaosema watahakikisha Kikwete?CCm hawafiki 2015? Katika sura hiyo, CCM watakuwa na moyo gani wa kukaa na watu ambao hawaonyeshi hata chembe ya heshima kwa Serikali au Rais aliyeko madarakani? (Rejea kauli ya Mbowe, mimi nachaguliwa na wananchi, RC anateuliwa na Rais) Mbowe anatoa kauli ya kuonyesha kuwa amesahau Rais amechaguliwa na Wananchi kutoka pembe zote za nchi na yeye kama mwenyekiti wa CHADEMA amechaguliwa na kundi dogo ndani ya Chama chake.

Mbowe pia amesahau, Rais amepewa mamlaka haya ya kuteua watendaji. Hatuwezi kudharau watendaji eti kwa sababu wameteuliwa na Rais. Hata CHADEMA ikiingia madarakani watakuwepo wateule wa Rais. Kama ma _RC hawatakuwepo anagalau mawaziri watakuwepo ambao ni wateule wa Kiongozi. Je watapaswa kudharauliwa?

Mwisho siafiki kuwa yote ya CCM ni mabaya na yote ya CHADEMA ni mazuri wala kinyume chake.

CHADEMA haijatupa hoja kwa nini wanasusia mjadala wa katiba bungeni. Kama ni swala la kusomwa mara ya kwanza, pili, tatu nk si waliseme humo bungeni?

Kuamua kususia mijadala ni dalili ya kuwa hawataki ionekana wanakubaliana na Serikali au Rais aliyeko madarakani. Ni sawa na hoja yako ndani ya mada hii. (CCM hawapaswi hata kushiriki mijadala ya katiba hi...)

Kwa hiyo tatizo hapa si mara ya ngapi unasomwa bali ni jinsi gani CHADEMA itaonekana inaongoza mchakato huu.

Chama kilichoko madarakani ni CCM na ndicho kinachopaswa kuwaongoza watanzania kwa kipindi hiki katika maswala ya nchi hii.

Naomba kuwasilisha.

The Good nafikiri ni mfuatiliaji mzuri wa huu mchakato lakini tatizo lako lipo kichama zaidi,kumbuka wapo wanaharakati ambao sio ccm wala cdm pia wanaupinga huu mswada,hoja ya msingi inayoangaliwa kwenye mchakato ni fair play ambayo itafanya pande zote ziaminiane,hakuna sababu ya msingi inayolazimisha Rais,Rais znz,waziri jmh,waziri znz,mwanasheria jmh,mwanasheria znz ndio wawe wateuzi wa tume itakayokusanya maon,i hawa wote wanatoka chama kimoja na serikali moja na hadidu rejea zinatoka kwa Rais.nafikiri kama kichwa chako kimepoa unaweza ona hisia za mashaka na kengele ya hatari inalia juu ya sababu inayofanya jk atuandalie mauaji. Naunga mkono hoja ya mm
 
"Tume itasikiliza maoni hayo na baadaye kutengeneza rasimu ya Katiba mpya ambayo baada ya kukubaliwa na Bunge itafikishwa kwa wananchi kutoa ridhaa yao kwa kupiga kura" - JK

"Ni kutokana na hoja hizo Spika akaamua Muswada uendelee kujadiliwa na Bunge na leo Bunge limeupitisha Muswada huo. Baadae Muswada utaletwa kwangu kwa ajili ya kutiwa saini uwe Sheria. Baada ya hapo itabakia kazi yangu na Rais wa Zanzibar kuunda hiyo Tume ili mapema mwakani kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ianze. Lengo letu ni kuwa ifikapo mwaka 2014 zoezi zima liwe limekamilika ili mwaka 2015 tufanye uchaguzi tukiwa na Katiba mpya. Itapendeza tukisherehekea miaka 50 ya Muungano na Katiba mpya. Ni matumaini yangu kwamba wananchi wote watashiriki kwa ukamilifu kutoa maoni yao kwa Tume hiyo" - JK

Mkuu ni tume ngapi JK ameziteua na hatujapata jawabu ktk lolote. Tume gani imewahi kufanikisha matatizo yetu toka yale ya Muungano hadi ya Richmond ikiwa hawa watu watachaguliwa na rais ambaye maslahi ya chama chake lazima yazingatiwe kwanza. Kama kweli anajali maslahi ya Watanzania kuna ubaya gani kuzungumza na vyama vingine vya Upinzani na akawashirikisha ktk uchaguzi wa tume hiyo maana sisi wananchi tunataka kuona ushiriki wa vyombo vyote vya kijamii kushiriki ktk kuunda tume. Sisi ni Wanajumuiya wa taasisi mbali mbali za kitaifa na huko ndiko itawezekana kukusanya mawazo yetu.
 
ametoa hotuba yenye mamlaka anayedhani ni utani basi ni mgumu wa kusoma alama za vitendo
 
Back
Top Bottom