Kitchen Parties zinasaidia Kuimarisha Ndoa na Mapenzi au ni tatizo...

SMU
Hapana hili si lengo zima la KP ingawa maana halisi siku hizi imepotea......
Lakini siku zilivyozidi kwenda ikageuka kuwa sherehe ya kumpongeza binti kwa kumpata mwenzi wake au kumletea mama/mzazi wa kike heshima nyumbani (na ndio maana wahusika wakuu huwa ni wanawake zamani ilikuwa wamama watu wazima kisha na wasichana wakaanza kualikwa kukidhi sehemu ya marafiki wa binti)

Ila siku zinavyozidi kwenda ndio maana halisi ya KP inavyozidi kupotea.......... kwa sasa hivi nyingi hazina tofauti na send offs.

That's the point! Thank you.
 
Huwa tunasaidiwa kupata vyombo vya ndani lakini mengineyo hata siamini ,unaweza kuta mama amekaa na mmewe miaka mitano na watoto juu bila kufunga ndoa eti siku akitaka kufunga ndoa anaomba afanyie kicheni party ndo nini hii?
 
huwa najiuliza kama kila wanachofundwa wadada ni kwa mujibu ya mahitaji ya waume zao. Kwa mfano anafundishwa kukata kiuno, kuvaa shanga kiunoni, kumnyenyekea mume, sijui na mengine mengi. Lakini hawajawahi kuwauliza wanaume wanafurahishwa na nini katika ndoa.

pia najiuliza kama huwa wanafanya ufuatiliaji kiwango ambacho mafunzo yao yameboresha mahusiano na ndoa za waliopigwa KP. Au kutafuta kutoka kwa wanaume kwamba wanapenda nini hasa na matatizo ya ndoa ni ya aina gani na ni kwa namna gani yanakabiliwa kwa tija.

otherwise, it is a belief that mwanaume anataka haya na haya which is not necessarily the case
 
Wanapewa mafunzo ya ndoa na mapenzi kwenye mikusanyiko inayoitwa "kitchen Parties". Katika mafunzo hayo wanaambiwa mambo ya mapenzi na hususan jinsi ya kufanya mambo fulani fulani na kuhusiana na mwenza. Matarajio ya mafundisho hayo ambayo hukusanya wanawake wengi ni kuwa mfundwa (kama tunaweza kuita huko ni kufundwa) ni kwamba atakuwa amejiandaa kwa maisha ya ndoa na mapenzi.

Kitchen Parties kimsingi imechukua nafasi ya utamaduni wa unyago ambapo wamama watu wazima ambao wanaheshima katika jamii hutoa mafunzo ya maisha ya ndoa kwa mabinti mara kwa mara (kama siyo mara zote) ni mabikira au ambao hawajawa katika mahusiano ya muda mrefu (wachanga wa mapenzi). Unyago uliongozwa na wale tuliowaita Makungwi. Siri za unyago kwa wamama zetu ni siri wanazoenda nazo kaburini. Mambo ya KP yamekuwa ni gumzo na yanarekodiwa kwenye video siku hizi.

Miaka hii michache iliyopita dada zetu na wadogo zetu wamepelekwa huko (au wamejipeleka wenyewe) na kufanyiwa hizo kitchen parties. Kwa upande wetu sisi wanaume sijui kama tumefaidika na mafunzo hayo au ndio tumepata ubutu wa kisu cha kina dada kujua kuwa na "vidumu" au kuwa promiscuous au kutojali mapenzi ya mume.


Hata hivyo ninabakia kujiuluiza kama maisha ya ndoa na mahusiano kati ya mume na mke yamejengwa au kufaidika na haya mambo ya KP au ni bora njia bora ya kutumia wamama watu wazima kufundisha mambo haya? Ni mama gani leo ambao ana ujuzi wa mambo ya mapenzi kama hawa vijana? Sehemu nyingine tumeona kuwa KPs inahusiana na mambo ya ngono zaidi kuliko mahusiano ya wapendanao kiasi kwamba wadogo zetu na dada zetu wanafikiria mahusiano ya ndoa ni mambo ya ngono tu.

Kitchen parties ni sehemu ya suluhisho ya matatizo ya ndoa au ni sehemu ya tatizo?

Hayo yote ni mawazo ya wanaume.Kwa wanawake wamekuwa wanatumia kucheza uchi.Ninayo video moja jamaa alinitumia hilikuwa kitchen party kinondoni.Uwezi amini ni kama danguro,walianza taratibu mara wakavua brauzi,mara siketi ,wakabaki na kufuli mziki ulipokolea wakafua hizo kufuli.sasa hapo bibiharusi mtarajiwa anafundishwa nini?
 
Hivi hizo "kitchen party" hazina jina la Kiswahili?

Na zilianza lini na kwa nini zikaitwa "kitchen party"? Au zilianzia Uingereza? Nauliza tu....
 
Carmel, ni kweli unayosema ila bado sidhani kama KP ni suluhisho la mahusiano bora kati ya watu wawili ambao wanaenda kuishi pamoja. KP inafanyika siku moja na haizidi lisaa limoja la hayo mashauri utakayopewa na baada ya hapo ni kula, kunywa, kucheza na zawadi. So ukiangalia muda uliotumika katika kumfunda huyo bibi harusi katika hiyo party haizidi one hour. Unadhani huyu aliyefanyiwa KP atakuwa amefaidika zaidi ya yule ambaye hakufanyiwa?

kama hujanielewa ni kwamba hata mimi nakubaliana kwamba hazisaidii kuleta mahusiano bora, badala yake ni kwa ajili ya zawadi na kuparty. Lakini pia si kweli kwamba wote wanafanya mambo ya kipuuzi.
 
ah ah ah anafundwa mziki ukikolea avue lol
Hayo yote ni mawazo ya wanaume.Kwa wanawake wamekuwa wanatumia kucheza uchi.Ninayo video moja jamaa alinitumia hilikuwa kitchen party kinondoni.Uwezi amini ni kama danguro,walianza taratibu mara wakavua brauzi,mara siketi ,wakabaki na kufuli mziki ulipokolea wakafua hizo kufuli.sasa hapo bibiharusi mtarajiwa anafundishwa nini?
 
haaaaaaha Pearl umenifuraisha sana kwaiyo mambo ikikolea na nguo zinavuliwa ,kwangu mie nyingi zimekaa kizawadi zaidi maana kuna mafundisho ukisikiliza inabid binti achanganye na zakwakwe kuliko kubeba huo uwendawazimu.

lakini nilishawahi hudhuria moja kwakweli ilikuwa na mafundisho hasaaa na ilikuwa kama tuko kwenye ibada fulani kwaiyo hii inategemea na familia au watu walikunzunguka kufanikisha hilo ni watu wa aina gani .



ah ah ah anafundwa mziki ukikolea avue lol
 
Ok kutokana na michango ya wengi wetu kubase sehemu moja, kwamba KP ni sehemu ya mwanamke kupata zawadi na si vinginevyo(hii ni 98% ya wachangiaji wamesema hivi). Zaidi ya hapo ni uhuni tuunaondelea!! Basi tufike conclusion kwamba kitchen part is nothng than Zawadi za Jikoni. Ok nini kifanyike??
Mtazamo wangu ni kwamba KPs ZIFUTWE....ndiyo...ZIFUTWE!! KWANINI??

1. Kupunguza bajeti ya maandalizi ya KPs-unaweza kuandaa KP kwa bajet kubwa(ukumbi,vinyaji,chakula ,muziki, picha n.k). Halafu zawadi unazopata hata hazilingani na garama za maandalizi.

2. KPs iwe substitute kwa Send-Off, coz utaandaa sherehe ya send off tu na sio KP, zawadi zooote zije kwenye hii party.

Mwanajamiione, Pearl,iane na wengineo...mnasemaje hapa?? Hii ni kwasababu KP zimeshachakachuliwa na ilinibidi watu ambao tayarri wapo kwenye ndoa ndio wahusika wakuu kwenye hii kitu,lakini sasa hivi mashosti wako woooooote wasioolewa nao wapo ndani ya nyumba...eeeh???kyawa???
 
party ya jikoni kwa kiswahili... maana yake ni kupeana vyombo vya kukusaidia kumpikia mumeo

naskia siku hizi wanafundishwa maujuzi ya kitandani
 
party ya jikoni kwa kiswahili... maana yake ni kupeana vyombo vya kukusaidia kumpikia mumeo

naskia siku hizi wanafundishwa maujuzi ya kitandani

hakuna kitu kama hiyo...mkuu fuatilia wachangiaji wengi...hii kitu hamna tena siku hizi!! ni kupeana vyombo tu..bada ya hapo ni kusaula kwa kwenda mbele, labda zile KPs chache za heshima,kama baadhi ya member walivyo-toa ushuhuda!!
 
Kitchen party siku hizi ni kama party zingine tu! Bibi harusi anapata vyombo vya ndani vinaenda kumsaidia huko kwake mafunzo anakuwa keshapewa akiwa ndani kwa wiki mbili wengine mwezi mzima, kwa hiyo siku hizi mkeo akienda kp ukae home usubiri maujuzi imekula kwako
 
Kitchen party siku hizi ni kama party zingine tu! Bibi harusi anapata vyombo vya ndani vinaenda kumsaidia huko kwake mafunzo anakuwa keshapewa akiwa ndani kwa wiki mbili wengine mwezi mzima, kwa hiyo siku hizi mkeo akienda kp ukae home usubiri maujuzi imekula kwako
Na kwa mtazamo wangu mie zinachangia pia katika kuvunja ndoa kwa sababu hata ile maana haisi ya baba kuwa kichwa cha nyumba kinapotea kwa sababu kwa vizazi vyetu vya dot com ambavyo heshima na maadili ni vya kuvuta na kamba kama binti wa dot com kaingia nyumbani kwako na kiiiiila kitu mpaka kitanda, makochi dijui dining sets, deepfreeza n.k. siku mkikorofishana hakawii kukwambia anakuweka mjini .............au kukunyima kwani utamfanya nini maana mpaka uwanja wa mazoezi kauleta yeye ni mali yake ................hahahahaaaaaaaaaaaa wakaka wa siku hizi kazi mnayo
 
Kitchen party kwa Kiswahili zinaitwaje? Au hazina jina kwa Kiswahili?

Na huu utaratibu asili yake wapi? Uingereza?

Sidhani kama kuna mtu kati yenu anayejua. Kama yupo na ajitokeze ajibu maswali yangu kwa kiwango cha kuridhisha.
 
Nafikiri kitchen party inategemea nani anafundisha....kuna kitchen party unaenda unafikiri uko ibadani na mafunzo ni ya utulivu na yenye muelekeo wa kidini....aina ya mama,shangazi na marafiki ulionao inaweza determine aina ya kitchen party msichana atakuwa nayo....Kitchen party hazifanani,kuna nyingine unaenda hata kuangalia unaona tabu na kuna nyingine unaondoka umelemewa na uzito wa mafundisho uliyopewa ma kina mama....Kweli kitchen party nyingi zimekuwa kingono na zenye ku-focus kwenye zawadi zaidi na hazizingatii maadaili wala mafundisho ya kidini...kuna nyingine hadi wanashawishi watu wafanye vitu vya ajabu ili waweze kuwafanya wanaume wasitoke nje ya ndoa....ila bado kuna kitchen party decent na zenye maana ya msingi wa kutoa mafunzo kwa binti kuelekea kwenye ndoa....
Kuhusu kufundisha watu wanaojua kuhusu walimu wenyewe, si kweli,hakuna anayejua kila kitu,daima kuna jambo la kujifunza kwenye mkusanyiko wa kinamama....waweza jua kukata kiuno sana lakini hata namna ya kumshawishi mume wako huna.....hakuna anayejua kila kitu!
 
Binti wa kisasa utamfundisha nini asichojua. Nilienda kwenye kitchen party moja mdada alikuwa anaolewa na mdhungu, basi wakitoa somo yeye anaguna tu. Mama yake akamwambia unanitia aibu. Akamwambia mama mnayonambia yote yanaingia sikio moja yanatokea la pili. Alikaa kwenye ndoa mwaka. Mtoto usimfunde toka umemzaa unategemea ataelewa somo la masaa mawili!
 
Experience is a good teacher. Hata wafundishe mazuri kiasi gani, ni mpaka mtarajiwa akutane na tukio ndio ataelewa somo. Sasa hizo theory tena mnataka mtu a catch zote kwa masaa ataelewa wapi! Mimi nilifanyiwa kitchen party ukiniuliza leo walikwambia nini hata moja kichwani hamna!

huwa najiuliza kama kila wanachofundwa wadada ni kwa mujibu ya mahitaji ya waume zao. Kwa mfano anafundishwa kukata kiuno, kuvaa shanga kiunoni, kumnyenyekea mume, sijui na mengine mengi. Lakini hawajawahi kuwauliza wanaume wanafurahishwa na nini katika ndoa.

pia najiuliza kama huwa wanafanya ufuatiliaji kiwango ambacho mafunzo yao yameboresha mahusiano na ndoa za waliopigwa KP. Au kutafuta kutoka kwa wanaume kwamba wanapenda nini hasa na matatizo ya ndoa ni ya aina gani na ni kwa namna gani yanakabiliwa kwa tija.

otherwise, it is a belief that mwanaume anataka haya na haya which is not necessarily the case
 
Back
Top Bottom