Kitchen Parties zinasaidia Kuimarisha Ndoa na Mapenzi au ni tatizo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitchen Parties zinasaidia Kuimarisha Ndoa na Mapenzi au ni tatizo...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, May 9, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wanapewa mafunzo ya ndoa na mapenzi kwenye mikusanyiko inayoitwa "kitchen Parties". Katika mafunzo hayo wanaambiwa mambo ya mapenzi na hususan jinsi ya kufanya mambo fulani fulani na kuhusiana na mwenza. Matarajio ya mafundisho hayo ambayo hukusanya wanawake wengi ni kuwa mfundwa (kama tunaweza kuita huko ni kufundwa) ni kwamba atakuwa amejiandaa kwa maisha ya ndoa na mapenzi.

  Kitchen Parties kimsingi imechukua nafasi ya utamaduni wa unyago ambapo wamama watu wazima ambao wanaheshima katika jamii hutoa mafunzo ya maisha ya ndoa kwa mabinti mara kwa mara (kama siyo mara zote) ni mabikira au ambao hawajawa katika mahusiano ya muda mrefu (wachanga wa mapenzi). Unyago uliongozwa na wale tuliowaita Makungwi. Siri za unyago kwa wamama zetu ni siri wanazoenda nazo kaburini. Mambo ya KP yamekuwa ni gumzo na yanarekodiwa kwenye video siku hizi.

  Miaka hii michache iliyopita dada zetu na wadogo zetu wamepelekwa huko (au wamejipeleka wenyewe) na kufanyiwa hizo kitchen parties. Kwa upande wetu sisi wanaume sijui kama tumefaidika na mafunzo hayo au ndio tumepata ubutu wa kisu cha kina dada kujua kuwa na "vidumu" au kuwa promiscuous au kutojali mapenzi ya mume.

  Hata hivyo ninabakia kujiuluiza kama maisha ya ndoa na mahusiano kati ya mume na mke yamejengwa au kufaidika na haya mambo ya KP au ni bora njia bora ya kutumia wamama watu wazima kufundisha mambo haya? Ni mama gani leo ambao ana ujuzi wa mambo ya mapenzi kama hawa vijana? Sehemu nyingine tumeona kuwa KPs inahusiana na mambo ya ngono zaidi kuliko mahusiano ya wapendanao kiasi kwamba wadogo zetu na dada zetu wanafikiria mahusiano ya ndoa ni mambo ya ngono tu.

  Kitchen parties ni sehemu ya suluhisho ya matatizo ya ndoa au ni sehemu ya tatizo?
   
 2. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kitchen party kwa mtazamo wangu ni sehemu tu ya kupata vyombo vya jikoni kwa akina mama pia ni sehemu ya kina mama ku party...

  Hayo mafunzo ya siku moja kwakweli sio essence kubwa, sasa hivi kparties zimekaa 'kikazi' zaidi, and am glad I had one maana hivyo vyombo vilitusave mno
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Dah MMJ ni napingana na hili kwa asilimia 100,KPs sio suluhisho la ndoa asilani. Mimi binafsi hapa nina video clips alinipa mshkaji wangu,zipo kama 6 hivi, yaani hayo madudu yanayofanyika ndani ya kitchen part, (wadada mpaka nguo zooooote wanasaula, wale wengine wanajaribu kuwavalisha lakini wapi), na kikubwa zaidi sikuona hata mtu mzima katika ile kitu. Sasa kama mambo yenyewe ndiyo haya nimeapa mke wangu hawezi kwenda kufundwa kwenye kitchen part asilani. Hii nimeapa.

  Sasa angalia!! KPs muundo wake ni kwamba wadada tu na wengi watu wazima ndio wanaoruhusiwa kuingia(sio watoto under 18 wala wanaume) hii ndio maana halisi ya KP. Cha ajabu ni kwamba hizo KPs wapiga muziki ni wanaume,wanaakuwepo ndani, wahudumu wa huo ukumbi ni wanaume...(yaani kwenye hizo clip unawaona wanaume na plate zao wanapitapita). Sasa hii ni nini?? Cha kuchekesha zaidi, huyo mwali wanayemfunda ni mjuzi kwenye naniliiiiu kuliko hao wanaomfundisha, damn it!!! Nothing new yaani. Hapa nakataa hamna funzo lolote.

  Mi nilijaribu kuongea na ma-mdogo kuhusu hii kitu, kumbe wasichana/wanawake wengi wanaanda hizi KPs kumbe lengo kubwa ni kuchangiwa hot-pots,vijiko,glass, vikombe na zawadi nyinginezo. Hii sasa kwa maisha haya ya .com ndio maana halisi ya KPs. Zawadi za dizaini hii bila kufanya KPs basi umeliwa,sio tena yale mambo ya jadi kama wewe MMj ulivyotujulisha hapo juu. BIG NO!!

  MWISHO: Kama hili ni swala la KPs ni muhimu, siku ikifika nitawaita wanamama wachache wenye busara zao, ndugu wengine, watamweka ndani mke wangu mtarajiwa wataongea nae, mwisho wa siku kitaeleka tu, sio biashara hii ya kucheza uchi na kugawana mahot-pot...sina shida nazo.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa KP ni kwa ajili ya vyombo vya ndani..
   
 5. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kaka umeshaoa? na kama hujaoa ikitokea siku unataka kuoa wazazi wa binti wakaamua kumfanyia mwana wao hiyo kitchen party au hata binti mwenyewe aitaka kufanyiwa wewe utakataa? maana hii kama ulivyosema mwenyewe ni zaidi ya kukusanya zawadi kutoka kwa wenzio ambao unakuta mama mtu au binti mwenyewe wameshiriki na kujitoa sana kwa ajili ya wengine sasa hii inakuwa chance yake naye kurudishiwa fadhila. mi sioni kama zina ubaya wowote hadi zionekane mbaya kiasi hicho inategemea tu na mtu mwenyewe, ana marafiki wa aina gani na wazazi wake ni wa aina gani, hii yote itashape aina ya kp atakayofanyiwa. kama unaoa shangingi mwenye marafiki na ndugu waliokubuhu, obvious kp itakuwa ya aina hiyo ya kishangingi. Lakini kama ni mtu anayejiheshimu kp itakuwa ya heshima na tena nimeshuhudia kp zikiendeshwa kibiblia na maneno ya hekima tele kutoka kwenye biblia, hizi zinaendeshwa na wamama wenye adabu zao, wanaomjua Mungu. So it all depend on a person herself. mwisho si kweli kp ni mbaya kama mnavyotaka tuamini... after all ni sehemu ya wakina mama kisocialize na kuwa happy.
   
 6. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nadhani lengo lake mwanzo halikuwa hilo, ila naona ni kama evolution inaendelea kutoka unyago na mafunzo ya kuishi na mume kuelekea zaidi kwenye kijiwe cha wanawake kuparty na kutoa zawadi. Kwa ufupi kp inachukua zaidi muonekano wa zawadi kushinda hayo mafundisho.
   
 7. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kama KPs ni sehemu ya akina mama sasa mijibaba inafuata nini huko,kupigisha mziki??au??
  Sikia, mi bado sijaoa, ila refence ya wanamama wengi wanavyoongea hadi maza angu mdogo ni kwamba KPs is nothing rather than getting f.u.c.k.n gifts...ambazo mi sina time nazo. Wahindi hata kama ni arranged marriage huwa wanapeana magari, viwanja na vitu vingine vya maana,sembuse hizo hot-pot. Kama ni zawadi atapewa siku ya harusi au Send-off..finish!!!
  Sifanyi KP kwa mke wangu mpaka nijiridhishe!! Na hili nitaliweka wazi tangu nipo kwenye uchumba!!
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kina dada mtujuze.

  Mie hujionea ni sherehe za kupeana zawadi, (labda wanaunganisha bridal shower humo humo kuokoa muda na gharama,) kuonyeshana madoido ya nyonga na style za mishono ya 'super wax.'

  Halafu siku hizi mmezua na Baby Shower,...uhhh!...

  - 'michango culture!' -
   
 9. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ishu ni kwamba si wewe unayemfanyia kp, ni wazazi wake mainly wamama, hata baba yake haimhusu, sasa wewe ukisema humfanyii sikuelewi, halafu inategemea na mwanamke unayemuoa, kwa mfano mimi na imani niliyonayo kwamba kp haina tatizo, especially ukiifanya kwa adabu, halafu nipate mchumba mwenye mawazo kama yako unilazimishe nisifanye just because u dont want sidhani kama hiyo ndoa itakuwepo maana huo utakuwa ni udikteta, this is abt a girl and her female parents and relatives, and friends, you have got no say in it. Unachoweza kufanya ni kumshauri afanye kp ya heshima ambayo haina uchafu wowote, na hii inarudi palepale kama unaemuo ni decent person hutahitaji hata kusema. You dont understand, hii imekaa kike zaidi n yes kuna wanawake ambao hawapendi kp na hawafanyi, na kuna wanaopenda kp na ni dream yao kufanya so it all depend na huyo utakayekuwa unamuoa really.
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Lengo la hizo KP ni kupata zawadi zaidi kama wengi wanavyosema na sio mbadala wa unyago...unakuta dada ambae tayari ana mtoto au aliolewa na kuachika, akiolewa tena eti anafanyiwa KP..............inashangaza kwa kweli!!
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ok, well-noted!! Kwa sababu mi ndio nitakayeoa,nadhani nitakuwa na sauti hata kama sihusiki kwenye KP,so my voice will have effect on it....mi ninavyojua ndoa is not all abt KP,kama yy ataona hamna ndoa without KP...then nitacheki altenatives nyingine...na ndio maana nasema mpaka nijiridhishe.

  So Carmel...ahsante kwa kuendelea kunichanganulia hii kitu.
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hizi K.p ni uoza hasa za huku mjini
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wanafundishana mambo ya ajabu huko...
  Faida yake imebaki kua zawadi tu!!
   
 14. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Carmel, ni kweli unayosema ila bado sidhani kama KP ni suluhisho la mahusiano bora kati ya watu wawili ambao wanaenda kuishi pamoja. KP inafanyika siku moja na haizidi lisaa limoja la hayo mashauri utakayopewa na baada ya hapo ni kula, kunywa, kucheza na zawadi. So ukiangalia muda uliotumika katika kumfunda huyo bibi harusi katika hiyo party haizidi one hour. Unadhani huyu aliyefanyiwa KP atakuwa amefaidika zaidi ya yule ambaye hakufanyiwa?
   
 15. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndio shida sasa hiyo. Unyago zamani ulikuwa unafanyika maana binti alikuwa bado ni virgin kwa hiyo kuna mambo muhimu alikuwa lazima aelekezwe, sasa siku hizi sijui wanaelekezwa nini tena wakati asilimia kubwa kila kitu wanajua. Kama Mzee Mwanakijiji alivyosema, "vijana wa leo wana ujuzi wa mambo ya mapenzi kuliko kina mama zetu"
   
 16. LD

  LD JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kitchen part..............Sherehe ya jikoni,
  Kwa ajili ya kupata vyombo.

  Ni sherehe ya vyombo, hata hao wanaofundisha huko hawafanyi wao hayo wanayofundisha.
  Wanaimba nymbo nyingi ambazo kiuhalisia hayafanyiki wala wao hawafanyi.

  Mi nataka kitchen pati ili mnichangie mivyombo tu, mengine nita Google.
   
 17. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Ni kweli mbu,
  maana halisi ya KP,
  Imeshageuzwa kabisa, siku hizi ni kupeana vyombo na kuonyeshana namna ya kukata nyonga,
  Hata hivyo bado mimi si shabiki sana wa hizi KP toka huko nyuma,
  Kwani siku zote sioni ni jinsi gani mafunzo hayo ya siku moja, tena masaa kadhaa,
  yanaweza kuwa na impact kwa huyo mfundwaji katika maisha yake ya ndoa,
  Ki msingi, kama hukufundwa/kulelewa vizuri na wazazi toka katika makuzi yako mpaka umekuwa kigoli,
  basi hiyo KP ya kufundana masaa 3 au 4 haina maana yoyote!!!!!!!
  Bado naegemeza fikra zangu kwa wazazi, binti atajua kuishi na mume kama wazazi waliplay part yao kwenye malezi!
   
 18. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  binti mmoja aliambiwa hivi kwenye kitchen party " mwanangu sufuria haikai kwenye mafiga mawili!!! shurti ili ikae uitengenezee mafiga 3, alafu mwanangu ukibeba ndoo kichwani jua kuna kujikwaa!! shurti mwanangu uwe na kidumu mkononi mama ili ndoo ikidondoka ubakie na kidumu!!! yule mfundaji akaongezea tena kusema, binti sikiaaaa jicho moja likipofuka mwanangu huitwa chongo sio jicho tena!!

  nikashindwa kuelewa kama pale kunajengwa ama kunabomolewa!!!

  Amaaaaaa hizo ndio kitchen party zetu za leo tunazokwenda kuchukua mitandio huko.
   
 19. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  To me KP inategemea inafanya na familia gani(yani binti anatoka ktk familia gani,Dini,uswahili mwingi etc)
  KP lengo lake hasa ni kufunza jinsi ya kuishi na mwenziwako lkn hasa ktk maswala ya jikoni,usafi na mazingira ya nyumba,watoto ambapo muhusika mkuu ni mwanammke.
  Mwanamke anatakiwa kuwa na kungwi wake ambae atamueleza mambo muhimu ya chumbani wakiwa wenyewe huko nyumbani,wiki moja to 2 weeks before ndoa,zen wakati wa KP sasa ni kukumbushwa tu kwa juu juu hasa na kupokea shuhuda za watu mbali mbali kuhusu ndoa.
  Kuna wamama wazuri sana hivi sasa wanaotoa mafunzo ktk KP nyingi ambazo nimeenda na kuona,watu hao wamekaa kwenye ndoa mda mrefu na hivyo hutoa mafunzo mengi lakini yanayotokana na Bible na mafunzo mbali mbali,(si kwamba ndoa zinafanana hapana lkn wanajaribu kumhasa binti ndoa nyingi zinahitaji siri na uvumilivu maana zamani hata kama mama katoka kupigwa na baba mtoto ngum kujua lipi limemsibu,na kamwe siri za nyumbani kutoka nje,so kama ss nowdaiz ukipata ka boyfriend tu mpaka mtaa wa saba watajua)
  Sikatai kuna KP ambazo ni laana hata mtu kuingia kwakweli maana hazitoi mafunzo yyte kwa huyo mtarajiwa mwenyewe thats y I said inategemea na familia hivyo ikoje hasa.
   
 20. CPU

  CPU JF Gold Member

  #20
  May 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hebu fafanua kwa lugha nyepesi hii kauli nielewe
   
Loading...