Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,102
- 2,540
Rais Samia Suluhu Hassan amefichua Siri iliyokuwa imefichika kuhusu gawio kwa serikali yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya mashirika na taasisi za umma huku yakiwa yamepata hasara.
Mkuu huyo wa nchi amesema viongozi wa mashirika hayo walikuwa wakikopa fedha benki na kupeleka gawio serikalini ili kuonesha yanatengeneza faida wakati yalikuwa yakijiendesha kwa hasara.
Hali hiyo ilijitokeza katika uongozi wa awamu ya tano ambapo mashirika ya umma yalitakiwa kutoa gawio serikalini,hali iliyozua maswali kwa yale yaliyotoa gawio ilhali yamepata hasara.
Rais Samia amesema viongozi wa mashirika hayo walikuwa wakihangaika huku na kule kuingia benki kukopa kulinda vibarua vyao,ikifika tarehe wahusika hao wanakuja na cheki zao wanatoa gawio lakini ukweli uzalishaji ni ziro.
======
Rais Samia Suluhu Hassan amefichua siri iliyokuwa imefichika kuhusu mali ya gawio kwa Serikali yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya mashirika na taasisi za umma huku yakiwa yamepata hasara.
Mkuu huyo wa nchi amesema viongozi wa mashirika hayo walikuwa wakikopa fedha benki na kupeleka gawio serikalini ili kuonyesha yanatengeneza faida, wakati yalikuwa yakijiendesha kwa hasara.
Hali hiyo ilijitokeza katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano ambapo mashirika ya umma yalitakiwa kutoa gawio serikalini, hali iliyozua maswali kwa yale yaliyotoa gawio hilo ilhali yamepata hasara.
Rais Samia alitoboa siri hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala na kushuhudia viongozi wa taasisi na mashirika ya umma wakila kiapo cha maadili.
Kauli ya Rais Samia ni ya kwanza kuelezea mchezo huo ambao hata Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikibainisha baadhi ya mashirika kujiendesha kwa hasara.
Katika kile unachoweza kusema ni kuwaweka kitanzi, alisema kinachohitajika sasa kufanyika ni jitihada kubwa kuhakikisha mashirika hayo yanaleta tija kwa Taifa.
“Kwa wale wa mashirika, ukweli ni kwamba mashirika yetu hayafanyi vizuri, machache sana yanayofanya vizuri, kwa hiyo tumewapeleka huko kasimamieni ili yafanye kazi vizuri,” alisema.
Akisisitiza eneo hilo, Rais Samia aliyekuwa makamu wa Rais katika awamu ya tano, alisema, “mimi najua miaka iliyopita kuna kipindi maalumu mashirika yalikuwa lazima yanatakiwa yatoe gawio.”
“Kwa kuwa yalikuwa hayafanyi vizuri, wengi wenu mlikuwa mnahangaika huku na kule kuingia benki kukopa kulinda vibaru a vyenu, ikifika terehe husika hao wanakuja na cheki zao wanatoa gawio lakini ukweli uzalishaji ni ziro.”
Aliwataka wakuu wa mashirika yanayofanya vibaya kujirekebisha kwa kuwa hatakuwa tayari kuwavumilia na hatasita kufanya mabadiliko kila atakapoona mambo hayaendi sawa.
Katika hoja hiyo, Dk Donath Olomi ambaye ni mtaalamu wa uchumi na biashara alisema baadhi ya watu wanaokopa ili kulipa gawio wanajua kufanya hivyo si sahihi lakini wanalazimika kulinda vibarua vyao na kuwa gawio linatakiwa litokane na faida.
Profesa Haji Semboja kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar alisema moja ya makosa yanayofanyika ni viongozi wa mashirika hayo, wakiwemo wakurugenzi, kuteuliwa na Serikali badala ya kufuata mchakato unaotakiwa wa watu kuomba kazi na kufanyiwa mchujo.
Katika hilo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alisema, “ilikuwa inajulikana dhahiri baadhi ya mashirika yalikuwa yanadanganya katika kutoa gawio. Rais kathibitisha tu jambo ambalo wengi tulikuwa tunajua.”
Zitto aliyewahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya mashariki ya umma (PAC) alisema, “mashirika ya umma yaweza kuwa chachu kubwa ya maendeleo iwapo Serikali ikiamua yawe hivyo.”
“Mashirika pia yawe huru kuweka fedha zake kwenye benki wazitakazo ili yawe na uhuru wa kusimamia fedha zao,” Zitto aliongeza.”
Wengine matumbo joto
Rais Samia pia alidokeza kwamba kuna mabadiliko mengine ya viongozi yanakuja kwa ngazi ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri , miji, majini na manispaa pamoja na makatibu tawala wa wilaya.
Katika hotuba yake alimtaka Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa kuwaandaliwa mafunzo maalumu ya kuwakumbusha wajibu wao.
“Tumefanya tathmini ya makundi yote, maDC (wakuu wa wilaya), wakurugenzi, maDas (makatibu tawala wa wilaya), wote, kwa vyovyote vile tutegemee kuna mabadiliko,” alisema Rais Samia.
“Kwa hiyo kila watakaoingia wafanyiwe mafunzo kama watakayofanyiwa wakuu wa mikoa, kila ngazi kwa aina yake ya mafunzo.”
Alisisitiza lengo la mafunzo hayo ni kukumbushana wajibu wa kazi zao ili mtu yoyote asiseme hakujua alipashwa kufanya nini.
Huduma kwa wananchi
Rais Samia alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wakuu wa mikoa na makatibu tawala kujitoa kwa dhati kuwahudumia wananchi kwa kuwa ndiyo jukumu walilokula kiapo kulitekeleza.
“Nendeni mkawahudumie wananchi kwa moyo safi. Huna pengine pa kuhudumia ni Tanzania na ukifanya vizuri Mungu anakunyanyua anakupeleka pazuri, ukifanya vibaya ipo siku ubaya wako utajulikana na utaadhirika,” alisema.
“Mwakilishi wa Rais katika mkoa asiwe na rafiki, kwenda kutengeneza mtandao wa marafiki halafu kazi kwa wananchi hakuna, hilo halikubaliki, hatukuwateua kufanya hayo,” alisema.
Akizungumza kwa sauti ya chini na yenye kutoa ujumbe wa msisitizo, Rais Samia alisema, “tumewatuma mkatumikie wananchi, kafanyeni hivyo bila kuchoka. Kama Rais halali hadi saa tisa usiku wewe usingizi unautoa wapi, mnatuma meseji hadi usiku najibu ina maana silalali, sasa kama mimi silali wewe usingizi unaupataje.”
Magwanda ‘out’
Samia ambaye ni amiri jeshi mkuu, alitoa maagizo kwa wakuu wa mikoa ambao ni wanajeshi na polisi waachane na magwanda kwanza.
“…kwa makanali hatuwatarajii mkivaa kombati wakati mkitekeleza majukumu ya wakuu wa mikoa, ziwekeni pembeni mtazivaa mkirudi jeshini,” alisema.
Kwa miaka ya karibuni umekuwepo mtindi wa viongozi wa kisiasa au watendaji walioteuliwa kutoka jeshini kuvaa magwanda yao ya kijeshi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Chanzo: Gazeti la mwananchi