Kitambulisho cha Taifa

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
7,640
12,235
Heshima kwenu wakuu!
Nimepoteza kitambulisho cha taifa,na nimesharipoti polisi,ofisi ya NIDA hapa mkoani,na nimeshaenda benki kulipia 20k kwa ajili ya kupata kitambulisho kipya.
Swali Je ninawezaje kukipata kwa haraka,niende makao makuu ya NIDA? Kama ndio makao makuu yao yapo wapi kwa Dar?
Asanteni.
 
inachukua miezi mitatu kupata id mpya au iliyopotea, ni maelezo niliyoyapata katika mojawapo ya ofisi za nida.
 
Mimi Sina hata kitambulisho nitakipataje wadau nimewahi kwenda pale tabata shule kwenye ofisi zao wakadai kwamba zoezi kwa dar es salaam limesitishwa ilikuwa mwaka jana.mpaka Sasa sielewi niende wapi utaratibu wake ukoje
 
Nafikiri kwa Ilala wamehamia Somewhere GongolaMboto, Nenda pale watakupa taratibu za kufanya na utapata tu, mimi mwaka jana huohuo kuna kijana wangu alipata bila matatizo yoyote yale
 
Mimi Sina hata kitambulisho nitakipataje wadau nimewahi kwenda pale tabata shule kwenye ofisi zao wakadai kwamba zoezi kwa dar es salaam limesitishwa ilikuwa mwaka jana.mpaka Sasa sielewi niende wapi utaratibu wake ukoje
Walishindwa kukupa maelezo mazuri, hili zoezi ni endelevu na kila wilaya wana ofisi zao za kudumu ulizia ukifika utapata huduma
 
Huku Arusha tunamaliza mwaka sasa hakuna jipya na tulishajiandikisha na kupigwa picha ila Bado havijatoka
 
Mimi Sina hata kitambulisho nitakipataje wadau nimewahi kwenda pale tabata shule kwenye ofisi zao wakadai kwamba zoezi kwa dar es salaam limesitishwa ilikuwa mwaka jana.mpaka Sasa sielewi niende wapi utaratibu wake ukoje
Nenda kwenye ofisi zao za wikaya ya Ilala Gongo la Mboto utashughulikiwa
 
Heshima kwenu wakuu!
Nimepoteza kitambulisho cha taifa,na nimesharipoti polisi,ofisi ya NIDA hapa mkoani,na nimeshaenda benki kulipia 20k kwa ajili ya kupata kitambulisho kipya.
Swali Je ninawezaje kukipata kwa haraka,niende makao makuu ya NIDA? Kama ndio makao makuu yao yapo wapi kwa Dar?
Asanteni.
Huko huko mkoani nenda kwenye ofisi ya wilaya ya Nida utapata maelezo
 
Hawa jamaa walinikera nikaamua kabisa kutofuatilia huo upuuzi wao .

Bora nina Cha mpiga kura na leseni. Tosha kwa sasa..

Hawa jamaa ni hopeles
Hopeless kabisa napatwa nahasira nikikumbuka usumbufu wao walivokuwa wanaandikisha nikapanga lifolen lirefu jua Kali af kumbe ndo mambo Kama haya
 
hivi kitambulisho cha taifa kwa watoto kinatakiwa kuanzia kutolewa kwa watoto wa miaka mingapi
 
Back
Top Bottom