ZENJIBARIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 669
- 1,602
Mkuu huu uzi nilijibizana sana na watu jaribu kuzipitia comments zangu nadhani jibu la hiki swali utakikuta sehemu,ni vuzuri ukazisoma ili ukipata jibu uwe ushapata na mengine na jibu liweze ku-make sense,jibu la mkato peke yake litakuchanganya tu.Mimi naomba nikuulize swali dogo sana nimalize ubishi. Kama Dunia ni Flat na wewe sasa hivi umesimama Ubungo na unataka kuelekea upande wa South tu kwa ndege yako, Je? Mwisho wa safari hiyo utaishia wapi? Utaenda milele na milele huko Kusini?
Theory ya dunia duara inasema wazi, ukienda upande mmoja tu wa dunia bila kupinda basi mwisho utajikuwa upo palepale ulipoanzia maana unakuwa unazunguka kwenye duara.
Nipe jibu mkuu labda na mimi naweza kukuelewa
Lakini kwa kujazia nyama hili swali,niseme hili kuwa sisi waswahili tuna neno ulimwengu,kwa sasa ulimwengu linamaanisha universe labda,ila hatujui ni neno lipi lilokuja mwanzo kama ni universe au ulimwengu.
Kinadharia ulimwengu kwa sisi waswahili ni dunia ambayo haina mwisho, au kwa kiingereza ulimwengu ingemaanisha realm kwa usahihi,na realm ni Physical environment Ambayo haina mwisho kwa mtazamo wa aliemo ndani ya realm