Kitakwimu UKAWA muungano wenu ume prove failure kwenye uchaguzi huu

IT IS TRUE WHEN YOU DISMISS A ''A Free and Fair Election'' Factor.........
 
Ukitaka kumtawala mtu kadri upendavyo mfanye maskini, mnyime pesa atakutumikia maisha yake yote, atakulamba miguu mda wote. Mikoa yenye umaskini wa kutupa uliosababishwa na ccm hawatakaa wabadilike kamwe na wataendelea kuwa maskini tu. Kama watu walikuwa wanamkataa lowasa basi hata madiwani tu wanashindwa, wabunge wa upinzani wanashindwa. Poor Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Pwani,Singida mtaendelea kulaumu oo mikoa ya kaskazini inapendelewa tuu.[/QUOTYOUR TRULY RIGHT
 
Hivi unaamini kuwa CCM hushinda pasipo faulo?

Ni ujinga na upumbavu kuamini ccm imeshinda kihalali kwa kiwango hicho. Chaguz za ndani ya chama tu ni shughuli, achilia mbali rushwa iliyokithiri,ongezea na ujinga wa watanzania na umasikini uliotukuka.
 
kwa hali hii wote mnaoshabikia ccm baada ya miaka mitano nategemea mtakuja kuongelea mprovement kwenye kila secta kama afya(kuongezeka kwa hospital bora zinazotoa huduma bora na wafanyakazi wengi),elimu(kuinuka kwa kiwango cha elimu,ajira kwa waalimu wanaotosheleza,mitaala na miundombinu bora za shule),maji safi na salama,transport na communication bila kusahau rushwa na ufisadi.mkifanikiwa hayo kwa miaka mi5 basi mtastahili kubaki madarakani...otherwise mtakuwa mmeprove failure kuliko any political party in africa...u have all resources u need...yetu macho

Ni ajabu kuamini kwamba Lowasa anaweza kukabiliana na changamoto hizo huku ukikataa CCM haiwezi kukabiliana nazo,hapa ndipo shaka inapoanza kuingiwa na watz waliowengi,
Lowasa ni CCM 100%,ujana na utuuzima wake wote ni CCM,aliamini sera na itikadi za CCM mpaka hatua ya mwisho.
Ila alipokatwa tu Lowasa yuleyule akawa kitu kingine.
Hem tizama Kingunge na Sumaye eti na wao mnawatumia kueleza ubaya wa CCM.
Kimkakati hili ni kosa wana UKAWA,
hili ndilo lililowagharimu kwani watz sio wajinga kiasi hicho.
 
Mimi naamini kwa Singida watajifunza kutoka Singida Mashariki na watabadilika katika chaguzi ijayo baada ya kuona matunda ya wenzao yatakavyokuwa

Watabadilika endapo waliochaguliwa wataleta maendeleo. La sivyo, mwaka 2020 wananchi hao hao watairudisha ccm kama ilivyotokea kwa majimbo ya Kasulu na Uvinza mkoani Kigoma
 
Mbowe, Mbatia na Seif walifanya maamuzi kibiashara na si kisiasa.

Nnawapongeza kwa hilo.

Wachagga na Wapemba ikija kwenye masuala ya pesa ni baba mmoja mama mmoja.
 
Level ya ujinga ni kubwa sana ktk taifa letu na haya ndiyo Matokeo yake.
Tunashindwa kujipanga na kupanga serikal yenye kuleta tija,shida siyo vyama wananchi ndo hatujitambui mfano umepitisha diwan had mbunge wa ccm jumbo zima unataraji nn ?
 
UKAWA wamefanikiwa sanaaa mwaka huu,waulize CUF wakwambie.muulize na shein anajua.
 
Ninaamini kwa mwenye kufikiri sawasawa lazima atakubali kwamba katika Africa hakuna kama CCM kwasababu.

Kimsingi lengo la kuungana kwa vyama vya upinzani ilikua ni kutozitawanya kura ili muweze kushinda kirahisi.

Pamoja na kuungana kwenu lakini ushindi unaojitokeza haulingani kabisa na idadi ya vyama vyenu vilivyoungana.
Vijana wakileo husema"msuli tembo matokeo sisimizi"

Pamoja na kuungana kwenu lakini bado kuna majimbo mmeshindwa kabisa kuambulia hata diwani mmoja.

Na ukizama hata majimbo mengine mmeshinda kwa ushindi mwembamba sana mfano Temeke.

Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.

Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.
Hata wangeungana vyama kumi hakuna impact kwa kuwa ni briefcase parties hazina wanachama; ccm inavuna kutoka kwa wanachama. Hivi vyama vianze na mkakati wa kujipatia wanachama hadi vijijini hawa watakupigia kura bila kujali njaa zao au agenda ya mgombea tofauti ya kutaka kuwashawishi. Leo hii ukifanya sensa ya wanachama wa UKAWA sidhani hata milioni mbili wanafika; wala sijawahi kuwasikia wakijivunia mtaji huo. Kule kanda ya ziwa wameyumbishwa na mambo ya ukabila na ukanda lakini wasingekuwa mashabiki wa mtaani ni wanachama wasingeyumba
 
Ni takwimu zipi unazungumzia Gimmy's? Mpaka leo asubuhi idadi ya wabunge wa upinzani wa kuchaguliwa imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 70% ikilinganishwa na uchaguzi wa 2010 (soma gazeti la Mwananchi) na bado matokeo zaidi! Kwa majiji muhimu ya DSM, ARUSHA, MBEYA, MOSHI na manispaa za Bukoba, Tanga na Iringa n.k. upinzani emepeta. Ushindi huu wa upinzani haujapata kufikiwa katika historia ya siasa za vyama vingi Tanzania.

CCM wametumia raslimali na pesa nyingi mno kuliko wakati wowote katika historia yetu! Vyombo vya habari kama Star TV vimekiuka maadili yote ya utangazaji kukibeba chama tawala bila kuchukuliwa hatua. Kwa ujumla upinzani hadi sasa umefanya vizuri sana kwa vigezo vyote kulingana na mazingira dhaifu ya kikatiba, sheria na miundo mbinu na raslimali.
 
Lowassa kawaponza ,bora wangeingia vitani na manati yao,kuliko kuingia na SMG ya kuazima isiyo na risasi za kutosha
Haikuwa na risasi kabisa. Kama zilikuwemo basi zilikuwa blank. Mbowe kapata hela lakini kaua upinzani. Watamkumbuka Dr. Mihogo!
 
Watz tunamatatizo makubwa kichwani kuliko matatizo tunayoyaona kwa macho,ni ujinga na ni upumbavu uliochanganyika na ulofa ndo unaoweza ukakufanya kumchagua mtu yule yule kutoka chama kile kile chenye ilani ile ile na inatumika katiba ile ile kwa muda wote halafu unasubiria mabadiliko. Bora ya wale wa kanda ya Ziwa wenye sababu zilizo wazi zisizo na mashiko .................( kwenye maofisi mengi na huduma za kijamii baadhi ya jamii yanaangalia sana hizi sababu utasikia huyu wa kule kule) ambapo kwao wao hoja ya maendeleo,mambo ya kimataifa na mengineyo si kipaumbele chao.

Watanzania siyo wajinga. Wajinga ni nyinyi wanasiasa mnapowachanganya na hayo magia yenu ya angani. Miaka karibu 10 mnamshambulia mtu kuwa ni fisadi mkubwa halafu from nowhere huyo huyo mnamteua kuwa mgombea wenu na mnategemea watu wawaamini tu? Hata kuelezea sera zake hakuna eti mapenzi mahaba. Msingejichangaya hivi wapiga kura wangewaelewa tu. Mbowe kapiga hela lakini kawaulia chama!
 
Ninaamini kwa mwenye kufikiri sawasawa lazima atakubali kwamba katika Africa hakuna kama CCM kwasababu.

Kimsingi lengo la kuungana kwa vyama vya upinzani ilikua ni kutozitawanya kura ili muweze kushinda kirahisi.

Pamoja na kuungana kwenu lakini ushindi unaojitokeza haulingani kabisa na idadi ya vyama vyenu vilivyoungana.
Vijana wakileo husema"msuli tembo matokeo sisimizi"

Pamoja na kuungana kwenu lakini bado kuna majimbo mmeshindwa kabisa kuambulia hata diwani mmoja.

Na ukizama hata majimbo mengine mmeshinda kwa ushindi mwembamba sana mfano Temeke.

Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.

Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.

Nenda kasome mwenyekiti wa Nec anateuliwa na nani? katiba inasemaje kuhusu matokeo ya uraisi kuhojiwa tatizo ni ujinga,umaskini na maradhi
 
Ninaamini kwa mwenye kufikiri sawasawa lazima atakubali kwamba katika Africa hakuna kama CCM kwasababu.

Kimsingi lengo la kuungana kwa vyama vya upinzani ilikua ni kutozitawanya kura ili muweze kushinda kirahisi.

Pamoja na kuungana kwenu lakini ushindi unaojitokeza haulingani kabisa na idadi ya vyama vyenu vilivyoungana.
Vijana wakileo husema"msuli tembo matokeo sisimizi"

Pamoja na kuungana kwenu lakini bado kuna majimbo mmeshindwa kabisa kuambulia hata diwani mmoja.

Na ukizama hata majimbo mengine mmeshinda kwa ushindi mwembamba sana mfano Temeke.

Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.

Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.
....the opposite is the truth....kwamba ukawa ni mafanikio makubwa kwenye uchaguzi huu....angalia ongezeko la wabunge na ukaribu wa mbio ya urais...Yaelekea we uko dunia nyingine ambako huoni wala husikii....ama umeamua tu kuwa ignorant kama ilivyo kawaida yenu kukubali uhalisia...
....ukawa ni mafanikio makubwa ..na ndio maana unaona ccm mmeshindwa kuiba urais wa Maalim Seif zenj na kupelekea uchaguzi kufutwa....

....ukawa ni mafanikio na ndio way forward ya kuitoa ccm madarakani....
...waangalie vyama vidogo vidogo nje ya ukawa uone wamepata kura ngapi ndio ujue nguvu ya ukawa....

.... ukitaka kuona umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu...angalia matokeo ya jimbo la segerea yaliyoumiza wengi hadi sasa....pale ambapo ukawa waliacha kumsimamisha mtu mmoja (mtatiro)wakaweka wawili na kupoteza jimbo kwa ccm....

...kama umeshindwa kuona nguvu ya kuungana kwa vyama kwenye uchaguzi huu basi wewe ni kilaza wa vilaza usiejua kufanya simple analysis....mko wengi wa hivyo huko ccm...
 
hakuna hata anayeongelea lowassa kura zake za vyuo vikuu peke yake ni zaid ya mil 1 ambazo zingemuwezesha kushinda urais....... TZ tunaitaj maombi yanayoendana na kufunga kwa mwez mzima kujielewa!!!

Hilo umenena mkuu. Unafikiri kuwatosa wanachuo kutokupiga kura ilikuwa bahati mbaya? Huo nao ulikuwa mkakati wa kudhoofisha kura za upinzani. Wanaelewa wazi kuwa umri huo ni wa mabadiliko na kweli ukawa hapo wamekosa kura milioni na zaidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom