Kitakwimu UKAWA muungano wenu ume prove failure kwenye uchaguzi huu

Nenda kasome mwenyekiti wa Nec anateuliwa na nani? katiba inasemaje kuhusu matokeo ya uraisi kuhojiwa tatizo ni ujinga,umaskini na maradhi

Hapo unataka kusema umeibiwa,
Sasa mbona Arusha mmeshinda kwa kishindo?
 
Kwa mashabiki wa siasa, Ukawa wamefeli, lakini kwa wanaojua siasa za nchi hii, upinzani kwa ujumla wake umeimarika zaidi ya mara mbili kuliko ilivyokuwa 2010. Term iliyopita, Chadema walikuwa na wabunge 23 wa kuchaguliwa na CUF walikuwa na 2, NCCR 4 jumla 29 (Bara). Hadi baada ya majimbo 201 kati ya 264 kutangazwa matokeo yake, Chadema walikuwa na wabunge 35, CUF 8, NCCR 1 jumla majimbo 44. Imechukua Halashauri karibu 19, na hapo kuna uwezekano mkubwa wa kupata wabunge wa viti maalum zaidi ya 50 maana kura za urais ni zaidi ya 41 percent
 
....the opposite is the truth....kwamba ukawa ni mafanikio makubwa kwenye uchaguzi huu....angalia ongezeko la wabunge na ukaribu wa mbio ya urais...Yaelekea we uko dunia nyingine ambako huoni wala husikii....ama umeamua tu kuwa ignorant kama ilivyo kawaida yenu kukubali uhalisia...
....ukawa ni mafanikio makubwa ..na ndio maana unaona ccm mmeshindwa kuiba urais wa Maalim Seif zenj na kupelekea uchaguzi kufutwa....

....ukawa ni mafanikio na ndio way forward ya kuitoa ccm madarakani....
...waangalie vyama vidogo vidogo nje ya ukawa uone wamepata kura ngapi ndio ujue nguvu ya ukawa....

.... ukitaka kuona umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu...angalia matokeo ya jimbo la segerea yaliyoumiza wengi hadi sasa....pale ambapo ukawa waliacha kumsimamisha mtu mmoja (mtatiro)wakaweka wawili na kupoteza jimbo kwa ccm....

...kama umeshindwa kuona nguvu ya kuungana kwa vyama kwenye uchaguzi huu basi wewe ni kilaza wa vilaza usiejua kufanya simple analysis....mko wengi wa hivyo huko ccm...

Nikweli kabisa wapo wengi sana wa aina yake huko ccm na hili linasababishwa haswa na kukosa elimu. Ndio maana Lowassa akaanza na kipaumbele cha elimu.Ukinikumbusha kumkosa Julius Mtatiro kwa kweli naumia roho sana kwani pamoja na kuuandikia uongozi wa ukawa kuhusu kutatua mgogoro uliokuwepo jimboni huko na hatari ya kulikosa jimbo kwa kugawa kura viongozi waliendelea kujichimbia tu maofisini.Haya yametoke majimbo mengi na Mwanza (Nyamagana) ikiwemo.Unafahamu nao viongozi wa vyama hivi ngazi za majimbo hawana mishahara hivyo anapokuja mwanachama alie ndani ya ukawa na uwezo wa fedha hata kama hana haki ya kugombea pale kiongozi atachukua hela na kumwambia aingie kwenye kinyanganyiro na atamlinda tu. Hapa ndipo walipotakiwa viongozi wa ki taifa kuingilia kati na kunyoosha mambo. Udhaifu huu umetugharimu sana kama upinzani.
 
Ninaamini kwa mwenye kufikiri sawasawa lazima atakubali kwamba katika Africa hakuna kama CCM kwasababu.

Kimsingi lengo la kuungana kwa vyama vya upinzani ilikua ni kutozitawanya kura ili muweze kushinda kirahisi.

Pamoja na kuungana kwenu lakini ushindi unaojitokeza haulingani kabisa na idadi ya vyama vyenu vilivyoungana.
Vijana wakileo husema"msuli tembo matokeo sisimizi"

Pamoja na kuungana kwenu lakini bado kuna majimbo mmeshindwa kabisa kuambulia hata diwani mmoja.

Na ukizama hata majimbo mengine mmeshinda kwa ushindi mwembamba sana mfano Temeke.

Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.

Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.

Kama wewe ni analyst kwa nini hukuwashauri kabla?
 
Comfort Zone!!!
 
Kama wewe ni analyst kwa nini hukuwashauri kabla?

Kama walimpuuza Slaa,"lowasa ni asset au liability?".
Lakini pia walimpuuza lipumba ambaye tulimsikia akisema,"Dhamira yangu inanisuta".
Badala yakuwasikia walidhihakiwa tena hata kuwa tusi matusi ya nguoni.
Kama hawa walipuuzwa sidhani kama kuna ambaye angesikilizwa.
 
Nikweli kabisa wapo wengi sana wa aina yake huko ccm na hili linasababishwa haswa na kukosa elimu. Ndio maana Lowassa akaanza na kipaumbele cha elimu.Ukinikumbusha kumkosa Julius Mtatiro kwa kweli naumia roho sana kwani pamoja na kuuandikia uongozi wa ukawa kuhusu kutatua mgogoro uliokuwepo jimboni huko na hatari ya kulikosa jimbo kwa kugawa kura viongozi waliendelea kujichimbia tu maofisini.Haya yametoke majimbo mengi na Mwanza (Nyamagana) ikiwemo.Unafahamu nao viongozi wa vyama hivi ngazi za majimbo hawana mishahara hivyo anapokuja mwanachama alie ndani ya ukawa na uwezo wa fedha hata kama hana haki ya kugombea pale kiongozi atachukua hela na kumwambia aingie kwenye kinyanganyiro na atamlinda tu. Hapa ndipo walipotakiwa viongozi wa ki taifa kuingilia kati na kunyoosha mambo. Udhaifu huu umetugharimu sana kama upinzani.
....mi nadhani kote ukawa walipokosa ushindi wa wabunge kulikuwa na shida hii ya kuachiana majimbo....na matokeo yake wamepoteza majimbo kwa ccm....

....sasa ni wakati wa ukawa kuimarika na kuchukua funzo hili lenye maumivu makali na kulifanyia kazi....kama watataka kuitoa madarakani ccm kwa uhakika....na hii ndio njia pekee iliyotumika kote vyama tawala vilikoondolewa (mfano kanu kenya)...

....ni wakati pia wa ukawa kuimarika na kujua ubinafsi hauna tija kwenye siasa za mageuzi....
...
 
We acha mimi nimeyashuhudia singida ,hasa iramba nnishida,
kwa hali hii
wote mnaoshabikia ccm baada ya miaka mitano nategemea mtakuja kuongelea mprovement kwenye kila secta kama afya(kuongezeka kwa hospital bora zinazotoa huduma bora na wafanyakazi wengi),elimu(kuinuka kwa kiwango cha elimu,ajira kwa waalimu wanaotosheleza,mitaala na miundombinu bora za shule),maji safi na salama,transport na communication bila kusahau rushwa na ufisadi.mkifanikiwa hayo kwa miaka mi5 basi mtastahili kubaki madarakani...otherwise mtakuwa mmeprove failure kuliko any political party in africa...u have all resources u need...yetu macho
 
....mi nadhani kote ukawa walipokosa ushindi wa wabunge kulikuwa na shida hii ya kuachiana majimbo....na matokeo yake wamepoteza majimbo kwa ccm....

....sasa ni wakati wa ukawa kuimarika na kuchukua funzo hili lenye maumivu makali na kulifanyia kazi....kama watataka kuitoa madarakani ccm kwa uhakika....na hii ndio njia pekee iliyotumika kote vyama tawala vilikoondolewa (mfano kanu kenya)...

....ni wakati pia wa ukawa kuimarika na kujua ubinafsi hauna tija kwenye siasa za mageuzi....
...

Vp kuhusu uraisivunafikiri mmeanguka kwasababu Mgwira na kina Dovutwa hawajaungana na UKAWA?
Upinzania bado unasafar ndefu sana tz
 
Furaha yangu kubwa ni kuona UKAWA wataendesha halmashauri kadhaa za majiji na mikoa mikubwa kitu ambacho hakikuwepo. Kwa mfano mtwara mjini, Singida mashariki, Newala, Iringa na Tanga ukiachia Dar na Mbeya. Nilishuhudia kuongezeka kwa mapato ktk jiji la arusha na hakukuwa na michango ya maabara. Katika kipindi cha miaka 5 natarajia katika maeneo haya kutakuwa na mabadiliko makubwa kielimu na huduma mbalimbali ikiwemo afya na ardhi. Kwangu mimi haya ni mafanikio ya UKAWA. Waimarishe ushirikiano huu wasijagawe na wajipange kujiimarisha zaidi kimkakati kwa ajili ya 2020
Ni kweli Mkuu, nami kama ningekuwa na uwezo wa kuwashauri UKAWA, ningewashari wakubali matokeo. Huwezi kuoa siku hiyo hiyo na kutarajia kupata mtoto siku hiyo hiyo na kumwandikisha shule siku hiyo hiyo. Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha, pamoja na ongezeko la Wabunge na Halmashauri zitakazokuwa chini ya UKAWA; EL amewasaidia kuongeza idadi ya % ya kura za Urais huenda hata wabunge wa viti maalum wataongezeka, hiki sio kitendo cha kubezwa, ndege aliyeko mkononi ni bora zaidi aliyeko juu ya mti. Kitendo cha UKAWA kuungana katika uchaguzi huu kimewapatia nguvu na wamefanya vizuri sana ikilinganishwa na chaguzi zilizopita. Hata hivyo, imeshuhudiwa muungano huu kutoheshimiwa miongoni mwao wenyewe kiasi cha kusimamisha wagombea wawili kutoka vyama shirika kitu ambacho kimewachanganya baadhi ya wapiga kura kutoamini kama kweli ni muungano wenye tija, na wengine kuchanganya kura na kusababisha wagombea kushindwa; Katika hali kama hii, UKAWA wanapaswa kuchukua changamoto zilizojitokeza na kuanza kuzifanyia kazi kuanzia leo ikiwa ni pamoja na kuimarisha Muungano wao kwa malengo maalum. Kitendo cha kugomea matokeo hakitakuwa na tija kwa sababu Rais akishatangazwa ataanza kutumia ngivu zake za Urais nao kuendelea kulalamika bila kuhudumia wapiga kaura wao kama ilivyotokea mwaka 2010 walivyogoma kutomtambua Mhe. JK, lakini mbona JK amekuwa Rai hadi leo.

Aidha, wahakikishe Chama kama CDM kinakua na taswira ya Kitaifa ili Watanzania wote wajione kama sehemu ya Chama ingawa kiuhalisia inaweza isiwe hivyo. Hebu fikiria kuhusu CCM Meneja Kampeni Alhaji Bulembo - kutoka Mara; Katibu wa Itikadi na Uenezi - Mtwara; Katibu Mkuu wa Chama - Arusha; Mwenyekiti wa Chama - Pwani, Makamu Mwenyekiti - Iringa. Katika hali kama hii watu wengi wanajiona kama sehemu ya chama kwa mfano wakiwa na mkutano wa Kampeni Musoma, Wanamusoma wakimwona Bulembo wanajiona kama sehemu ya Chama hata kama kiuhalisi sio hivyo. Sasa Angalia kwa CDM - Mwenyekiti - Arusha; Meneja wa Kampeni - Arusha, Mkurugenzi wa Fedha - A, Komu; huko huko !!! Hata kama ni kwa nia nzuri hiyo inajenga taswira gani kwa jamii ya Tanzania ambayo asilimia kubwa inahitaji elimu, elimu, elimu sio ya darasani tu hata ya kuchanganua mambo. Wakiambia kuhusu CDM kuwa ni ya ukabila na ukanda, wakipewa mfano kama huo, wanabadilsishwa kwa urahisi na kuwanyima UKAWA kura kuanzia hata Diwani na Mbunge ambao kimsingi ni wazaliwa wa eneo hilo hilo.
 
Ninaamini kwa mwenye kufikiri sawasawa lazima atakubali kwamba katika Africa hakuna kama CCM kwasababu.

Kimsingi lengo la kuungana kwa vyama vya upinzani ilikua ni kutozitawanya kura ili muweze kushinda kirahisi.

Pamoja na kuungana kwenu lakini ushindi unaojitokeza haulingani kabisa na idadi ya vyama vyenu vilivyoungana.
Vijana wakileo husema"msuli tembo matokeo sisimizi"

Pamoja na kuungana kwenu lakini bado kuna majimbo mmeshindwa kabisa kuambulia hata diwani mmoja.

Na ukizama hata majimbo mengine mmeshinda kwa ushindi mwembamba sana mfano Temeke.

Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.

Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.

Unasema "kitakwimu" halafu huweki hata takwimu moja 2010 vs 2015. weka hizi takwimu.
 
Mtalalama sana ila ukweli ni kwamba huyu fisadi kawagharimu.Kama jinsi mbowe alivyo change gia angani basi kuna baadhi ya wana UKIWA wanaojitambua nao walichange gia angani wakahamia kwa magufuli,

Mwaka 2010 Lowasa hakuwepo upinzani mbona hiyo mikoa ya Dodoma, Ruvuma haikutoa mbunge hata mmoja wa Upinzani?
 
Tathimi yangu kuu kuhusu uchaguzi 2015
1. UKAWA wamesaidia kuongeza idadi ya wabunge name madiwani
2. Kura za rais zitaongezeka
3. Wammetoa changamoto/ ushindani unao stahili kwa wapinzani wao
4. Wametoa Sera nzuri ambazo hata Ccm watazifanyia kazi
5. Muungano huo umesababisha ccm kutoa ahadi nyingi ambazo wataazimika kuzitekeleza hivyo wananchi kupata maendeleo bora zaidi. Wakilala imekula kwao 2020.
 
Back
Top Bottom