Kitakwimu UKAWA muungano wenu ume prove failure kwenye uchaguzi huu

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,271
Ninaamini kwa mwenye kufikiri sawasawa lazima atakubali kwamba katika Africa hakuna kama CCM kwasababu.

Kimsingi lengo la kuungana kwa vyama vya upinzani ilikua ni kutozitawanya kura ili muweze kushinda kirahisi.

Pamoja na kuungana kwenu lakini ushindi unaojitokeza haulingani kabisa na idadi ya vyama vyenu vilivyoungana.
Vijana wakileo husema"msuli tembo matokeo sisimizi"

Pamoja na kuungana kwenu lakini bado kuna majimbo mmeshindwa kabisa kuambulia hata diwani mmoja.

Na ukizama hata majimbo mengine mmeshinda kwa ushindi mwembamba sana mfano Temeke.

Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.

Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.
 
Ukitaka kumtawala mtu kadri upendavyo mfanye maskini, mnyime pesa atakutumikia maisha yake yote, atakulamba miguu mda wote. Mikoa yenye umaskini wa kutupa uliosababishwa na ccm hawatakaa wabadilike kamwe na wataendelea kuwa maskini tu. Kama watu walikuwa wanamkataa lowasa basi hata madiwani tu wanashindwa, wabunge wa upinzani wanashindwa. Poor Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Pwani,Singida mtaendelea kulaumu oo mikoa ya kaskazini inapendelewa tuu.
 
Gia ya angani ilibadilisha fikra za wengi, including me. Huwezi kuaminisha watu kwa miaka nane kuwa fulani ni mwizi wa kuchomwa moto, then miezi miwili kufikia uchaguzi unamchukua huyo mtu apeperushe bendera yako. Lazima wanaojitambua wataona unacheza na fikra zao na watakupiga chini.

Katika kuongea kwangu na watu, wengi hilo limewakatisha tamaa na hata kura walizigawa sana. Hilo ni kosa la Mbowe, kafanya mambo kwa interest zake binafsi bila kufikiria impact kwa wapiga kura wanaojielewa...
 
Ninaamini kwa mwenye kufikiri sawasawa lazima atakubali kwamba katika Africa hakuna kama CCM kwasababu;
Kimsingi lengo la kuungana kwa vyama vya upinzani ilikua ni kutozitawanya kura ili muweze kushinda kirahisi.
Pamoja na kuungana kwenu lakini ushindi unaojitokeza haulingani kabisa na idadi ya vyama vyenu vilivyoungana.
Vijana wakileo husema"msuli tembo matokeo sisimizi"
Pamoja na kuungana kwenu lakini bado kuna majimbo mmeshindwa kabisa kuambulia hata diwani mmoja.
Na ukizama hata majimbo mengine mmeshinda kwa ushindi mwembamba sana mfano Temeke.
Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.
Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.
Furaha yangu kubwa ni kuona UKAWA wataendesha halmashauri kadhaa za majiji na mikoa mikubwa kitu ambacho hakikuwepo. Kwa mfano mtwara mjini, Singida mashariki, Newala, Iringa na Tanga ukiachia Dar na Mbeya. Nilishuhudia kuongezeka kwa mapato ktk jiji la arusha na hakukuwa na michango ya maabara. Katika kipindi cha miaka 5 natarajia katika maeneo haya kutakuwa na mabadiliko makubwa kielimu na huduma mbalimbali ikiwemo afya na ardhi. Kwangu mimi haya ni mafanikio ya UKAWA. Waimarishe ushirikiano huu wasijagawe na wajipange kujiimarisha zaidi kimkakati kwa ajili ya 2020
 
Gia ya angani ilibadilisha fikra za wengi, including me. Huwezi kuaminisha watu kwa miaka nane kuwa fulani ni mwizi wa kuchomwa moto, then miezi miwili kufikia uchaguzi unamchukua huyo mtu apeperushe bendera yako. Lazima wanaojitambua wataona unacheza na fikra zao na watakupiga chini.

Katika kuongea kwangu na watu, wengi hilo limewakatisha tamaa na hata kura walizigawa sana. Hilo ni kosa la Mbowe, kafanya mambo kwa interest zake binafsi bila kufikiria impact kwa wapiga kura wanaojielewa...

True, move ya Mbowe kumchukua Lowassa imesaidia sana CCM kushinda. Wana-Ukawa wengi kwa nje walikuwa washabiki lakini walipoingia kwenye kale ka box roho zao ziliwasuta na wakaamua mawili kumpigia Magufuli au kuharibu kura ya urais. Kitu ambacho hadi sasa viongozi wa UKAWA hawajaelewa.
 
Hivi unaamini kuwa CCM hushinda pasipo faulo?

Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.
Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.
 
Ukitaka kumtawala mtu kadri upendavyo mfanye maskini, mnyime pesa atakutumikia maisha yake yote, atakulamba miguu mda wote. Mikoa yenye umaskini wa kutupa uliosababishwa na ccm hawatakaa wabadilike kamwe na wataendelea kuwa maskini tu. Kama watu walikuwa wanamkataa lowasa basi hata madiwani tu wanashindwa, wabunge wa upinzani wanashindwa. Poor Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Pwani,Singida mtaendelea kulaumu oo mikoa ya kaskazini inapendelewa tuu.
Mimi naamini kwa Singida watajifunza kutoka Singida Mashariki na watabadilika katika chaguzi ijayo baada ya kuona matunda ya wenzao yatakavyokuwa
 
Wewe ni mpumbavu na statistics sijui ulisoma chuo gani.
Chukua idadi ya majimbo ambayo chadema,NCCR,NA CUF ilipata 2010 kwa tanzania bara ambapo hawakuwa ktk muungano wa ukawa linganisha na ambayo wamisha pata mpaka sasa kutokana na muungano kama hamna tofauti ndio njo na uzi kama huu.
Kumbuka huu ni muungano wao kwa mara ya kwanza,na mabadiliko huwa ni kidogo kidogo sasa sijui wewe ulitaka wapate majimbo 200 kwa wakati moja.ukitaka hvyo waombe wawe kwenye muungano zaidi ya chaguzi 2 zijazo uone kama CCM yako haitafutika kwenye uso wa dunia.
 
Gia ya angani ilibadilisha fikra za wengi, including me. Huwezi kuaminisha watu kwa miaka nane kuwa fulani ni mwizi wa kuchomwa moto, then miezi miwili kufikia uchaguzi unamchukua huyo mtu apeperushe bendera yako. Lazima wanaojitambua wataona unacheza na fikra zao na watakupiga chini.

Katika kuongea kwangu na watu, wengi hilo limewakatisha tamaa na hata kura walizigawa sana. Hilo ni kosa la Mbowe, kafanya mambo kwa interest zake binafsi bila kufikiria impact kwa wapiga kura wanaojielewa...

Hayo ndio mawazo ya wengi tunaojitambua. Wasiojitambua bado wataendelea kuonea huruma ukawa ambao kimsingi hauna dira
 
Furaha yangu kubwa ni kuona UKAWA wataendesha halmashauri kadhaa za majiji na mikoa mikubwa kitu ambacho hakikuwepo. Kwa mfano mtwara mjini, Singida mashariki, Newala, Iringa na Tanga ukiachia Dar na Mbeya. Nilishuhudia kuongezeka kwa mapato ktk jiji la arusha na hakukuwa na michango ya maabara. Katika kipindi cha miaka 5 natarajia katika maeneo haya kutakuwa na mabadiliko makubwa kielimu na huduma mbalimbali ikiwemo afya na ardhi. Kwangu mimi haya ni mafanikio ya UKAWA. Waimarishe ushirikiano huu wasijagawe na wajipange kujiimarisha zaidi kimkakati kwa ajili ya 2020

Yeah faraja kiasi lakini sio lengo, lengo lilikuwa ni LOWASSA...
 
Ukitaka kumtawala mtu kadri upendavyo mfanye maskini, mnyime pesa atakutumikia maisha yake yote, atakulamba miguu mda wote. Mikoa yenye umaskini wa kutupa uliosababishwa na ccm hawatakaa wabadilike kamwe na wataendelea kuwa maskini tu. Kama watu walikuwa wanamkataa lowasa basi hata madiwani tu wanashindwa, wabunge wa upinzani wanashindwa. Poor Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Pwani,Singida mtaendelea kulaumu oo mikoa ya kaskazini inapendelewa tuu.

Mtalalama sana ila ukweli ni kwamba huyu fisadi kawagharimu.Kama jinsi mbowe alivyo change gia angani basi kuna baadhi ya wana UKIWA wanaojitambua nao walichange gia angani wakahamia kwa magufuli,
 
Bila faulo CCM wasingefurukuta uchaguzi huu, umiliki wa dola umewasaidia sana, hilo lazima tukubali hata kama tuna mapenzi na CCM........
 
Ninaamini kwa mwenye kufikiri sawasawa lazima atakubali kwamba katika Africa hakuna kama CCM kwasababu.

Kimsingi lengo la kuungana kwa vyama vya upinzani ilikua ni kutozitawanya kura ili muweze kushinda kirahisi.

Pamoja na kuungana kwenu lakini ushindi unaojitokeza haulingani kabisa na idadi ya vyama vyenu vilivyoungana.
Vijana wakileo husema"msuli tembo matokeo sisimizi"

Pamoja na kuungana kwenu lakini bado kuna majimbo mmeshindwa kabisa kuambulia hata diwani mmoja.

Na ukizama hata majimbo mengine mmeshinda kwa ushindi mwembamba sana mfano Temeke.

Ukitizama dira kwa jinsi matokeo yanavyoendelea kutoka utagundua bado CCM itashinda kwa zaidi ya 60% ushindi ambao hautopishana sana na ushindi ambao CCM ilijipatia 2010.

Kuna kila sababu yakusema kwamba Muungano wenu ume prove failure.
Huu Muungano utapimwa kwa uwiano wa asilimia za Urais, Ubunge na Udiwani.
We unaangalia kiti cha Urais tu, mbona husemi Udiwani na Ubunge? Unadhani kati ya viti walivyopoteza wapinzani na walivyovipata vipi vitakua vingi??
 
Lowassa kawaponza ,bora wangeingia vitani na manati yao,kuliko kuingia na SMG ya kuazima isiyo na risasi za kutosha
 
unapomkataa lowassa afu unamchagua chenge na mama tibaijuka akili yako ina walakini
 
Tatizo la watanzania siyo kushinda kwa CCM au ukawa, ni kupata viongozi watakaowaletea maendeleo.
Ushabiki wa CCM vs UKAWA siyo muhimu sana, bali cha msingi ni aina gani ya waliochaguliwa.
Hatutaki tena wawakilishi wanaoshiriki au kutetea wizi wa fedha za uma (mfano EPA, ESCROW etc).
Awe UKAWA au CCM kama anashriki au kutetea wizi wa mali au fedha za uma, basi huyo hafai na ni adui wa wananchi na kama ameshinda basi vita dhidi yake iendelee!
 
Huu Muungano utapimwa kwa uwiano wa asilimia za Urais, Ubunge na Udiwani.
We unaangalia kiti cha Urais tu, mbona husemi Udiwani na Ubunge? Unadhani kati ya viti walivyopoteza wapinzani na walivyovipata vipi vitakua vingi??

Ukumbuke vyama vimepambana na chama kimoja lakini ukitizama utofauti wa matokeo licha ya kua bado hayajakamilika hatutarajii utofauti mkubwa kwakulinganisha na matokeo ya 2010.UKAWA mtakataa tu kwani ni tabia yenu kujifanya wajuaji wa kila kitu ila ukweli ni kwamba Lowasa zaidi yakuchafua upinzani hana impact yoyote chanya.
Hii ahueni nyembamba tunayoina chanzo ni mkusanyiko wa kura(vyama) na si Lowasa.
Na ukweli ni kwamba kama huyu fisadi asingekaribishwa UKAWA tungeshuhudia kuimarika kwa UPINZANI zaidi.
 
unapomkataa lowassa afu unamchagua chenge na mama tibaijuka akili yako ina walakini

Kwasasa hamna tena uhalali wakupambana na Ufisadi,mnamponda Chenge huki mnamtamani ahamie UKAWA.
Halafu tizama nafasi ya Chenge CCM na nafasi ya Lowasa CDM hueleweki mkuu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom