The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,433
- 17,070
Changamoto kubwa itakayomkabili Samia Suluhu ni Uzanzibari wake.
Makundi mengi ndani ya CCM hayapendezwi Tanzania kuongozwa na wazanzibari wote, yaani Rais wa Muungano ni Mzanzibari na Rais wa Zanzibar Mzanzibari, hapo ndio kuna mzizi wa fitina.
Juzi nilikuwa na watu fulani wenye inside information, wanasema mama anajaza wazanzibari kwenye Serikali ya Muungano kinyume cha utaratibu, kwa mfano, wanasema Magufuli alikosea kumteua Mbarawa kuwa waziri kwenye wizara isiyo ya Muungano, mama amerudia kosa lile lile kwa maksudi kabisa huku akijua ni kosa, yaani ana justify kosa kwa kosa la mwenzake, kwamba kama mtu aliiba na hakukamatwa kwanini na wewe usiibe?
Sio hilo tu, kwamba kwenye teuzi nyingi za maded, nk amewaingiza wazanzibari kibao kinyume cha Katiba.
Zamani wazanzibari ndio walikuwa wanalalamika kuonewa kwenye Muungano, sasa watanganyika ndio wanaolalamika.
Viongozi wengi wa CCM kinachowauma ni Mzanzibari kufanya maamuzi ya mikopo kwa niaba ya watanganyika, hilo ndio linawauma ndio maana unaona Bwana Job amejitokeza kusema tunakopa mikopo mikubwa isiyo eleweka, hoja iko hapo, Uzanzibari.
Kilichopo sasa ni kuhakikisha mama hagombei 2025 bali agombee mtanganyika, haiwezekani Zanzibar na Tanganyika ziongozwe miaka zaidi ya 10 na wanzanzibar watupu. Hata mimi kwenye hili nawaunga mkono.
CCM sasa ndio wanaanza kuona kwamba Muungano umekaa kimagumashi, watu wameambiwa miaka na miaka hawasikii, sasa ndio wanaanza kuliona hilo wakati ni too late.
Tusubiri tuone.