Hapo naona picha ya mwanamke wa kiafrika aliyependeza na vazi la kitenge lenye picha ya jembe.
Mwanamama huyu amebeba mkoba na kuna mahali anapoelekea ila sio shamba!
Kwa miaka hiyo ya azimio la arusha mama huyu anaonekana kuwa kwenye maisha ya unafuu kwa mavazi yake. Sio masikini kabisa.
Kipindi hicho chenye kauli mbiu za kilimo ni uti wa mgongo na nyingine, watu wa kipato cha kati na cha juu hawakuwa tayari kujishughulisha na kilimo cha jembe la mkono moja kwa moja.
Hivyo watu hawa walipenda kujionyesha kuwa pamoja na viongozi na kampeni za kukuza kilimo kwa kushiriki mambo mbalimbali yenye kutoa picha kwamba nao wako pamoja katika kuboresha kilimo.
Ila ukweli ni kuwa hawakuwa tayari kujishughulisha na kilimo moja kwa moja.
Walikuwa tayari kushiriki mikutano inayohusiana na kilimo, kuvaa nguo zenye kauli mbiu ya kuhamasisha kilimo ila sio zaidi ya hapo.
Walipenda kulivaa jembe ila hawakuwa tayari kulishika.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.