KITABU; Kurasa Za Maisha Ya Mafanikio, Nidhamu Uadilifu Na Kujituma

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,915
3,407
Kuna mambo matatu muhimu sana kila mmoja wetu anatakiwa kujua kuhusu maisha, ili kuweza kuwa na maisha bora na yenye mafanikio. Na hapa mafanikio ni vile wewe unavyoyaona maisha yako kwa ubora, vile wewe unavyotamani maisha yako yawe na vile ambavyo ndoto zako kubwa kwenye maisha zilivyo.
Jambo la kwanza muhimu sana unalotakiwa kujua ni kwamba mafanikio kwenye maisha hayatokei mara moja tu, kwa ghafla. Bali mafanikio ni mchakato, ni mkusanyiko wa mambo madogo madogo yanayofanyika kwa muda mrefu. Mwishowe yanajikusanya na kuwa mafanikio makubwa. mafanikio kwenye maisha siyo sawa nakushinda bahati na sibu, kwamba umelala masikini na kuamka tajiri, ni mchakato wa muda mrefu. Kwa kujua hili itakuwezesha kuendelea kuweka juhudi hata kama huoni mafanikio mara moja.
Jambo la pili muhimu sana kujua ni kwamba kile ambacho unafikiri muda mrefu kwenye akili yako, ndiyo kinachotokea kwenye maisha yako. kwa lugha nyingine ni kwamba maisha uliyonayo sasa, ni zao la mawazo ambayo umekuwa unafikiri. Na unachofikiri sasa, ndiyo kitazalisha maisha yako ya kesho. Kwa kifupi ni kwamba tunakuwa kile tunachofikiri, mawazo yetu yanavuta vitu tulivyonavyo kwenye maisha yetu. Kama mawazo yako ni chanya muda wote utavutia vitu ambavyo ni chanya, na utafanikiwa. Kama mawazo yako ni hasi, utavutia vitu ambavyo ni hasi na kila mara utaona ni vigumu sana kufanikiwa.
Jambo la tatu muhimu sana kujua ni kwamba unaweza kuishi siku moja tu kwa wakati. Kuna leo, jana na kesho. Katika siku hizi tatu, unaweza kuishi leo tu, unaweza kuifanya leo kuwa bora sana au kuiharibu kabisa. Jana imeshapita, hivyo hata kama ulifanya vizuri sana au ulifanya vibaya, huwezi kuibadili jana. Kesho bado haijafika, hivyo kuifikiri sana bado hakutakusaidia. Leo ndiyo siku ambayo ipo kwenye mikono yako. Leo ndiyo siku ambayo unaweza kufanya mabadiliko yoyote unayotaka kwenye maisha yako. Na leo ndiyo siku ambayo unaweza kuianza safari ya mafanikio.
Unawezaje kuyatumia mambo haya matatu kuwa na maisha bora na ya mafanikio?
Hapa ndio mahali muhimu sana kama kweli unataka kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa. unahitaji kuweka mambo haya matatu pamoja, na kuyafanyia kazi kila siku. Hii ina maana kuwa tayari kuweka juhudi kila siku, hata kama huoni matokeo mara moja, kuwa na mawazo chanya kila siku na kila mara, na kuchagua kuishi siku ya leo.
Kwa sababu jamii yetu imejaa kelele na upotoshaji mwingi sana, ni vigumu sana kuweza kufanya vitu hivyo vitatu. Wakati unakazana kuweka juhudi kwenye kazi au biashara yako, kuna watu wanakuhubiria kwamba kuna njia ya mkato, wengine wanacheza kamari. Kila unapoamka kuna habari hasi nyingi sana zinasambaa, kuna ulalamishi mwingi unaendelea na wengi wamekata tamaa. Na watu wengi wanajilaumu sana kwa jana zao, na kuwa na hofu kubwa ya kesho zao, hivyo kushindwa kuishi vyema kwenye siku husika.
Unawezaje kuepuka yote hayo yanayokuzuia?
Hapa ndiyo sehemu muhimu sana, kwa sababu unakwenda kupata dawa ya kutimu maeneo hayo matatu na hivyo kuweza kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa.
Katika hali hii unahitaji kitabu; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Hiki ni kitabu kitakachokuwezesha kuishi siku yako vizuri, kukufanya uwe na mawazo chanya kwenye akili yako, na kukupa moyo uendelee kuweka juhudi hata kama bado huoni matokeo uliyokuwa unatarajia.


Kitabu hiki cha KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, kimeandaliwa kwa dhana kwamba kila siku mpya ya maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu. Na wewe ndiye mwandishi ambaye unaamua maisha yako yaweje siku hiyo. Kitabu hiki kina kurasa 366, sawa na siku 366 za mwaka huu 2016.
Kwa kuwa na kitabu hiki, kila siku unasoma ukurasa mmoja, na hapo utaweza kuianza siku yako vyema kwa kuwa na fikra sahihi zitakazokuwezesha kuboresha maisha yako.
Kitabu hiki ni mkusanyiko wa makala za KURASA ZA MAISHA ambazo zimekuwa zinaandikwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hapa unazipata makala zote tangu kipengele cha kurasa kianze, na badala ya kusoma makala moja moja kwenye KISIMA, hapa unazisoma kwa pamoja.
Kitabu hiki ndio mwongozo wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2016. Kurasa hizo zimeandaliwa kusoma kurasa moja kwa siku, kusema tamko la siku na kwenda kufanyia kazi.
Kitabu hiki kitakupa mbini za kutumia vizuri muda wako, kuwa na matumizi mazuri ya fedha zako, kuweza kupambana na changamoto za kila siku za maisha, na pia kuimarisha mahusiano yako na wale wanaokuzunguka.
Hakikisha hukosi kitabu hiki, na kipate mapema sana leo, ili mwaka wako 2016 uweze kwenda vizuri.


MOJA YA KURASA ZA KITABU HIKI.

Jinsi ya kukipata kitabu; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO.
Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa kielektroniki yaani softcopy (pdf). Kwa mfumo huu, kitabu hiki unaweza kukisomea kwenye simu yako ya mkononi, kwenye tablet au kwenye kompyuta. Kwa njia hii ni rahisi sana kuwa na kitabu hiki popote pale ulipo, hata kama umesafiri, ukitaka kukisoma ni kufungua tu kwenye simu yako. na hii ni muhimu kwa sababu hiki ni kitabu cha kusoma kila siku kwa mwaka mzima.
Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email, hivyo popote pale ulipo duniani, unaweza kutumiwa kitabu hiki. Huhitaji kwenda popote kukifuata, kinakufuata hapo ulipo wewe.
Kupata kitabu hiki tuma ujumbe kwenda namba 0717396253.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, kumbuka hakuna wa kukuzuia bali wewe mwenyewe. Usikubali kujizuia.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
0717 396 253
 
Hongera mkuu kwa maarifa uliyotupa. Kitabu kinapatikana kwa bei gani? au ni free? maana hujaweka bei
 
Back
Top Bottom