Kitabu Kipya: Historia na Kumbukumbu za Rais Mkapa kutoka Nov 12, 2019

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
774
1,456
Taarifa rasmi inasema kua Kitabu Kipya cha Historia na Kumbukumbu za Rais Mkapa kutoka Nov 12, 2019. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolea na Uongozi Institute, Katika kitabu hicho, pamoja na mambo mengine, Rais Mkapa atazungumzia historia yake toka utoto na Nyakati za Urais wake wa awamu ya 3

1572286476463.png

1572286716315.png
 
Kwa Kweli kitakuwa Kitabu kizuri kweli kweli

Kikiuzwa kwa bei ya Kizalendo itabidi nikipate

Mzee mkapa alikuwa Rais kweli kweli

Hotuba za Mkapa zinafaa kabisa kufundishia Siasa au course za Habari

Serikali yake ilisifika kwa utawala bora na uwazi. Watu walipanda vyeo based on merits, seniority and experience. Sheria, taratibu na protocals ziliheshimiwa sana
 
Serikali yake ilisifika kwa utawala bora na uwazi. Watu walipanda vyeo based on merits, seniority and experience. Sheria, taratibu na protocals ziliheshimiwa sana

Mzee Mkapa alikuwa Rais wa Viwango vya nchi zilizoendelea
 
Kwa Kweli kitakuwa Kitabu kizuri kweli kweli

Kikiuzwa kwa bei ya Kizalendo itabidi nikipate

Mzee mkapa alikuwa Rais kweli kweli

Hotuba za Mkapa zinafaa kabisa kufundishia Siasa au course za Habari
Kwa lugha hiyo iliyotumika hakiwezi kuitwa cha kizalendo bali cha kibeberu. Asilimia ngapi ya wananchi wa kawaida watasoma kwa lugha hiyo? Ndogo sana
 
Rais ambaye aliuza viwanda vyote alivyojenga Mwalimu na yeye mwenyewe kuneemeka na kuuzwa kwa NBC, kufilisika kwa ATC pamoja na Tanesco etc. Alipwaya sana katika uongozi wake ashukuru yupo TZ nchi nyingine asingepewa hata pension.
 
Taarifa rasmi inasema kua Kitabu Kipya cha Historia na Kumbukumbu za Rais Mkapa kutoka Nov 12, 2019. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolea na Uongozi Institute, Katika kitabu hicho, pamoja na mambo mengine, Rais Mkapa atazungumzia historia yake toka utoto na Nyakati za Urais wake wa awamu ya 3

View attachment 1247419

View attachment 1247428
HABARI NJEMA.

JIWE SO FAR HAJAANDIKA.

ILA ANSBERT NGURUMO KAMWANDIKIA
 
Mzee Mkapa alikuwa Rais wa Viwango vya nchi zilizoendelea

Mbona hakutufikisha kwenye nchi zenye viwango vya maendeleo kama unavyo msifia....ni kawaida lakini kusiafia kwa mtu ambaye tayari kisha ng'atuka kwenye uongozi au akifa ndo zetu wabongo
 
Ni hatua nzuri wazee kuanza kuandika vitabu kuhusu mapito na maisha yao.

Kitabu hicho kwa umahiri wake Benjamin Mkapa ktk lugha ya Kiingereza kitaleta shauku ulimwengu mzim kujua juu ya uongozi wa ki-CCM na hatima ya CCM kisiasa.
 
Back
Top Bottom