Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,913
- 30,255
- Thread starter
- #61
Gavana,Tafuta kitabu cha Padri Sivallon kinaitwa Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania bara , utajua kanisa ni nini
Hivyo vitabu viwili hapo chini vilitaabisha sana Kanisa kwa kuwa yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu yalidhihirisha mipango ambayo haikutakiwa ifahamike.
Ilipokuja kufahamika athari yake ikawa hakuna tena la kufanya siri zote ziko nje.
Hatua ambayo ilichukuliwa ni kwa kitabu cha Sivalon kisichapwe tena na cha Bergen kisiingizwe tena Tanzania.
Mna nini cha kutisha ndani ya vitabu hivi?
Prof. Njozi katika kitabu chake, ''Mwembechai Killings...'' (2002) alisherehesha vizuri vitabu hivi.
Yawezekana hii ndiyo sababu ya kitabu chake kupigwa marufuku.
Nasoma matusi na kejeli najisemea hawa ni watu kama mimi lakini wao wako upande ambao unanufaika hawawezi kuwa na fikra kama zangu muhimu kwangu ni kutuliza akili na kujaribu kufahamisha kuwa haya niandikayo si uchochezi ni tatizo la kweli ambalo iko siku litatuangamiza sisi sote kwani mficha maradhi kifo kitamfichua.