Kitabu kimoja ambacho kila Mtanzania anapaswa kukisoma na jinsi ya kukipata hapa bure

Makirita Amani

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Messages
1,216
Likes
493
Points
180
Makirita Amani

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2012
1,216 493 180
Ni jambo lililo wazi ya kwamba moja ya vitu vinavyopelekea sisi watanzania kushindwa kupiga hatua katika maisha yetu ni kukosa maarifa ua uongozi bora. Kwa sasa tuna tatizo kubwa sana la kiuongozi hapa Tanzania. Tatizo hili linaanzia juu kabisa kwenye uongozi wa nchi na linashuka mpaka chini kabisa kwenye uongozi wa familia.

Kama ilivyo mambo yoyote kwenye maisha, uongozi una misingi yake, uongozi una miiko yake na pia uongozi unahitaji hekima na busara za hali ya juu. Tunaona watu wengi wenye nafasi za uongozi wakifanya maamuzi ambayo yanakuja kuleta madhara makubwa kwa wananchi na hata kwao binafsi. Tunaona watu wakiacha kabisa misingi ya uongozi na kufanya mambo ambayo yanawafurahisha watu kwa wakati mfupi. Wanashindwa kujua kwamba kwa wakati mrefu watu hao watakuja kuumia zaidi.

Kumekuwepo na dhana mbili kuhusu viongozi;

Wapo wanaosema kwamba viongozi wanazaliwa na wapo wanaosema kwamba viongozi wanatengenezwa.

Wanaosema viongozi wanazaliwa wanaamini kwamba kuna watu wamezaliwa ili wawe viongozi. Watu hawa tayari wanakuwa na sifa za uongozi ndani yao na wakipata nafasi ya kuongoza wanafanya vizuri.

Wanaosema kwamba viongozi wanatengeneza wanaamini kwamba mtu anafundishwa kuwa kiongozi mzuri. Kwamba mtu yeyote akiwa tayari kujifunza misingi ya uongozi anaweza kuwa kiongozi bora.

Ukweli ni kwamba viongozi wote wanatengenezwa, wapo wanaojitengeneza wenyewe kupitia kujifunza misingi ya uongozi, na wapo wanaotengenezwa na jamii walizokulia na hawa ndiyo wanaonekana kama wamezaliwa viongozi.

Changamoto kubwa ya kutengeneza viongozi ni kwamba kama jamii haina misingi mizuri ya uongozi, basi viongozi watakaotengenezwa hawawezi kuwa wazuri. Na hapa ndipo matatizo makubwa ya kijamii yanapozaliwa.

CHANZO KIKUU NA SULUHISHO LA MATATIZO YA UONGOZI YANAYOENDELEA HAPA TANZANIA.

Kila siku kuna habari mpya na malalamiko ya watu walioaminiwa na kupewa nafasi ya uongozi kutumia vibaya madaraka yao. Hali hii imekuwa inapelekea watu kuumia na kupata madhara makubwa.

Tatizo hili lipo kuanzia uongozi wa juu kabisa wa nchi mpaka uongozi wa chini kabisa wa mtaa. Na pia linaenda mpaka kwenye uongozi wa familia, uongozi wa kazi na hata uongozi wa biashara.

Chanzo kikuu cha matatizo haya ya uongozi ni watu kukosa maarifa sahihi ya kiuongozi. Watu wanajikuta na madaraka makubwa ambayo hawajui wayatumieje, mwishowe wanayatumia kimakosa na wanaleta madhara makubwa kwao na kwa wengine kwa ujumla.

Watu wengi wamekuwa hawana utamaduni wa kujisomea maarifa ya uongozi na hata historia za mambo yaliyowahi kutokea huko nyuma. Namna ambavyo watu walitumia vizuri madaraka yao na kufanikiwa na namna ambavyo wengine waliyatumia vibaya na wakashindwa kabisa.

Hivyo tatizo kuu kabisa ni watu kukosa maarifa sahihi, na kwa kuwa wengi hawana utamaduni wa kujisomea, basi wanaishia kufanya mambo kwa mazoea au kwa kuangalia wengine wanafanya nini.

Suluhisho la tatizo hili ni watu waanze kutafuta maarifa sahihi ya uongozi. Kwa sababu kila mmoja wetu ana nafasi fulani ya uongozi, basi ni vyema tukajijengea utaratibu wa kujifunza na kujisomea kuhusu uongozi. Lazima tujenge utaratibu wa kujifunza kutokana na historia za watu waliopita.

KITABU KIMOJA CHA UONGOZI AMBACHO NASHAURI KILA MTU AKISOME.

Katika utaratibu wangu wa kujisomea vitabu, nimekutana na kitabu kimoja ambacho nimekuwa nakisoma na kukisikiliza mara kwa mara. Kitabu hichi nilikutana nacho kwa mara ya kwanza mwaka 2013 na nimekuwa nakisoma kila mara. Kwenye gari nina AUDIO BOOK ya kitabu hiki, na mara nyingi ninapokuwa kwenye foleni huwa nasikiliza kitabu hiki. Kupitia kitabu hiki nimekuwa naona wazi makosa makubwa ambayo viongozi na hata watu wa kawaida wanayafanya na yanaharibu kabisa sifa zao.

Kitabu hiki kinaitwa THE 48 LAWS OF POWER, ambacho kimeandikwa na mwandishi ROBERT GREEN. Mwandishi amechimba sana historia ya tangu enzi na enzi na kuonesha namba ambavyo watu wamekuwa wanayatumia madaraka kwa mafanikio na wanaoyatumia vibaya na kushindwa.

Mwandishi amekuna na sheria 48 za madaraka ambapo kwa kila sheria ametoa mifano ya watu waliotii sheria hiyo na kufanikiwa na mifano ya watu waliokiuka sheria hizo na kuumia. Na sheria ya kwanza kabisa kwenye kitabu hiki inaitwa NEVER OUTSHINE THE MASTER, yaani usitake kuonekana wewe upo juu kuliko mkubwa wako, hata kama unajua kuliko mkubwa wako, kuonesha hilo wazi ni lazima atakuondoa. Na ametoa mifano ya waliotii sheria hii na kufanikiwa na walioikiuka na wakaishia kuondolewa kwenye madaraka madogo waliyokuwa nayo.

Hiki ni kitabu ambacho nashauri kila mtu akisome, kwa namna ninavyokielewa kitabu hiki kinaweza kukusaidia kwa pande mbili.

Upande wa kwanza kinakupa mbinu za kiuongozi ambazo unaweza kuzitumia popote, kuanzia kwenye familia, kazi, biashara, mahusiano. Hapa unapata njia sahihi za kufuata ili kuweza kutimiza kile unachotaka.

Upande wa pili kinakuzuia wewe kutumika kwa faida ya wengine. Baadhi ya sheria kwenye kitabu hiki zinaonesha namna gani viongozi wanaweza kuwatumia watu wengine kwa manufaa yao. Kwa mfano unaweza kufanya kazi wewe lakini sifa akazibeba mtu mwingine. Kupitia kitabu hichi utajifunza namna ya kulinda sifa yako na kuhakikisha hutimiki na wengine.

Ushauri wangu ni kila mtu akisome kitabu hiki, maana ni mgodi wa dhahabu linapokuja swala la uongozi.

Raisi mteule wa Marekani Bwana Donald Trump, kwa sehemu kubwa alitumia sheria za kitabu hiki na ndiyo maana aliweza kushinda kinyume na mategemeo ya wengi.

ANGALIZO; KITABU HIKI KINAWEZA KUWA HATARI.

Sheria za kitabu hiki, kama zitatumika vibaya zinaweza kuzalisha viongozi hatari kabisa. zinaweza kuzalisha viongozi ambao ni madikteta, wanaowatumia watu kupata chochote wanachotaka wao.

Hivyo ni imani yangu kwamba utakuwa na hekima na busara ya kukuwezesha kukichambua kitabu hiki na kuchukua yale mazuri yanayoweza kuleta faida kwa nchi yetu.

Mwisho kabisa kama yupo mtu anayeweza kumfikishia Raisi ujumbe huu, basi amshauri sana asome kitabu hiki. Kina mambo mazuri yatakayomwezesha kuongoza vizuri.

Unaweza kupata kitabu hiki kwa kukinunua kwenye maduka makubwa ya vitabu, au kupakua hapa bure nakala tete (softcopy) ya kitabu, kwa link nitakayoweka. Kama utapenda AUDIO BOOK ili uweze kuisikiliza popote ulipo tunaweza kuwasiliana na ukapata. Audio book ni kubwa, zaidi ya masaa 10 ya kusikiliza, hivyo unaweza kuwa unasikiliza kila siku unapokuwa kwenye gari.

Link ya kupakua nakala tete bure fungua; Dropbox - Robert Greene - The 48 laws of power.pdf

KUHUSU AUDIO BOOKS (VITABU VYA SAUTI).

Vipo vitabu ambavyo vipo kwenye mfumo wa sauti, hii ni njia rahisi kwako kuweza kupata maarifa ukiwa sehemu ambayo unapoteza muda lakini huwezi kusoma kitabu cha kawaida. Mfano kama upo kwenye foleni unaweza kusikiliza vitabu vilivyosomwa.

Kuna vitabu zaidi ya 100 ambavyo vipo kwenye mfumo wa sauti na moja ya vitabu hivyo ni hichi cha THE 48 LAWS OF POWER. Vitabu hivi vimewekwa kwenye memory card 3 za ukubwa wa 4GB. Memorycard hizi unaweza kuweka kwenye simu ya kawaida, simu ya kisasa, tablet, kompyuta na hata redio ya gari.

Vitabu hivi vya sauti vimegawanyika katika makundi yafuatayo; UONGOZI, BIASHARA, MAUZO NA MASOKO, USHAWISHI, na HAMASA YA MAFANIKIO. Vipo vitabu kama THINK AND GROW RICH, RICH DAD POOR DAD, CASHFLOW QUADRANTS, SALES BIBLE, LESSONS FROM THE RICHEST MAN, THE RICHEST MAN IN BABYLON, AUTOMATIC MILLIONAIRE, NEVER GIVE UP na vingine vingi.

Huu ni mfumo ambao umeniwezesha mimi kuweza kusoma zaidi ya vitabu vitatu kwa wiki, kwa sababu kila ninapokuwa kwenye gari, basi kuna kitabu nasikiliza.

Kupata AUDIO BOOK ya kitabu hiki na vingine fungua link hii; AUDIO BOOKS « AMKA MTANZANIA

Nikutakie usomaji mwema wa kitabu hiki cha THE 48 LAWS OF POWER, pata maarifa na ongeza hekima na busara yako katika kuyatumia kwa usahihi.

Usikose kupata AUDIO BOOKS hizo ili uweze kujiongeza maarifa kwenye biashara, uongozi na hata kupata hamasa ya mafanikio.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com

nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,531
Likes
11,238
Points
280
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,531 11,238 280
48 laws of power ninacho tokea kitambo,huwa nasoma mstari kwa mstari,neno kwa neno...sipendagi ujingaujinga mimi.
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,760
Likes
25,216
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,760 25,216 280
Hakika umesema vema
 
demigod

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Messages
5,121
Likes
9,911
Points
280
demigod

demigod

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2015
5,121 9,911 280

Biggs

Senior Member
Joined
May 3, 2014
Messages
180
Likes
97
Points
45
B

Biggs

Senior Member
Joined May 3, 2014
180 97 45
48 laws of power ninacho tokea kitambo,huwa nasoma mstari kwa mstari,neno kwa neno...sipendagi ujingaujinga mimi.[/QUOT
48 laws of power ninacho tokea kitambo,huwa nasoma mstari kwa mstari,neno kwa neno...sipendagi ujingaujinga mimi.
Kwa wanaopenda kukisoma nakiweka hapa.
 
Attachments:

Jaslaws

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Messages
5,856
Likes
3,451
Points
280
Jaslaws

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined May 31, 2011
5,856 3,451 280
Robert green ni mwandishi mzuri sana wa vitabu kunakitabu kingine nasikia ni kizuri sijabahatika kukuona wala kukisoma kama unacho naomba nikutumie email yangu unitumie!!
 
Nyanidume

Nyanidume

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
2,337
Likes
552
Points
280
Nyanidume

Nyanidume

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
2,337 552 280
Vilivyotafsiriwa kwa kiswahili vipo?
 
Upepo wa Pesa

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Messages
12,173
Likes
15,021
Points
280
Upepo wa Pesa

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2015
12,173 15,021 280
Shida ni kwamba watz wengi kusoma ni kama msamiati flan hivi!!

Na huyo unayesema ashauriwe asome nadhan itakua hatari sana kama akikisoma
 
Makirita Amani

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Messages
1,216
Likes
493
Points
180
Makirita Amani

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2012
1,216 493 180
Robert green ni mwandishi mzuri sana wa vitabu kunakitabu kingine nasikia ni kizuri sijabahatika kukuona wala kukisoma kama unacho naomba nikutumie email yangu unitumie!!
Vitabu vyake vingine ni hivi;
1. The Art of Seduction
2. The 50th Law
3. The 33 Strategies of War
4. Mastery
 
Patrickn

Patrickn

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
8,354
Likes
5,170
Points
280
Patrickn

Patrickn

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
8,354 5,170 280
Mkuu asante kwa link..nimedownload tayari..naomba utupe na hivyo vingine kama hutojali
 
Z

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Messages
1,045
Likes
1,089
Points
280
Z

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2015
1,045 1,089 280
Unadhani Watanzania hawajui hizo principles za good governance? Wanazijua. But too many wa-Tz ni wanafiki, wabinafsi na hawana hofu ya Mungu. Very few care about the next person. Wengi mno hawana utu. Ndio maana unaona greda inapelekwa kuvunja nyumba alfajiri bila kuwatangazia watu angalau waondoe fenicha na mali nyingine. Siku moja si ingetosha? Kama ni kweli walikaidi kuhama wakipewa saa 24 si wangeondoa vitu vyao? Hawapewi. Ndio kukosa utu huko. Inatia uchungu sana. Hivi, huyo anayesema bomoa kwa staili hiyo amewahi kujiuliza ingekuwa ni yeye anabomolewa ingekuwaje?
 
Ngushi

Ngushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
8,403
Likes
16,651
Points
280
Ngushi

Ngushi

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
8,403 16,651 280
Ahsante 48 laws of power nilikua nakitafuta kweli
 
Forum statistics

Threads 1,275,223
Members 490,932
Posts 30,536,086