Alisina
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 4,069
- 4,263
Safi sana,Mtanzania kusoma hata umshikie bunduki..
Mimi mwenyewe nilikuwa mvivu ila nimeanza kusoma hivi vitabu taratibu taratibu na sasa umekuwa ni utaratibu wangu..
Kila Jambo Jema linagharama yake.
Miezi miwili iliyopita nilikuwa namsoma kijana mmoja Walter Rodney,
Huku nikiwa na kumbukumbu ya M'jamaica Marcus Garvey "People without a knowledge of their past history,origin and culture is like a tree without roots"
Mwafrika huyu Walter kiufupi alikuwa Smart/Brilliant huku akipata first degree akiwa na miaka 21 kwa first class na PHD Miaka 24.
Alipata kufundisha University of Dar el salaam UDSM Mwaka 1969-74.
How Europe underdeveloped Afrca; Moja ya kitabu chake kizuri katika kuitambua vyema Africa na yaliyotokea katika Enzi za ukoloni.
Kimeelezea mambo mengi mfano growth without development & development by contradiction.
Pia hakusahau kuwachachafya apologists & Bourgeois writer wa Ukoloni barani africa huku akiwaita wapuuzi wakubwa sana kwa kufanya balance sheet credits & debits wakihitimisha good & bad mema yamezidi mabaya hivyo ukoloni ulileta neema kwa Africa, labda umeleta neema ya maize na viazi na Cash crops kama banana republic's....na kusambaza Elimu ya kitumwa na kuwagawa watu na unyonyaji wa kiwango cha Juu mno.
Pia Kelezea ulafi na uchu wa Portugal na Spain waliodai wao ni kizazi na wanapaswa kurithi Mali zote za dunia hivyo Papa Vatican apigie mstari ghafla England,Holland na France wakasema nyinyi mabwana habari gani za ajabu mwatuletea..? Hilo jambo haliwezekani hata kidogo.
Kitabu kinaelezea kwa uzuri sana Africa yetu.
Walter alizaliwa 1942 akafa mwaka 1980 kwa Gari kutegewa bomu.
"Reading books makes you a wonderful person, an Intellegent, a creative person and What not,When you read good books"
Ni jambo zuri sana kutafuna vitabu Kama viwavi Jeshi.