Kitabu gani ambacho kimewahi kubadilisha maisha yako na unatamani wengine tukisome?

asante sana kwa alieanzisha hii thread, imenisaidia, nimpepata kitabu kimoja cha the rich man from babylon, kikubwa nilichosoma ni kuweza 1/10 ya mapato yote unayopata, NATAFUTA KITBU CHOCHOTE CHA STRTEGIES OF WAR, THANK U
 
Vitabu vinauwezo wa kubadili kabisa maisha ya mtu yeyote yule. Baada ya vita vya pili ya dunia wajapan walikuja na nadharia iitwayo KAIZEN (Continuous improve), yaani angalau kila siku uongeze kitu kipya kichwani chenye kukuza uelewa wako na kuboresha maisha yako kwa njia yeyote ile.

Hapa tujadili nguvu ya vitabu katika maisha ya mtu yawezekana ulisoma wewe au umewahi kukisikia kwa watu tushirikishane.

Kuna wengi tumebadilishwa au kuboreshwa maishani mwetu kiafya, kijamii, kibiashara, kitaaruma, kimitazamo, kiimani, kimwili, mahusihano nk kupitia vitabu.

Kitabu gani ambacho kiligusa maisha yako au kukubadilisha na unatamani wanajf wenzako tujifunze pia, unaweza kueleza kimekusaidiaje kwa ufupi kama hutojali.

=========

Unaweza kujipakulia au kujisomea baadhi ya Vitabu kwenye hii thread=>Vitabu vilivyowahi kubadilisha maisha yako
BIBLIA TAKATIFU ndo kitabu pekee kilichoweza kuyabadili maisha yangu na bila Biblia cjui maisha yangu yangekuwa ya ajabu namna gani Ahsante MUNGU
 
"Dreams, memories and reflections " - Carl Gustav Jung
"Three theories of child development " nimesahau author.
 
The Big Picture: Ben Carson.
Hichi kitabu kilinifanya nikagundua kwa nini nipo hapa nilipo na nitatokaje hapa nilipo. Na nilikinunua when i was going through a difficult phase in my life. It was an eye opener.
una pdf ya hicho kitabu mkuu
 
Kuna vitabu vitatu ambavyo vimeshangia kubadili maisha yangu kwa kiwango kikubwa sana. Ningependekeza kila mtanzania avisome.
1. THINK AND GROW RICH
Hiki kimenisaidia kuweza kufikia uwezo mkubwa ulio ndani yangu na kuniwezesha kuona fursa nyingi zinazonizunguka.
2. RICH DAD, POOR DAD
Hiki kimenisaidia kuhusu utofauti kati ya elimu ya darasani na elimu halisi ya mtaani. Kimenisaidia kuona mambo ambayo nilifichwa darasani na ambayo ni ya msingi sana ili kufanikiwa.
3. THE RICHEST MAN IN BABYLON
Hiki kimenisaidia kuhusiana na maswala yote yanayohusuana na fedha kuanzia kuweka akiba mpaka kuwekeza. Kimeniwezesha kuweza kujilipa mimi mwenyewe hata kwa kipato kidogo sana na kuweza kujenga akiba iliyotosha kuanzia biashara.
Hivyo ni vitabu ambavyo natamani kila mtanzania avisome. Kama huna vitabu hivi nitumie email kwenye amakirita@gmail.com na nitakutumia vyote vitatu bure kabisa.
Au unaweza kutembelea AMKA MTANZANIA na ukajifunza mengi pamoja na uchambuzi wa vitabu hivi.
 
Back
Top Bottom