Kitabu gani ambacho kimewahi kubadilisha maisha yako na unatamani wengine tukisome?

Wasalaaam ndugu zangu, natumai wote ni wazima.

Leo hii naanzisha huu uzi kwa dhumuni zuri na maalumu la kusambaza maarifa kwa wanajukwaa hili na pengine watu wengine wa nje ya jukwaa hili.

Mpango ni kurusha vitabu mbalimbali kwenye jukwaa hili ambavyo vitaweza kuwasaidia watu na kuweza kuwapanua uwezo wa kiakili endapo utakuwa umesoma vitabu vizuri na bado unavyo itakuwa ni vema ukirushe kwenye uzi huu ili watu mbalimbali wasome na waelewe.

Natumai watu wa kada mbalimbali watapita na hakuna mtu ambaye atakosa cha kujifunza hapa. Sasa vitabu vinaweza kuja kwa mfumo wa PDF, MOBI, EPUB etc. Na kama utakuwa na hard copy basi watu wanaweza kukutafuta kama tu mtakuwa mekubaliana.

Natanguliza shukrani zangu.

Mimi naanza na kitabu kizuri sana ambacho kimenisadia kwenye kukuza uwezo wa kufikiri mambo kwenye biashara. Kinaitwa "The Go Giver" nashauri mtu akipata muda akisome.
Kama kimenisaidia basi natumai hata wewe kitakusaidia.

Kwa kifupi kinaelezea jinsi gani ambavyo mtu anaweza kufanya biashara kubwa lakini bado biashara hiyo itaipa jamii inayomzunguka faida.
Tofauti na mawazo ambayo wafanya biashara wengi na wajasiriamali wanakuwa nayo kwamba biashara ni faida tu na utafanya biashara sehemu yenye faida tu.

Kinaanza na mtu moja alikuwa ni kijana mdogo anafanya kazi kwenye kampuni fulani huko MAREKANI sasa akawa anahangaika sana kupata utajiri wa haraka. Kila siku alikuwa na mipango mikubwa ya biashara lakini hafanikiwi. Siku moja akapata nafasi kukaa na tajiri mkubwa huko MAREKANI na akaambiwa sifa ya kuwa Tajiri ni lazima ujifunze kutoa kwa watu kabla ya kutanguliza faida.

Mbeleni kinaonyesha jamaa analalamika kwamba ukifanya biashara kwa huruma huwezi kutajirika hata siku. Lakini akakutana na tajiri mwingine ambaye alimueleza vilevile. Na mwishowe akaja kujua kama matajiri wakubwa wote wanakuwa na sifa zinazofanana.

Young Malcom.

CC: UncleBen , FisadiKuu , MSEZA MKULU , Consigliere
Mkuu ni wazo zuri sana na ningeshauri huu uzi wako usingeunganishwa na huu... Anyways, ngoja nikisome hiki kitabu kwanza.. Kitu ninachojua na wengi nadhani hawajui ni kwamba matajiri wakubwa tu wanapenda sana kusoma hivi vitabu. Siku moja niliingia ofisini kwa tajiri mmaarufu tu nikakuta vitabu vya aina hii vingi tu mezani kwake..
 
Mkuu idea Nzuri. Mods wanatakiwa wawe waelewa wanaweza kuachana thread yako ijitegemee na kuweka links kwenye ya related threads ndani ya thread kama further JF references.
Hivi vitu useful vinatakiwa kuachwa viwe vingi mbona thread za siasa Sijui tundu lissu huwa hata kumi. Otherwise create title unique kidogo uwe kama unaadress issue mpya. Hicho kitabu nitakipitia
 
Mkuu ni wazo zuri sana na ningeshauri huu uzi wako usingeunganishwa na huu... Anyways, ngoja nikisome hiki kitabu kwanza.. Kitu ninachojua na wengi nadhani hawajui ni kwamba matajiri wakubwa tu wanapenda sana kusoma hivi vitabu. Siku moja niliingia ofisini kwa tajiri mmaarufu tu nikakuta vitabu vya aina hii vingi tu mezani kwake..
Uko Sawa kuna ceo wa private company hapa jijini wadau wangu walikuwa wanafanya kazi kwake aliwapa kila mmoja wakiwa kama young ambitious graduates folder lenye vitabu zaidi ya 200 na kuwahimiza wawe wanasoma hata muda aliwapa.

Mmiliki wa kampuni kubwa duniani ya uwekezaji Berkshire Hathaway Inc na miongoni mwa matajiri watatu wakubwa duniani Wallen buffet anauwezo wa kusoma hadi vitabu zaidi ya 100 kwa siku. Anasema I read everyday so that I may not make a silly investment decisions
 
BIBLIA ndiyo kitabu pekee kilichobadili maisha yangu ambacho natamani kila mtu akisome, kabla ya hapo nilikuwa na maisha ya mashaka mashaka sana;mfano mke wangu alikuwa kila mimba anayopata mtoto anazaliwa akiwa mfu, watu walianza kutucheka na kutusema vibaya, lakini kitabu hiki { BIBLIA } NILIPOANZA KUKISOMA kilinionyesha chanzo cha tatizo,namna ya kutatua pia ninajua upendo mkuu wa MUNGU kwangu hata akaamua kumtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele Yohana 3:16 tena YESU ANAITA ''AKISEMA NJOONI KWANGU NYINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KULEMEWA NA MIZIGO NAMI NITAWAPUMZISHA''MATHAYO 11:28
 
Biblia takatifu ya Mungu, Ina mafungu katika nyakati zooote za maisha hasa zile za kukatisha tamaa na kuvunja moyo ambazo binadamu yoyote hazifurahii..
I read it everyday,inanipa moyo kuendelea mbele
 
Bible ndio kila kitu , ndani kuna kila hitaji la mwanadamu, science, leadership, economics, struggles, comfort, happiness, it's mystery book
 
BIBLIA
Ina kila kitu, ina elimu yote, imekamilika. maandishi na maudhui yake hayachakai vizazi na vizazi. ki ukweli menibadikisha sana.
 
QUR AN

QUR-AN ni kitabu chenye sifa ambazo vitabu vingine vyote duniani havina.
ni ktabu kidogo chenye maandishi machache na chenye maana pana kuliko kitabu chochote ulimwenguni.
yeyote atakaye jifunza QUR-AN na akaifuata ataishi vizuri hapa duniani na kesho akhera
SIFA ZA QUR-AN
1. Ni kitabu peke ambacho hakibadilishwi wala hakibadilishiki
2. Ni kitabu pekee ambacho kinasomeka kwa lugha moja tu.
3. Ni kitabu pekee ambacho kinahifadhiwa kichwani na watu.
4. Ni kitabu kepee ambacho kimefafanua kwa ufasaha maisha yaliyopita na ya sasa na yajayo.
5. Ni kitabu pekee chenye sura inayomzungumzia maisha ya mwanamke anavyotakiwa kuishi.
Yapo mengi tosheka na hayo

1. Nimejifunza kupitia QUR-AN kwamba chimbuko la Sayansi ni QUR-AN.
QUR-AN imezungumzia uumbwaji wa dunia karne ya saba, katafute kwenye vitabu vyako vyote ma prophesa waligundua sayansi mwaka gani? utapata jibu.
2. Nime jifunza kupitia QUR-AN kwamba sisi wanaadamu ndio viongozi wa hii dunia, uwezo tuliokuanao wanaadabu majinni hawaufikii hata robo.
Tosheka na hayo ukitaka kujua zaidi kuhusu QUR-AN tafuta waalimu wakufundishe.
 
Why Men Don't Listen and Women Can't Read Maps - Allan & Barbara Pease.
 
god bless you kujisomea vitabu ndo njia pekee ya kubadili maisha yako na kuhisi bado una nafasi katika hii dunia thanks......
 
Vitabu vinauwezo wa kubadili kabisa maisha ya mtu yeyote yule. Baada ya vita vya pili ya dunia wajapan walikuja na nadharia iitwayo KAIZEN (Continuous improve), yaani angalau kila siku uongeze kitu kipya kichwani chenye kukuza uelewa wako na kuboresha maisha yako kwa njia yeyote ile.

Hapa tujadili nguvu ya vitabu katika maisha ya mtu yawezekana ulisoma wewe au umewahi kukisikia kwa watu tushirikishane.

Kuna wengi tumebadilishwa au kuboreshwa maishani mwetu kiafya, kijamii, kibiashara, kitaaruma, kimitazamo, kiimani, kimwili, mahusihano nk kupitia vitabu.

Kitabu gani ambacho kiligusa maisha yako au kukubadilisha na unatamani wanajf wenzako tujifunze pia, unaweza kueleza kimekusaidiaje kwa ufupi kama hutojali.

=========

Unaweza kujipakulia au kujisomea baadhi ya Vitabu kwenye hii thread=>Vitabu vilivyowahi kubadilisha maisha yako

UNAWEZA PIA SOMA "Purpose driven life" UNAWEZA DOWNLOAD KWENYE SEARCH ENGINE YOYOTE ILE, KITABU HIKI KIMEBADILISHA MTAZAMO NA MFUMO WA MAISHA YANGU.
 
Back
Top Bottom