Kitabu cha Yussuf Makamba kutumika mashuleni!!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
32,030
58,459
Wana JF,

..kwanza nimpongeze Mzee Makamba kwa kuandika kitabu kupinga RUSHWA akitumia mifano kutoka ktk KURAN TUKUFU na BIBLIA.

..sasa nimesoma kwamba serikali imeamua kwamba kitabu hicho kitumike mashuleni kuwafunda vijana wetu wachukie rushwa.

..wakati nakubaliana na wazo la kuwafundisha watoto wetu kuchukia rushwa, nina mashaka sana na busara za kutumia mifano ya KURAN na BIBLIA ktk mitaala ya wizara ya elimu.

..hivi kwa uamuzi huu ni nini kitatuzuia baadaye kuamua kufundisha Biolojia,Fizikia, au Kemia kwa kutumia Kurani na Biblia?

..vipi ikiwa mimi ni mzazi wa Kiislamu/Kikristo na sitaki mwanangu afundishwe kuhusu Biblia/Kurani?

..Sasa kutakuwa na maana gani kumuandikisha mtoto ktk shule ya public ikiwa ataenda kufundishwa DINI[Uislamu au Ukristo]?
 
kula tano JokaKuu, bongo hamna separation of church/ mosque/ state.

Halafu vile vile Makamba ni Secy wa CCM. Sasa watu wa CHADEMA wakisema inakuwa unfair kwao watasemaje? Ina maana wameshindwa kutafuta vitabu vya watu wasio high profile? Makamba amependelewa kwa sababu ya kazi yake ya Chama?

Inafurahisha kuona mtu anaandika kitabu kinachokemea rushwa wakati mazingira ya kitabu kutumika shuleni yanaweza kushukiwa kuwa ni ya ki-rushwa rushwa!
 
Pundit,Kitila,

..naelewa kwamba Ibrahim Kaduma naye ameandika kitabu kuhusu maadili ya Mtanzania kwa kutumia mifano ya BIBLIA. sasa huyu naye anaweza kudai kitabu chake kitumike mashuleni.

..Ungetegemea basi atokee Shekhe/Mchungaji/Padri kukemea suala hili.

..waliojisemea TANZANIA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU hawakukosea.
 
Sijasoma hicho kitabu..ila ningeshauri viongozi wa DINI husika wangesoma hicho kitabu wakatoa maoni yao kabla ya kukipeleka shuleni

Kama kitabu kitakuwa kimegusa kweli nafikiri si mbaya, tunachoangalia Lengo litafikiwa au La. Tunachohitaji watoto wachukie RUSHWA kutoka watoto.

Kama walivyozungumza wengine CCM wanatafuta UJIKO TU, maana uchukiaji wa Rushwa si wa maandishi, Tunahitaji vitendo
 
We havent seen even the cover of the book and we are starting criticising it! kazi kweli kweli....
 
Kuna vitu vingine huhitaji kuviona kujua kuwa vimekosewa au kuna dalili ya makosa.

Hata hivyo ni lazima tutambue kuwa katika Tanzania hatuna mstari wa utengano kati ya dini na siasa. Hatujawahi kuwa nao na tusichukulia ukuta wa utengano walio na Marekani sawa na Tanzania.

Kama somo la kitabu ni kuhusu Rushwa nadhani anayo haki ya kutumia mifano yoyote ile toka kwa Aristotle, Papa, na ma Imam kuelezea point yake.

Hata hivyo, kama kitabu chake ni cha masuala ya dini na rushwa ni sehemu mojawapo hapo sina budi kuuliza ana qualification gani ya kufundisha dini au masomo hayo.

Implication yangu ni kuwa ni kitabu cha kiada/ziada ambacho kinazungumzia masuala ya uwajibikaji wananchi hususan suala la rushwa, na ndani yake anatumia mapokeo na mafundisho ya vitabu viwili kujenga hoja zake au kuzitetea.

Naamini ana haki hiyo.

Swali la msingi ni kwanini ni kitabu chake na si cha wengine, hapa nauliza kuhusu ubora wake kuzidi vitabu vingine vyote vinavyohusiana na masuala ya rushwa. Je kitabu chake kimepewa upendeleo wa pekee?
 
Kabla ya kuamua kutukika mashuleni,. nadhani wataalam wa mitaala watakipitia na kutoa maoni yao. Si vizuri serikali kujiamulia mambo yahusuyo vitabu vya kutumika mashuleni bila kuhusisha wataalamo wa mitaala.
 
Wana JF,

..kwanza nimpongeze Mzee Makamba kwa kuandika kitabu kupinga RUSHWA akitumia mifano kutoka ktk KURAN TUKUFU na BIBLIA.

..sasa nimesoma kwamba serikali imeamua kwamba kitabu hicho kitumike mashuleni kuwafunda vijana wetu wachukie rushwa.

..wakati nakubaliana na wazo la kuwafundisha watoto wetu kuchukia rushwa, nina mashaka sana na busara za kutumia mifano ya KURAN na BIBLIA ktk mitaala ya wizara ya elimu.

..hivi kwa uamuzi huu ni nini kitatuzuia baadaye kuamua kufundisha Biolojia,Fizikia, au Kemia kwa kutumia Kurani na Biblia?

..vipi ikiwa mimi ni mzazi wa Kiislamu/Kikristo na sitaki mwanangu afundishwe kuhusu Biblia/Kurani?

..Sasa kutakuwa na maana gani kumuandikisha mtoto ktk shule ya public ikiwa ataenda kufundishwa DINI[Uislamu au Ukristo]?

Jokakuu:

Kwanini hicho kitabu kisiwekwe KWENYE MANIFESTO YA CHAMA CHA MAPINDUZI. Kwa matatizo tuliyonayo sasa viongozi wa serikali na wa chama tawala wanakiitaji zaidi kitabu hiki kuliko wanafunzi ambao pesa yenyewe hawaishiki.
 
I like JF, watu wana shusha nondo haswa duu..??

Good point, wapate dozi kwanza wao make ni wako mahututi zaidi yetu wote!
 
Wana JF,

..kwanza nimpongeze Mzee Makamba kwa kuandika kitabu kupinga RUSHWA akitumia mifano kutoka ktk KURAN TUKUFU na BIBLIA.

..sasa nimesoma kwamba serikali imeamua kwamba kitabu hicho kitumike mashuleni kuwafunda vijana wetu wachukie rushwa.

..wakati nakubaliana na wazo la kuwafundisha watoto wetu kuchukia rushwa, nina mashaka sana na busara za kutumia mifano ya KURAN na BIBLIA ktk mitaala ya wizara ya elimu.

..hivi kwa uamuzi huu ni nini kitatuzuia baadaye kuamua kufundisha Biolojia,Fizikia, au Kemia kwa kutumia Kurani na Biblia?

..vipi ikiwa mimi ni mzazi wa Kiislamu/Kikristo na sitaki mwanangu afundishwe kuhusu Biblia/Kurani?

..Sasa kutakuwa na maana gani kumuandikisha mtoto ktk shule ya public ikiwa ataenda kufundishwa DINI[Uislamu au Ukristo]?

Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni! Kaandika kitabu cha kupinga rushwa tena kitabu chake kimepasishwa kutumika mashuleni, sijui kigezo gani kilichotumika.

Wakati huo huo hata siku moja hajakemea wala rushwa wakubwa waliojaa ndani ya chama cha majambazi, BoT na siri kali na hata anapoulizwa kuhusu ufisadi wa CCM huwa anakanusha kwamba CCM ni safi! sasa sijui hiyo rushwa anayoipinga huwa inachukuliwa na akina nani!

Huyu hata ujumbe wa nyumba kumi kumi haumfai achilia mbali ukatibu mkuu wa chama cha mapinduzi!
 
Swali la msingi ni kwanini ni kitabu chake na si cha wengine, hapa nauliza kuhusu ubora wake kuzidi vitabu vingine vyote vinavyohusiana na masuala ya rushwa. Je kitabu chake kimepewa upendeleo wa pekee?

Yaaani bongo kuanzia wananchi mpaka serikali tumegeuka Ze-Comedy, yaaani what is this? Eti kitabu cha Makamba? Jamani msalieni mtume wakuu!
 
Jamani Mbona vituko Mwandishi anapalilia na kurutubisha rushwa,halafu awafundishe watoto wachukie rushwa.Hivi Mwalimu asimame mbele ya wanafunzi akiwa mchafu halafu awape mafundisho awambie wawe wasafi wataelewa? Maana wakimwangalia tu wanaona ni mchafu kuliko wao sasa somo hilo litapanda?
 
Back
Top Bottom