Kitabu cha Wangwe chaanika ukweli tunaotakiwa kuujua

Sijaona jipya lolote katika kitabu hicho endapo hayo uliyoeleza ndiyo yaliyomo ndani!
Kama nitanunua kitabu hicho, basi ni kwa nia ya kukiweka kwenye museum yangu, ili watoto wa wanangu waje waone bongo za baadhi ya binadamu zilivyokuwa katika karne hizi za mwanadamu kujivua MAGAMBA kama mjusi-kafiri!

Habari za madai ya 'Uchaga' wa cdm tumezisikia toka mwanzo wa dahari, na hivyo hakuna kitakachonivutia tena kwa suala hilo...na mbaya zaidi ni kuwa tulishajua wanaoeneza maneno hayo kuwa wana nia gani!

Naamini pia (japo mleta mada hajasema hapa) kuwa watakuwa wameongelea juu ya Ukatoliki wa Mbowe, Slaa, au mwinginewe yeyote, maana hizi ndizo hoja na propaganda za wenzetu...hawana la kusema zaidi ya hayo!

Binafsi naamini kitabu hiki kimeandikwa kama mtaji wa kisiasa wa watu fulani(kwa kumtumia na kumlipa fedha mjingamjinga mmoja), na namna ya kujaribu kuiteteresha cdm, jambo ambalo naona ni utoto na KIDUKU ya kipumbavu!

Hata vichaa wanajua kuwa cdm ina uongozi unaokubalika kitaifsa, na ndiyo maana ikasajiliwa na mamlaka husika, sasa mambo ya kudai kuwa inaendeshwa kama kampuni ya mtu binafsi ni ubunifu na usanii wa sanaa-mfu!

Najua kuwa mtakiuza kitabu hicho kwa bei ya kutupa hata kugawa bure ili mradi lengo lenu litimie, lakini kwasasa naogopa mtakuwa mnafanya kazi bure, maana watu wanaelewa vizuri zaidi kwa kujionea wenyewe matendo ya viongozi wao, na kwa asilimia 95 washajua mbinu za MWOVU!
NAWASILISHA!
Hata wafanye nini CDM rocks, Hakuna asiejua kazi inayofanywa na cdm, huyo mwandishi na hao waliomtuma wameonyesha ni jinsi gani harakakat za cdm zinawakosesha watawala usingizi! Cdm rocks
 
Dada Freema
Hapa context iliyopo ni huu uandishi wa vitabu baada ya kufariki wanasiasa!
C.Wangwe alikuwa Mbunge tu, na tokea alipokufa yeye kuna wabunge wengine kadha waliokufa, na hatujaona vitabu vyao, huoni kuwa hapo kuna kitu cha kujiuliza?..Au kama ni kwa vile alikufa kwa ajali, Mbona Salome Mbatia pia alikufa kwa ajali?...au hilo neno la "mtetezi wa wanyonge" ndio linamfanya aonekane alikuwa wa pekee kuliko hawa wengine wanaofariki?
Sijakuelewa bado!

Binafsi nilikuwa namkubali Chacha Wangwe. Nilishtushwa sana na kifo chake cha ghafla. Hivyo nilipopata hiki kitabu, nikafurahi kuwa na kumbukumbu ya mpiganaji shujaa aliyesimamia analoliamini liko kwa manufaa ya wengi hata pale alipoitwa mvuta bangi. Huwa namkumbuka na kuwaza kila ninapoona CHADEMA wanasuasua hata katika mambo madogo madogo nikiamini angekuwepo Chacha angesaidia kuwaweka sawa, God knows better.

Chacha alikuwa na mchango wa pekee katika kuhuisha demokrasia nchini na ndani ya chama chake, na pia katika juhudi za kupambana na ufisadi ndani ya CCM. Aliinua ari ya mageuzi ya kisiasa na nguvu yake wote tunaijua.

Tusisite kumuongelea kwa vile hawajaongelewa wengine. Two wrongs do not make a right.
 
Mzito Kabwela,

Wewe ulitaka hicho kitabu kitoke wakati gani?
vilishaandikwa vya namna hiyo wananchi wakapuuza na sasa wakati chadema inapambana na MIJIZI ndo huyo fisadi nae anatoa chake ili ku-waterdown nguvu ya chadema kwenye mapambano.
CCM walivyo wapuuzi watalipia airtime TBC ili wakipromote hicho kijarida
 
Freema, Chacha Wangwe (RIP) hakuwahi kuvuta bangi? Je alipoitwa mvuta bangi alisingiziwa?

Kuvuta au kutokuvuta kunaweza kusiathiri utendaji wake na hakuondoi dhana ya upiganaji kama alikuwa nao.

Tatizo ni propaganda zinazofanywa kuonyesha kwamba ile Corolla ilivyopata ajali kulikuwa na mkono wa mtu. Huo ni uongo. Kama kuna ambaye ana ushahidi au hata taarifa tofauti ni vyema akautoa badala ya haya maneno ya mtaani.

Huyo Deo Mack mwandishi wa kitabu namsikia leo kwa mara ya kwanza. Ameandika kitabu gani kingine?
 
Freema, Chacha Wangwe (RIP) hakuwahi kuvuta bangi? Je alipoitwa mvuta bangi alisingiziwa?

Kuvuta au kutokuvuta kunaweza kusiathiri utendaji wake na hakuondoi dhana ya upiganaji kama alikuwa nao.

Tatizo ni propaganda zinazofanywa kuonyesha kwamba ile Corolla ilivyopata ajali kulikuwa na mkono wa mtu. Huo ni uongo. Kama kuna ambaye ana ushahidi au hata taarifa tofauti ni vyema akautoa badala ya haya maneno ya mtaani.

Huyo Deo Mack mwandishi wa kitabu namsikia leo kwa mara ya kwanza. Ameandika kitabu gani kingine?

Je kama atakuwa ameandika kitabu kingine chochote ndio utaamini aliyoandika kwenye kitabu hiki?

Any way, hapa kama ulivyoanza kujadili jadili kwa sababu gani yaliyoandikwa kitabuni ni ukweli au uongo; sio kumzima mleta mada kafanya dhambi kuleta hii mada.

Hii ndio cost ya transparency tunayoililia, sio tu kutoka serikalini bali pia kwenye vyama vya upinzani na taasisi zote.
 
KAMBOTA;1885507]Nimesoma kitabu chenye jina la "Chacha Wangwe mtetezi wa wanyonge" kilichoandikwa na mwandishi Deo Mack ambapo nasema bila kupindisha maneno kuwa kinawadhalilisha Mbowe , John Mnyika na CHADEMA, mfano rahisi ukisoma ukurasa wa 71 mpaka 74 inaelezwa kuwa marehemu Chacha Wangwe alikuwa anapambana na ubabaishaji wa Mbowe katika uongozi ndio maana Mbowe alikuwa akimwekea mizengwe pia ingawaje mwandishi hajataja waziwazi ila kwa jinsi alivyoelezea mambo yake ni kama vile anaihusisha CHADEMA na kifo cha Chacha Wangwe.
Sasa Bwana Kambota,mbona na wewe unakuwa mbabaishaji kama huyo Deo Mack?Unabainisha waziwaz kuwa mwandishi hajataja waziwazinamna gani Mbowe alikuwa anamwekea mizengwe Chacha Wangwe YET unahitimisha "bila kupindisha maneno" kuwa kitabu hicho kinawadhalilisha Mbowe,John Mnyika na Chadema!!!Mwenyekiti Mao aliwahi kusema NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK.Huwezi kuwa-implicate Chadema na kifo cha Wangwe pasipo ushahidi wa kueleweka.Kama mwandishi ameshindwa kuthibitisha madai yake,iweje basi madai hayo yapelekee kuidhalilisha Chadema?Kichaa yoyote yule anaweza kukurupuka na kutoa madai kuhusu jambo flani.Wapuuzi wachache wanaweza kuamini madai hayo.Nawaita wapuuzi kwa vile ni wavivu wa kushughulika bongo zao kujiuliza maswali beyond wanachoambiwa.

Tunazungumzia MAUAJI ya mwanasiasa maarufu.Na haihitaji ujuzi mdogo tu kufahamu kuwa katiika mazingira ya uhasama kati ya CCM na Chadema,mafisadi wangetumia kila mbinu kuhakikisha jambo hilo linawamaliza Chadema.And actually,they tried their best level,lakini siku zote ukweli una-prevail juu ya uongo,uzushi,majungu,hear say na ubabaishaji.

Tell you what,bwana mdogo,you're not the only one trying.Zimejaribu mamlaka zenye nguvu zikashindwa,and so will you.
Pia mwandishi huyu anadai kuwa John Mnyika ni mnafiki wa kutupwa kwa madai kuwa alimkana Deo Mallya aliyekuwa dereva wa Wangwe wakati alikuwa anamfahamu
How did he know?Na hata tukiamini kuwa Mnyika alikuwa anamjua Mallya,how did that amount to mchango wa mwanasiasa huyo katika kifo cha Wangwe?Kuna tofauti kati ya kumfahamu mtu na kufahamiana.Kwa mfano,nakufahamu wewe kuwa mtu unayejaribu kuandika makala lakini hatufahamiani.Kwa kiingereza,ni tofauti kati ya TO KNOW and TO KNOW EACH OTHER.

pia mwandishi anachagiza kwa tuhuma kuwa CHADEMA inapendelea wachaga na wote wanaojinyenyekeza kwa Mbowe
Kweli akutukanae hakuchagulii tusi.Hata hivyo,nakusihi ujaribu kutambua na kuheshimu uwezo na uhuru wa kila Mtanzani kupenda na kuchagua apendacho.Kuituhumu Chadema inapendelea Wachagga pasipo takwimu za kusapoti tuhuma hizo ni uwendawazimu wa daraja la juu.Lakini hizi sio tuhuma mpya dhidi ya Chadema.Zilijaribiwa huko nyuma lakini zikashindwa kuzaa matunda yaliyotarajiwa.Zikaletwa tuhuma za udini lakini nazo hazijaweza kuzaa matunda.Majaribio ya character assassination kama vile Mbowe kudaiwa na NSSF au private life ya Dkt Slaa pia vimeshindwa kupunguza kasi ya Chama hicho.Kwanini tusiwanyooshee vidole wanaotuhumu ukabila kwamba wao wenyewe ni wakabila?Bcoz kama unaangalia tu kabila ya mtu na kupuuza vigezo vingine kama elimu,ukaribu,jiographia,ushawishi,mvuto,nk utakuwa unafanya analysis ya kilevi.

huku akitupa kombora lake kwa kuhitimisha kuwa Mbowe anaendesha CHADEMA kama NGO yake na familia yake
Haya ni matusi kwa mamilioni ya Watanzania wanaoisapoti Chadema.Hivi ndani ya Chadema kuna akina Mbowe wangapi hadi atuhumiwe kuendesha chama hicho kifamilia?Hii sio chuki bali mtindio wa ubongo hasa kwa vile wakati unatoa tuhuma mfu kuhusu Mbowe kuendesha Chadema kama NGO ya familia yake,hutaki kuangalia upande wa pili wa namna Kikwete na familia yake wanavyoendesha nchi.Je mwanafamilia gani wa Mbowe ana nguvu kama Ridhiwani huko UVCCM?Je kaka/mdogo wa mbowe ni kiongozi wa Chadema as related to kaka ya Kikwete?Mke wa Mbowe na mama Salma je?

...je huku kama sio kudhalilisha CHADEMA ni nini?
unamuuliza nani ilhali umeshatamka bayana "naandika bila kupindisha maneno kuwa kitabu husika kinawadhalilisha Mbowe,Mnyika na Chadema?

mbona wahusika wapo kimya?

Unataka wakujibu nini?Wakishakujibu utabadili msimamo wako?kama umeshawahukumu kabla ya kuwasikiliza,what's the point kwa wao kulumbana nawe?
Kwa sababu wamekupuuza..
Tafakari!
Ili iweje?
 
Huu ni mwendelezo wa propaganda dhidi ya CHADEMA. Walianza na udini wakapuuzwa, ukabila wakapuuzwa, chama cha msimu wakapuuzwa, kikundi cha wanaharakati wakapuuzwa, Uhaini wakapuuzwa na hilo nalo lilishapuuzwa wakati wa uchaguzi mdogo wa Tarime hadi CHADEMA wakatetea jimbo lao. Nilidhani baada ya CCM kujivua gamba na kuwatimua waropokaji kama Makamba na Tambwe Hiza ingeacha hizi siasa za maji ya taka kumbe ndio wanakuwa wapuuzi zaidi.
 
Hakuna mwandishi yeyote aliyeandika kitbu juu ya kifo cha Kolimba?
Au aliyeandika kuhusu Balali ambaye yeyote mwenye akili anaamini HAJAFA?
Au kifo cha Salome Mbatia?
Au kifo cha Mzee Karume??
Na hicho cha Wangwe kutoka nyakati hizi ni coincidence au??
Nauliza tu jamani
Hata mimi namwunga mkono Kabwela. Sasa tunataka kusikia habari za jinsi CCM walivyohusika kuuondoa uhai wa Horace Kolimba ambaye ndiye mtabiri wa kwanza wa CCM kupoteza uelekeo, Kighoma Malima ambaye baada ya "kuisaliti" CCM na kuunda chama chake cha NRA alikufa ghafla, Salome Mbatia aliyeuwawa kwa "ajali" ya gari Iringa ambaye duru zinaonyesha aliuwawa kwa bahati mbaya tu kwani mlengwa wakweli alikuwa Mh. Zitto Kabwe ambaye gari lake lilikuwa mbele ya msafara wa mama yule lakini akasimama kwa muda ili akate kiu hivi kutoa mwanya kwa gari lililokuwa limembeba mama yule kuwa mbele. Wote tulisikia kilichotokea na baadae police cover up iliyofuatia mpaka leo hatujasikia hatua zilizochukuliwa kwa muuaji na wapangaji wa mauaji yale kina Makamba.
Kifo cha Wangwe kimetumika sana katika propaganda za CCM na ndicho kilisababisha CCM kukosa jimbo la Tarime baada ya wenyeji wakule kuupima ukweli na kugundua hila na uongo wa CCM. Ni CCM haohao waliojipenyeza katika kila idara zikiwemo polisi, Mahakama, Usalama wa Taifa waliofanya juu chini ili yule kijana muuaji wa Chacha Wangwe kuachiwa! Sijui kama huyo mwandishi kibaraka wa CCM ameandika nini juu ya "Nyaraka" za Chacha Wangwe inazosemekana aliziandaa eti kuiumbua CHADEMA kuwa mikononi mwa Makamba masaa machache tu baada ya kifo chake. Hili ni nini kama si kuhusika moja kwa moja kwa CCM katika kifo cha kada wa CHADEMA yule?
Nina uhakika Tanzania siku moja itapata serikali yenye kuwajibika itakayochunguza vifo vyote vyenye utata kama hivi na mchawi kupatikana. Kwa kifupi kitabu cha Deo kinachochea tu hasira zetu dhidi ya chama kilichoigandamiza na kuiifilisi nchi hii zaidi ya alivyofanya mkoloni wa kiingereza! Ipo siku watanzania wanyonge wataamka na kusema sasa basi tumetosheka, na wahusika wa hujuma zote watafikishwa mbele ya haki. Hapo ndipo Tanzania itakapokuwa imerudisha heshima yake tuliyojengewa na Baba wa Taifa lakini ambayo iliporwa na manyang'au waliojipenyeza na kuiteka CCM iliyokuja geuka kuwa mwiba wa tende kwa wananchi. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
chama hiki ni cha kikabila, cha kichagga cha kindugu zaidi. mwenye macho haambiwi tazama
 
kuna mambo mengine kwenye kijitabu hicho huenda yamepikwa, maana kwanini kitolewe wakati huu, inatia shaka kidogo, maana tutathibitishaje kua mchapaji hakuongeza yake, ninani amehariri hiyo kazi. ni maswali yanayo nijia.
mbona wanaoshabikia kitabu hiko ni walewale ambao wameonyesha rangi zao stahiki katika kushabikia mgogoro ndani ya CHADEMA.
MAISHA MAREFU KWA CHADEMA


Mbinu kubwa ambayo CCM imekuwa inatumia kudhoofisha upinzania ni hii ya kuchochea migogoro ya ndani kwenye hivi vyama vya upinzani. Lyatonga Mrema amekuwa mtekelezaji mahiri katika zoezi zima la uvurugaji. Ni vigumu ku-imagine historia ya mtu kama huyu Mrema itasomekaje kwa wajukuu na vituu vya nchi hii. Wanasema ukuiishi kwa upanga utakufa kwa upanga na Mungu si Athumani, maana sasa domestic violence imahamia CCM and its killing them squarely.

Nadhani hata timing ya hiki kitabu ni kwamba hawakutegemea kama wao CCM wangekuwa so consumed na zoezi la kujivua magamba ambalo kimsingi limeibuwa 'domestic violence- endelevu'. haponi mtu!
 
Hayo yalishapita, ila kama kuna yaliyobaki bila kufanyiwa kazi basi tutayatazama. Nafikiri hata wewe unaona tufauti ya cdm ya wakati ule na sasa. Hiyo ni historia sasa.:whoo:
 
Narudia tena. Chadema si chama cha siasa makini. Ni genge la mafisadi weusi!
Inasikitisha kwamba watanzania wengi wenye uchungu na nchi yao wanatumiwa na genge hili kwa manufaa ya familia moja au ukoo mmoja.
Watanzania tuna genuine grievances ila CDM ni wrong platform. They are manipulating us.
Wake up people, let us find a genuine platform!

CDM ni Mabepari WEUSI---------------------J.K Nyerere!
 
Hizi ni propaganda ambazo zipo na zinasemwa kila siku, kwenye siasa kila mtu anajua jinsi ya kurusha makombora na jinsi ya kujitetea, kitabu kinaandikwa na binadamu kama mimi, naweza kuandika chochote, hili suala la Wangwe huwa linaletwa hapa pindi tu CCM inapokuwa katika hali ya kiama, nadhani hiyo ndiyo imekuwa kama mbinu yao ya kujihami. Waswahili husema '' ukimchunguza sana samaki huwezi kumla'' asanteni
Ni kweli kabisa ni mawazo yake, na mimi naandika changu kuhusu Kolimba alivyofariki baada ya kulikosoa joka kuwa limekosa muelekeo!
 
Vyama Vipo vingi, hata kipindi Chacha alikuwa hai vilikuwepo. Je alifungwa kamba kujiunga na CDM. Na wote waliojiunga na CDM je hufanya hivyo kwa kulazimishwa?
Kama ni kweli CDM ni NGO ya Mbowe, sioni kwa nini wanaume na wanawake wenye akili timamu hawafanyi maamuzi kuondoka huko waende vyama vingine vilivyo huru na uongozi safi? au watu wenye vision kama anavyopendekezwa Chacha Wangwe kwa nini hakuondoka kuanzisha Chama chake ili atimize adhma yake njema ya kuwatetea watanzania?
Sioni watu wazima kwa msingi upi wakubali kuendelea kubuluzwa na Mwanaume mmoja, mwenye udini na ukabila na ujimbo ilhali wao ni kabila tofauti, dini tofauti na wa majimbo tofauti?
Ushahidi wa uzuri wa CDM uko kwenye uungwaji mkono na wananchi. Kama wasomi hawaungi mkono ni bora!
Kama akili zetu zinaweza kufikiri hivi tu kama mleta thread hii, ni bora tusiwe hai kama Wangwe. Kwani aliye kufa mapenzi yake. na chuki zake zimekufa pamoja naye.
 
Narudia tena. Chadema si chama cha siasa makini. Ni genge la mafisadi weusi!
Inasikitisha kwamba watanzania wengi wenye uchungu na nchi yao wanatumiwa na genge hili kwa manufaa ya familia moja au ukoo mmoja.
Watanzania tuna genuine grievances ila CDM ni wrong platform. They are manipulating us.
Wake up people, let us find a genuine platform!

CDM ni Mabepari WEUSI---------------------J.K Nyerere!

A son of a snake is a snake even if he removes his skin he bites, I am afrad of you. stay awa:spy:y
 
Binafsi nilikuwa namkubali Chacha Wangwe. Nilishtushwa sana na kifo chake cha ghafla. Hivyo nilipopata hiki kitabu, nikafurahi kuwa na kumbukumbu ya mpiganaji shujaa aliyesimamia analoliamini liko kwa manufaa ya wengi hata pale alipoitwa mvuta bangi. Huwa namkumbuka na kuwaza kila ninapoona CHADEMA wanasuasua hata katika mambo madogo madogo nikiamini angekuwepo Chacha angesaidia kuwaweka sawa, God knows better.

Chacha alikuwa na mchango wa pekee katika kuhuisha demokrasia nchini na ndani ya chama chake, na pia katika juhudi za kupambana na ufisadi ndani ya CCM. Aliinua ari ya mageuzi ya kisiasa na nguvu yake wote tunaijua.

Tusisite kumuongelea kwa vile hawajaongelewa wengine. Two wrongs do not make a right.

Naona mpo wengi mnaomshabikia Chacha, muundieni Chama muendeleze mawazo yake.
 
Tangu Msekwa kuchukizwa na JF imekuwa balaa humu, hapashikiki, kuna mamluki wa kike na wa kiume nadhani watakuwa wamepatiwa modem za bure kuhakikisha kwamba wanarudisha hadhi ya CCM kama ilivyokuwa awali. CCM ni watu wenye siasa za ubaguzi sana, kwanza walianza kwa siasa za udini wakiwatumia Waislam, na sasa Wanataka kutuaminisha kwamba CHADEMA ni chama cha ki kabila kwa kutumia kifo cha Wangwe, Kuna ushahidi gani au ni maneno tu ya kuandikwa na mtu anayenufaika na ufisadi wa CCM? hawa jamaa ni mabingwa sana wa kuandika Vitabu, nakumbuka baada ya JK kuingia madarakani kuna mtu aliandika kitabu cha kumpamba , kinaitwa '' JAKAYA KIKWETE, TUMAINI JIPYA LILILOREJEA KWA WATANZANIA'' nadhani hiyo ndiyo heading, kama kuna mtu anaikumbuka vizuri naomba anisahihishe, lakini kiufupi ni kwamba Mti mwema ndio hupondwa mawe.
 
Mwandishi wa Kijarida hiki alipaswa atueleze uhusiano wa kipekee kati ya Dr Walid Aman Kaburu, Rostam Aziz, Makamba,Chacha Wangwe, na mgodi wa North Mara... Watanzania tunajua uharamia unaofanywa na Barrick kwa kushirikiana na JOKA KUU... hata mjivue magamba ya matakoni haitowasaidia! watanzania tumeamka na tuko tayari kuwa mwagia chumvi ya kutosha popote mnapopita mteseke mpaka mfe kifo dhalili...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom