Kitabu Cha Wakristo na Biashara ya Utumwa.

doriani

Member
Nov 24, 2019
42
38
Hiki ni kitabu kikongwe katika vitabu vingi hapa Ulimwenguni hata kuzidi kitabu cha Waislamu, na tuangalie kwa pamoja habari hii ya biashara ya watumwa.

Utumwa katika dunia. Tukianzia katika miaka ya kiza mwenye nguvu ndie atawale. Vita vinapotokea baina ya nchi na nchi au kabila hii na kabila ile, wale watakao shindwa vitani hao huchukuliwa mateka.

Hivyo walishinda vita hiyo ni hiari yao kuwauwa hao mateka au kuwatumia kwa shughuli zao kama Wataona inafaa kufanya hivyo. Ikiwa watawatumikisha basi hapo huitwa watumwa.

Utumwa una historia ndefu sana, kwa mfano, katika kitabu kikongwe cha Wakristo unapokisoma utaona dhahiri kwamba Utumwa uliruhusiwa na Mungu kama nilivyo nukuu sehemu hizi:
Tena katika habari za Watumwa wako na wajakazi wako, utakao kuwa nao mataifa
yaliyo kandokando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi wako, utakao kua nao mataifa yalio kando kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi. (Walawi 25:44).

(Anaambiwa Nabii Ibrahim na Mungu).

Mtu mwizi anauzwa.(Kutoka 21:32).
Nae akamtendea Abraham mema kwa ajili yake nae alikuwa na Kondoo, na ng'ombe, na punda waume, na Watumwa na wajakazi. (Mw 12:16.)

Usitamani nyumba ya jirani yako, Usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake. (Kutoka 20:17.).

Hapa yaonesha biashara ya Utumwa ilikuwa rukhsa kwa mujibu wa kitabu hiki kikongwe cha Biblia.
Ndani ya kitabu cha Christianity in Afrika kiliandika yafwatayo:

"Hata kukamata watumwa na biashara ya watumwa vilifahamika kuwa ni vitendo vya uchamungu vya Kikristo kwa sababu vilionekana hivyo ndio njia iliyokuweko ya kuokowa roho za washenzi."

Na ndani ya kitabu kiitwacho The New Congo kimeandika kuwa:

"kwa miaka mia tatu na khamsini (350) mfunulizo mapadri hao wakaendesha kazi ya kukamata watumwa ili kuokowa roho zao kwani walistahiki ya kwamba si vibaya
Kama mili yao iteseke utumwani endapo roho zao zitaokoka huko mbinguni kwa Bwana Yesu".

Vile vile ndani ya kitabu cha "Labour and Slavery in Christianity" tunasoma kwamba Papa Leo II aliwaandikia barua Maaskofu wa Brazil kuwa Yesu hasemi neno lolote liwalo la kupinga utumwa, na kwamba amekubali utumwa kama vile alivyokubali maneno mengine na ya kwamba watumwa hawamtumainii Yesu msaada wowote.

Na ndani ya" Encyclopaedia of Religion" Jalada la II, UK 602 Inaeleza kwa kusema
"katika mafunzo ya Mungu wetu hakupatikani kuchukia utumwa na hakuna hata dalili moja inayoonesha kuharamisha utumwa".

Baada ya Papa kutowa rukhsa ya kukamata watumwa meli mbili za kubebea watumwa hao zilipelekwa na majina ya meli hizo moja ilipewa jina la Yesu na ya pili ilipewa jina la Maria. Mambo hayo yalitia fora wakati wa utawala wa Wakristo huko Roma.

Halafu kitu cha kushangaza ndani ya Biblia utaona kitabu hiko kinatowa miongozo juu ya watumwa. Mfano:

"Watumwa watiini walio bwana zenu kwa
jinsi ya ya mwili kama kwamba kumtii Kristo, kwa hofu na kutetemeka kwa unyoofu wa moyo."
(Waefeso 6:5)

"Wowote walio chini ya mafunzo hali ya utumwa, wawahesabu bwana zao kuwa wamestahili heshima yote".
(1 Timotheo 6:1)

Na istitoshe ndani ya "Insight on the scripture Vol II UK 977 unaeleza hivi
" For a Slave to have a Christian master was a blessing". Yaani kwa mtumwa kuwa na Bwana wa Kikristo ni baraka kwake.

NI vizuri kwa wale wanao zungumza Uwarabu na Utumwa kwanza wasome darasa hili wa jitahidi kupekuwa na kupembuwa kisha walete hoja na ushahidi wa dini ya Kiislamu juu ya habari za utumwa. Uislamu na Uwarabu ni vitu viwili tofauti. (Soma ujuwe).
 
Huu ni upuuzi, na wenye kuufanya ni wale wasiyo na mambo ya maana ya kufanya...kwanza ni tabia za waswahili kulumbana kwenye mambo ambayo hayana maana kwao na yaliyowazidi upeo!
 
Horseshoe. Unajuwa kwako unaona upuuzi kwa vile umeamini ubaya wa Kanisa juu ya biashara ya utumwa. Kama sisi tunvyoamini unyama wa Waarbu walioutenda kwa ndugu zetu. Dogo lako ni kubwa kwa mwenzako. Upuuzi kupewa maandiko na ushahidi wa matokeo ya mapapa na mapadri au na wewe ni miongoni mwa waliosibiwa na jambo hilo kwani ulikuwa ukiyajuwa hayo au leo ndio yamekutowa taka za msikio.?

Nikupashe basi kama huyajuwi. Kilasiku ya Mungu taasisi mbali mbali kutoka Tanganyika zinavushwa bahari kupelekwa Zanzibar kwenye Kanisa la Mkunazini ili kuongeza chuki na uaduwi baina ya watu wa Bara na Zanzibar kwa kutumia karata za biashara ya utumwa fhidi ya Waarabu na kuficha ukweli wa mambo kama hayo ulikwisha yasoma ndani ya Makala haya. Sasa utasemaje kuwa sina kazi ya kufanya ndio naandika vitu vya aina hiyo?

Sasa nani mpuuzi zaidi mimi mwenye kuelezea historia hii au hao wanao vusha watu kutoka Bara kuja Zanzibar kwa kuweka chuki ndani ya raia wa nchi moja?
TAFAKARI.
 
william wilberfoce alipambana na utumwa Waarabu mpaka leo biashara inaendela

William Wilberforce (24 August 1759 – 29 July 1833) was a British politician, philanthropist, and a leader of the movement to abolish the slave trade
 
ENCYCLOPEDIA OF RELIGION
 
Attachments

  • ENCYCLOPEDIA OF RELIGION_Lindsay Jones.pdf
    11.6 MB · Views: 3
Wakurochi unazungumza Waingereza mbona wao ndio walifunguwa Bank ya Barclay kwasababu ya biashara ya utumwa hata hao Waingereza waluzana wao kwa wao katika biashara ya utumwa. Hata Malkia wa I wa Uingereza alifanya biashara sana ya kununua watumwa. Wachina, wahindi, Waafrika na wazungu wote walifanya biashara ya utumwa ndio hilo neno "BIASHARA" nani asifanya biashara hiyo labda Machifu yaani watemi ambao ni mababu zako yawezekana hawakufanya lakini makabila yote yamefanya biashara hiyo. Mabibi zetu ndio walikuwa wajakazi wa Waarabu na wakazaa nao na ndio tukapatikana sisi waswahili na MACHOTARA wa kiarabu kwa kuzaliana na bibi zetu sio nyie ni sisi MACHOTARA wa kibantu na Waarabu. Sisi ndio wakulaani sio nyinyi mabibi zenu ndio wametuzaa sisi MACHOTARA hapa visiwani. Kelele zenu za nini sasa.?
 
Horsishoe tumewekewa "Jukwaa la Historia" Sasa unaposema kwamba mtu anae andika hivi hua hana kazi ya kufanya. Hebu jitathmini uone kosa lako la kukemea mtu anaetumia mlangu huu wa Jukwaa la Historia kuwa ni mpuuzi hana kazi ya kufanya.
 
Wakurochi unazungumza Waingereza mbona wao ndio walifunguwa Bank ya Barclay kwasababu ya biashara ya utumwa hata hao Waingereza waluzana wao kwa wao katika biashara ya utumwa. Hata Malkia wa I wa Uingereza alifanya biashara sana ya kununua watumwa. Wachina, wahindi, Waafrika na wazungu wote walifanya biashara ya utumwa ndio hilo neno "BIASHARA" nani asifanya biashara hiyo labda Machifu yaani watemi ambao ni mababu zako yawezekana hawakufanya lakini makabila yote yamefanya biashara hiyo. Mabibi zetu ndio walikuwa wajakazi wa Waarabu na wakazaa nao na ndio tukapatikana sisi waswahili na MACHOTARA wa kiarabu kwa kuzaliana na bibi zetu sio nyie ni sisi MACHOTARA wa kibantu na Waarabu. Sisi ndio wakulaani sio nyinyi mabibi zenu ndio wametuzaa sisi MACHOTARA hapa visiwani. Kelele zenu za nini sasa.?
sahihi sana lakini mwaka (1784–1812) hao haeio waingereza wakaanza kujadili jinsi ya kutokomeza hii biashara. hii bungeni mbona huongelei hilo usichague historia haifutiki.
waarabu mpaka leo wanauza watu mnadani i.e
 
Kilicho wa fanya Waingereza kupiga marufuku biashara ya utumwa ni Mapinduzi ya viwanda ambayo yaliweza kuleta afueni ya kuwapeleka watumwa ulaya. Baya zaidi sasa wakaja kuzipora nchi zao hao watumwa wenyewe na kuwatumia katika ardhi zao na kuwalazimisha kuzilima Ardhi zao wenyewe hao watumwa. Unyama mara mbili zaidi wamezidisha. Ndio sasa ikawa hawataki kuona vinaondolewa vitendea kazi vyao na kuhamisha kwenye Ardhi walizozipora za hao watumwa hip ndio sababu ya kupiga marufuku kuwaondowa maana mtumwa yule yule anae na Ardhi yao wameipora.
 
mabibi zenu ndio wametuzaa sisi MACHOTARA hapa visiwani. Kelele zenu za nini sasa.?
Km mnajua sisi ni ndugu wa Bibi mmoja , mbona mna kiburi, Ubaguzi, kejeli na dharau kwa weusi? kuliko hata Muarabu original? mnatamani kujitenga?

Yaani mpo, mpo tu, hamueleweki kama rangi zenu, tukikandamizwa sana na wazungu, au tukikutana mitaani huko Oman mnajiita nyie ni waarabu,
Tukikamata Dola nchi na kubinafsisha mali za Mabepari, Mandela akiwa maarufu tu, mnaanza.

Oooh! sisi ni waafrica tu wenzenu, chotara! eti mlizaliwa na bibi Mtumwa Mdengeleko! mara mkurya!
Bibi aliwazaa siyo kwa ridhaa yake alilazimishwa, apigwe mkuyenge na vitisho vingi, vya kupewa kazi ngumu! walikuwa hawatongozwi!
 
Waingereza waluzana wao kwa wao katika biashara ya utumwa.
Thubutu! Mzungu alikuwa hawezi kazi ngumu! kufungwa tu nyororo jioni huyu! kavimba!

akikaa sehemu chafu yenye kinyesi kimoja tu anakufa! ilikuwa gharama sana kutunza mtumwa mweupe, jahazi kwanza liwe safi, liwe na swimming pool! kuwe na dining table, na madaktari wasiopungua kumi,

chakula kilichopikwa uzuri kwa Gas, siyo moshi wa kuni na maharagwe ya mbeya! na uji wa juzi,
ukimpatia tu hivi vyakula mweupe ataharishia mabaharia mpaka washibe mavi ya watumwa weupe?

Kinyume na hapo utasafirisha harufu ya mahiti walikuwa wanakufa mara moja km nzi! ambayo ilikuwa ni hasara!
 
Nyaru kwani hawa mababerian na Vikings hawa washenzi hasa wa kizungu ni watu makatili wa kila nyama mbichi waliuzana kwani hao Maslavia ni wazungu na wanaitwa SLAVIA Maana yake ni Slave.
 
Barbarics/Barbarian- means some one who is brutal, unsophisticated manner of living, Primitive, Heartless, Stony hearted.

Ni neno la Kigiriki Barbados, wahuni majambazi walikuwa pwani ya Africa kaskazini, hawa hawakufanya biashara ya utumwa, bali ujambazi,
 
mababerian
Katika utawala wa Wagiriki ambao ndo waarabu wa leo, lilianzia kwao, Barbarian alikuwa mtu asiye ongea Kigiriki, kwa ufasaha, na wengi walikuwa ni kabila la Goth- Germany, ambao badaye walikuwa mwiba kwao.

taratibu jina likabadilika. na kuwa cruel.

Hakuna mtumwa Muarabu wala mzungu wale walikuwa waungwana bana!, kidooogo Wahindi lkn pia walipewa kazi laini, km kujenga Reli. na biashara.

Viking walikuwa wapya ktk nchi mpya during ICe age, ilibidi walane kwa zamu sababu hakukuwa na chakula.
 
sahihi sana lakini mwaka (1784–1812) hao haeio waingereza wakaanza kujadili jinsi ya kutokomeza hii biashara. hii bungeni mbona huongelei hilo usichague historia haifutiki.
waarabu mpaka leo wanauza watu mnadani i.e
HISTORIA YENU YA UTUMWA IMO NDANI YA BIBLIA,TENA MBAYA ZAIDI
AU HAO WATU WA BIBLIA WALIKUWA WAARABU PIA?
 
sahihi sana lakini mwaka (1784–1812) hao haeio waingereza wakaanza kujadili jinsi ya kutokomeza hii biashara. hii bungeni mbona huongelei hilo usichague historia haifutiki.
waarabu mpaka leo wanauza watu mnadani i.e
Nielekeze na mimi ,uko wapi huo mnada wa watumwa siku hizi?
ili nikajipatie angalau watumwa waili wa kunisaidia kazi.
 
Hiki ni kitabu kikongwe katika vitabu vingi hapa Ulimwenguni hata kuzidi kitabu cha Waislamu, na tuangalie kwa pamoja habari hii ya biashara ya watumwa.

Utumwa katika dunia. Tukianzia katika miaka ya kiza mwenye nguvu ndie atawale. Vita vinapotokea baina ya nchi na nchi au kabila hii na kabila ile, wale watakao shindwa vitani hao huchukuliwa mateka.

Hivyo walishinda vita hiyo ni hiari yao kuwauwa hao mateka au kuwatumia kwa shughuli zao kama Wataona inafaa kufanya hivyo. Ikiwa watawatumikisha basi hapo huitwa watumwa.

Utumwa una historia ndefu sana, kwa mfano, katika kitabu kikongwe cha Wakristo unapokisoma utaona dhahiri kwamba Utumwa uliruhusiwa na Mungu kama nilivyo nukuu sehemu hizi:
Tena katika habari za Watumwa wako na wajakazi wako, utakao kuwa nao mataifa
yaliyo kandokando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi wako, utakao kua nao mataifa yalio kando kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi. (Walawi 25:44).

(Anaambiwa Nabii Ibrahim na Mungu).

Mtu mwizi anauzwa.(Kutoka 21:32).
Nae akamtendea Abraham mema kwa ajili yake nae alikuwa na Kondoo, na ng'ombe, na punda waume, na Watumwa na wajakazi. (Mw 12:16.)

Usitamani nyumba ya jirani yako, Usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake. (Kutoka 20:17.).

Hapa yaonesha biashara ya Utumwa ilikuwa rukhsa kwa mujibu wa kitabu hiki kikongwe cha Biblia.
Ndani ya kitabu cha Christianity in Afrika kiliandika yafwatayo:

"Hata kukamata watumwa na biashara ya watumwa vilifahamika kuwa ni vitendo vya uchamungu vya Kikristo kwa sababu vilionekana hivyo ndio njia iliyokuweko ya kuokowa roho za washenzi."

Na ndani ya kitabu kiitwacho The New Congo kimeandika kuwa:

"kwa miaka mia tatu na khamsini (350) mfunulizo mapadri hao wakaendesha kazi ya kukamata watumwa ili kuokowa roho zao kwani walistahiki ya kwamba si vibaya
Kama mili yao iteseke utumwani endapo roho zao zitaokoka huko mbinguni kwa Bwana Yesu".

Vile vile ndani ya kitabu cha "Labour and Slavery in Christianity" tunasoma kwamba Papa Leo II aliwaandikia barua Maaskofu wa Brazil kuwa Yesu hasemi neno lolote liwalo la kupinga utumwa, na kwamba amekubali utumwa kama vile alivyokubali maneno mengine na ya kwamba watumwa hawamtumainii Yesu msaada wowote.

Na ndani ya" Encyclopaedia of Religion" Jalada la II, UK 602 Inaeleza kwa kusema
"katika mafunzo ya Mungu wetu hakupatikani kuchukia utumwa na hakuna hata dalili moja inayoonesha kuharamisha utumwa".

Baada ya Papa kutowa rukhsa ya kukamata watumwa meli mbili za kubebea watumwa hao zilipelekwa na majina ya meli hizo moja ilipewa jina la Yesu na ya pili ilipewa jina la Maria. Mambo hayo yalitia fora wakati wa utawala wa Wakristo huko Roma.

Halafu kitu cha kushangaza ndani ya Biblia utaona kitabu hiko kinatowa miongozo juu ya watumwa. Mfano:

"Watumwa watiini walio bwana zenu kwa
jinsi ya ya mwili kama kwamba kumtii Kristo, kwa hofu na kutetemeka kwa unyoofu wa moyo."
(Waefeso 6:5)

"Wowote walio chini ya mafunzo hali ya utumwa, wawahesabu bwana zao kuwa wamestahili heshima yote".
(1 Timotheo 6:1)

Na istitoshe ndani ya "Insight on the scripture Vol II UK 977 unaeleza hivi
" For a Slave to have a Christian master was a blessing". Yaani kwa mtumwa kuwa na Bwana wa Kikristo ni baraka kwake.

NI vizuri kwa wale wanao zungumza Uwarabu na Utumwa kwanza wasome darasa hili wa jitahidi kupekuwa na kupembuwa kisha walete hoja na ushahidi wa dini ya Kiislamu juu ya habari za utumwa. Uislamu na Uwarabu ni vitu viwili tofauti. (Soma ujuwe).
Hahahaha! Utumwa huo wa biblia si wa waarabu ni mahausboi au mahausigeli. Vijakazi. Jisikie aubu bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom