Kitabu cha ujinga wa mwafrika

MJINI CHAI

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
2,196
1,218
wakuu nawaombeni mwenye kitabu tajwa hapo juu nakihitaji sana hasa kipindi hiki cha waTZ kutaka KATIBA mpya(Nataka kukifanyia kazi) kwani kuna kisa cha UCHU WA MZEE MIKIDADI kinaniumiza sana ukilinganisha na hali ya sasa TZ

inauma sanaa
 
mzee wa mikidadi ndio nani? mbona umeniacha mwenzio
wakuu nawaombeni mwenye kitabu tajwa hapo juu nakihitaji sana hasa kipindi hiki cha waTZ kutaka KATIBA mpya(Nataka kukifanyia kazi) kwani kuna kisa cha UCHU WA MZEE MIKIDADI kinaniumiza sana ukilinganisha na hali ya sasa TZ

inauma sanaa
m
 
Nafikiri unataka kitamu kinachoitwa 'Waafrika ndivyo walivyo'? kwa walko ughaibuni ni vigumu sana kukipata, labda huko bondo sijui vipi.
 
kimetoka lini, na kinappatikana wapi? tupashane jamani?

mkuu sikumbuki kilitoka linikwa sababu ni muda kidogo ila kuna kisa cha mzee mmoja anaitwa mzee Mikidadi, kulikuwa na sherehe wakati wa maakuli ulipofika akiwa na watoto akawa anawaambia watoto wale kile chakula (ugali) kwani sikukuu ni yao wakati yeye anakula mapaja ya kuku peke yake wakati ule nasoma niliona kama hadithi tu, nataka kukisoma upya nione Maudhui ya Mwandishi
 
simulizi la "Uchu wa Bwana Mikidadi" libakia kama mfano wa ufisadi uliokubuhu... kulikuwepo na masimulizi mengine mengi ambayo tukiyakumbushia leo hii tunaweza kupigwa marufuku.
 
Umenikumbusha mbali sana ndugu yangu, hata mimi ninakikumbuka sana kitabu hiki na ninakitafuta. Ninakumbuka tulikuwa nancho home enzi tukiwa wadogo sasa kwa ujinga nadhani tulikitelekeza.

Ninakumbuka baadhi ya tipics:
1.uchu wa nzee mikidadi
2.urembo wa ndonya
3.kijimbwa cha mzungu
 
Hebu tukumbushane ...
Leteni yaliyomo kwenye Kitabu tujadili

Du yaani nimekumbuka utotoni kabisa tulikua kama na nakala tatu hivi ya kile kitabu sikumbuki sana content zake kwasababu nilikisoma miaka ya mwisho ya themanini.

Kwa kumbukumbu niliyonayo kilielezea kuhusu matatizo ya waafrika na jinsi tusivyotatua matatizo ya msingi. Kwa kifupi, kinaelezea, sababu zinazo tuletea umaskini katika mila zetu ni kutoweka vipaumbele katika mambo muhimu ya maendeleo. Tunatumia muda mwingi kwenye mambo ya starehe na ushirikina.

Mfano badala ya kumpeleka mgonjwa hospitali anapelekwa kwa waganga wa kienyeji. kitabu kile kianelezea jinsi jamii zetu za kiafrika zinavyopenda kuamini mambo ya ushirikina. Nakumbuka kuna baadhi ya sura nilikuwa naogopa kuzisoma (LOL) , nilikuwa kama na miaka 6 hivi, kwasabau picha zake zilikuwa zinanitisha kidogo.

Kuna kisa ambacho Mzee Mikidadi (muhusika mkuu) anawaahidi wanawe jinsi atakavyo waandalia sikuku, wanawe wanafurahi na kujiandaa kwa hamu, kuja kushituka ni ahadi tuu ya maneno.

Katika kitabu hicho kuna picha ya Mzee Mikidadi akiwa na watoto wake huku yeye akila kuku wakati watoto wanakula wali kwa mchuzi. Ana waambia watoto wake "kuleni wanangu kuleni wanangu sikuku yenu hii" hadi anamalizia wanawe wanaambulia vipapatio na mchuzi tuu huku yeye akifaidi wali wa kuku.
 
kwenye hili Mzee Mwanakijiji amesherehesha...........nimependa sana maono yake yenye busara Ujinga hasara.......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom