Kitabu cha My American Experience Ndio kitabu bora kwa mwaka 2018

Per Diem

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
2,191
3,710
Heshima zenu wadau wa Jf, niseme ukweli mm ni mmoja wa watu ambao tulikuwa tunabeza sana kitabu cha My American Experience kilichoandaliwa na kuandikwa na William Malecela.
Nilipata uthubutu wa kukinunua na kusoma yaliyomo ndani ili niweze kujifunza na pengine kuniongezea maarifa ya kukabiliana na maisha ya kila siku.
Niwe tu muwazi, Kitabu kimeandikwa kwa ustadi na ufundi mkubwa sana huku stori ikiwa imepangiliwa kwelikweli. Na nimejifunza mengi sana mazuri, hakika Lemutuz ni mpiganaji haswa.
Kwa mwaka huu 2018 nimenunua vitabu 7 lakini kitabu bora kabisa ni cha My American Experience.
Nisikuchoshe, usinichoshe nenda kanunue na usome mstari kwa mstari
 
Mi nilisoma tu yale maandiko yaliyokuwa yanaletwa humu na wadau toka Instagram kweli ni kitabu kizuri na jamaa na fighter wa ukweli ukweli!!
 
mi nasoma sana vitabu ila nasoma vya kama kina mengi ivi au dewji ila eti nisome kitabu cha le mutuz sitak kuambukizwa ujinga na yule mzee wakati nikiwa bado kijana
Soma tu na hicho mkuu utapata la kujifunza maana kama kijana kila siku unatakiwa ujifunze (elimu bahari) huyu William kaona na kupitia mengi huenda ukaona linalokufaa ukajifunza.
 
Lemtumboz kitabu kimedoda ameamua kuja na ID fake kukinadi
 
Nnacho now nipo ukurasa wa 50,hakika jamaa anamengi sana ambayo vijana inabidi tujifunze toka kwake ningekiweka hapa but siyo vizuri ntakuwa navunja sheria na kumrudisha nyuma mwenzetu,pia nmemaliza juzi cha ujasusi wa kidola hakika dunia ina mengi sijajutia kuvinunua hivi vitabu japo nmetumia pesa ndefu kuvinunua
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom